Friday, April 14, 2017

PIGO BAYERN, BOATENG, HUMMELS PANCHA.

MABEKI wa Bayern Munich Jerome Boateng na Mats Hummels wameondolewa katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Bayer ya Bayer Leverkusen unaotarajiwa kuchezwa kesho. Hummels alipata matatizo ya kifundo cha mguu na kumfanya kukosa mchezo wa robo fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo walifungwa mabao 2-1 na Real Madrid juzi. Meneja wa Bayern ameithibitisha kuwa Boateng anasumbuliwa na tatizo la misuli na anatarajia kutomtumia mwishoni mwa wiki hii, ingawa ana matumaini atakuwa tayri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Madrid wiki ijayo. Akizungumza na wanahabari, Ancelotti alithibitisha taarifa hizo za kuwakosa nyota wake hao kesho na kubainisha kuwa atawatumia David Alaba katikati na Juan Bernat upande wa kushoto wa safu yake ya ulinzi.

OZIL KUJUA MUSTAKABALI WAKE MWISHONI MWA MSIMU.

KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil amedai kuwa hataki mazungumzo ya mkataba yakabugudhi kipindi hiki muhimu kuelekea mwishoni mwa msimu na anatarajia kusubiri mpaka Ligi Kuu itakapomalizika kabla ya kuzungumza mustakabali wake. Nafasi ya Ozil katika klabu hiyo limekuwa jambo jambo linalojadiliwa na vyombo vya habari nchini Uingereza huku taarifa zikidai nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye mkataba wake umebakiza chini ya kiezi 15, amekataa kusaini mkataba mpta utakaomuwezesha kupata paundi 250,000 kwa wiki. Arsenal kwasasa wanashikilia nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa alama saba nyuma ya nafasi nne za juu. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, Ozil amesema kwa kipindi hiki yeye sio muhimu sana kwani klabu ndio muhimu zaidi. Ozil aliendelea kudai kuwa bado wana kibarua kizito msimu huu hivyo anadhani sio sahihi kufikiria jambo linguine zaidi ya soka.

RONALDO AFURAHIA KUFIKISHA MABAO 100 ULAYA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hakuwa kufikiria kuwa siku moja angeweza kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 kwenye michuano ya Ulaya wakati anaanza, lakini anaona fahari na furaha kufikia mafanikio hayo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 alifikia idadi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata Madrid dhidi ya Bayern Munich juzi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alitunukiwa shati maalumu la kumbukumbu na rais wa Madrid Florentino Perez jana kufuatia mafanikio hayo aliyopata. Akikaririwa na tovuti ya klabu hiyo, Ronaldo amesema ni heshima kubwa kufikisha idadi ya mabao 100 Ulaya na juzi ilikuwa ni siku maalumu na ushindi muhimu. Ronaldo aliendelea kwa kuishukuru klabu kwa nafasi ya kipekee waliyompa, wachezaji wenzake na mashabiki kwa kumuunga mkono. Ronaldo alianza kufunga mabao Ulaya katika mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Debrecen Agosti mwaka 2005.

MOURINHO ATUPA LAWAMA KWA BEKI ZAKE.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amewalaumu washambuliaji wa kikosi chake kwa kukosa umakini baada ya Anderlecht kusawazisha dakika za mwisho na kupata sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Europa League. United walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Ubelgiji mpaka dakika ya 86, wakati wenyeji hao waliposawazisha kwa shuti lao la kwanza lililolenga lango la United. Akizungumza na wanahabari, Mourinho amesema kama angekuwa beki wa United ni wazi angekuwa amekasirika na washambuliaji walivyofanya. Mourinho aliendelea kudai kuwa mabeki walifanya kazi nzuri lakini watu waliostahili kumaliza mchezo walishindwa kufanya hivyo pamoja nafasi nyingi walizopata.

Thursday, April 13, 2017

DYBALA ASAINI MKATABA MPYA JUVENTUS.

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Paulo Dybala amesaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Italia ambao utamalizika mwaka 2022. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 amefunga mabao 16 kwa Juventus msimu huu na kulikuwa na tetesi zikimuhusisha na kuondoka. Dybala alijiunga Juventus kwa kitita cha paundi milioni 23 kutoka Palermo na kupewa mkataba wa miaka mitano Juni 2015 na kufanikiwa kushinda mataji mawili mwaka jana. Dybala amesema siku zote amekuwa akitaka kufanikiwa kwenye kila kitu na anafahamu Juventus ndio mahali sahihi kuwepo kama anataka kushinda mataji. Dybala amefunga mabao 39 na kusaidia mengine 16 kwenye mechi 82 toka ajiunge na Juventus, ikiwa ni dadi kubwa zaidi ya mchezaji yeyote katika klabu kwa muda aliojiunga.

RAIS WA SOKA WA ARGENTINA KUMFUATA MESSI HISPANIA.

RAIS wa Chama cha Soka cha Argentina-AFA, Claudio Tapia amesisitiza safari ya kwenda nchini Hispania ni mahsusi kwa ajili ya kwenda kujadili kesi ya Lionel Messi ya kufungiwa mechi nne na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, na sio kwenda kuzungumza na Jorge Sampaoli au Diego Simeone kuhusiana na kubarua cha kuinoa nchi hiyo. Messi alilimwa adhabu hiyo na FIFA baada ya kumtolea kauli chafu mwamuzi wakati wa ushindi wa bao 1-0 Argentina iliyopata dhidi ya Chile mwezi uliopita na kumfanya kukosa mchezo waliofungwa na Bolivia mabao 2-0 na nyingine tatu zijazo za kufuzu Kombe la Dunia. Nyota huyo wa Barcelona anayo nafasi ya kukata rufani ya kutaka kupunguzwa kwa adhabu hiyo mwezi ujao kitu ambacho Tapia alitaka kwenda kujadili naye ana kwa ana. Tapia amesema FIFA imemtaka Messi kupeleka shauri lake hilo la kufungiwa mechi nne baada ya mchezo wao dhidi ya Chile Alhamisi Mei 4 mwaka huu hivyo ilikuwa muhimu kwenda kujadiliana naye kuhusiana na hilo. Mchezo ujao wa Argentina utakuwa ni ule wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Brazil utakaofanyika nchini Australia Juni mwaka huu huku mechi za kufuzu Kombe la Dunia zikitarajiwa kuendelea Agosti.

UEFA YAKANUSHA KUPUUZA TAARIFA ZA KUTAKIWA KUSOGEZA MBELE MCHEZO WA DORTMUND NA MONACO.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limejibu tuhuma za kushindwa kuahirisha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco, ba kusisitiza hawakupata taarifa zozote kuwa timu hizo hazikutana kucheza. Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali uliahirishwa Jumanne baada ya basi la timu ya Dortmund kushambuliwa na milipuko wakati wakitoka hotelini kuelekea Signal Iduna Park. Mchezo huo ulikuja kuchezwa jana, lakini meneja wa Dortmund Thomas Tuchel alikuwa akihitaji muda zaidi ili wale waliokumbwa na tukio hilo waweze kusahau lakini alipuuziwa. Naye meneja wa Monaco Leonardo Jardim amekiri ilikuwa vigumu kwa wachezaji kuwa mchezoni baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wao wa jana. Msemaji wa UEFA, amesema uamuzi wa kusogeza mbele mchezo wa Dortmund na Monaco uliamuliwa kwa kushirikisha pande zote mbili. UEFA iliendelea kudai kuwa ilikutana na pande zote mbili na kamwe hawakupewa taarifa yeyote ya kusogeza mbele zaidi mchezo huo.