Monday, October 31, 2011

GERRARD HATARINI KUIKOSA HISPANIA NA SWEDEN.

Steven Gerrard akishuka katika gari huku akiwa na magongo mara baada ya kutoka Hospitali.

Liverpool inasubiri kufahamu ukubwa wa jeraha la Steven Gerrard baada ya nahodha huyo kuonekana na magongo ya kutembelea huku kifundo cha mguu kikiwa kimefungwa plasta.Gerrard hakucheza siku ya Jumamosi, Liverpool ilipoilaza West Brom mabao 2-0 kutokana na kuumia kifundo cha mguu, ikiwa ni hivi karibuni tu alipona matatizo ya nyonga.Alipigwa picha akitoka hospitali akiwa na magongo na kulikuwa na taarifa alitolewa maji katika kifundo hicho cha mguu.
Kuna wasiwasi Gerrard huenda asiweze kucheza katika mechi ambayo England itapambana na Hispania pamoja na Sweden mwezi wa Novemba mwaka huu. Nahodha huyo alisafiri na kikosi cha Liverpool hadi Black Country siku ya Ijumaa, lakini baadae kifundo cha mguu wake kikaanza kuvimba siku ya Jumamosi asubuhi na hivyo kutangazwa hataweza kucheza dhidi ya West Brom.

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA.



Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatavyo;




Oktoba 30-Kagera Sugar vs Azam (Uwanja wa Kaitaba)


Oktoba 30-Villa Squad vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)


Oktoba 30-Mtibwa Sugar vs Moro United (Uwanja wa Manungu)


Novemba 2-Oljoro JKT vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid)


Novemba 2-Moro United vs Simba (Uwanja wa Taifa)


Novemba 2- Polisi Dodoma vs Yanga (Uwanja wa Jamhuri)


Novemba 2-Toto Africans vs Azam (Uwanja wa CCM Kirumba)


Novemba 2-Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu)


Novemba 2- Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi)


Novemba 3- Kagera Sugar vs Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba)





LIGI DARAJA LA KWANZA





Mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatazo;


Kundi A


Oktoba 30- Morani vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Kiteto)


Oktoba 30- Transit Camp vs Burkina Faso (Uwanja wa Mkwakwani)


Oktoba 31- Temeke United vs Mgambo Shooting (Uwanja wa Mlandizi)


Kundi B


Oktoba 30- Mbeya City vs Small Kids (Uwanja wa Sokoine)


Oktoba 30- Majimaji vs Tanzania Prisons (Uwanja wa Majimaji)


Oktoba 31- Polisi Iringa vs Mlale JKT (Uwanja wa Samora)


Novemba 3- Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Samora)


Kundi C


Oktoba 31- 94KJ vs Manyoni (Uwanja wa Mlandizi)

ZIMBABWE KUANDAA AFRICA WOMEN CHAMPIONSHIP.

SHIRIKISHO la Soka la Zimbabwe-ZIFA- limekubali kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika ya wanawake itakayofanyika 2012.Shirikisho hilo hivi sasa linasubiria jibu kutoka serikalini kabla ya mwezi Novemba kwa ajili ya kuandaa michuano hiyo.Zimbabwe wamepewa nafasi hiyo na Shirikisho la Soka la Afrika- CAF- baada ya kuandaa kwa mafanikio michuano ya wanawake ya Cosafa iliyofanyika mwezi Julai mwaka huu.Ofisa Mkuu wa ZIFA amesema michuano hiyo itasaidia kupandisha kiwango cha soka cha nchi hiyo pamoja na kufungua milango kwa watalii kumiminika kuitembelea nchi hiyo.

POULSEN AITA 22 STARS.

Jan Poulsen
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars JAN POULSEN ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mchezo wa mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Chad utakaochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.Katika kikosi hicho POULSEN amewaita kwa mara ya kwanza Golikipa MWADINI ALLY wa Azam na kiungo SHOMARY KAPOMBE kutoka Simba. Kikosi kamili cha timu hiyo kwa upande wa makipa ni JUMA KASEJA na MWADINI ALLY Walinzi ni AGGREY MORRIS, JUMA NYOSO , IDRISSA RAJAB, ERASTO NYONI, NADIR HAROUB, GODFREY TAITA na JUMA JABU.
Mwadini Ally
Kwa upande wa viungo yupo HENRY JOSEPH ,NURDIN BAKARI ,SHABANI NDITI ,ABDI KASSIM ,RAMADHAN CHOMBO na SHOMARI KAPOMBE . Washambuliaji ni NIZAR KHALFAN, MRISHO NGASSA, MBWANA SAMATA , DAN MRWANDA, ATHUMAN MACHUPA, HUSSEIN JAVU pamoja na THOMAS ULIMWENGU. Timu hiyo itaingia kambini Novemba 3 Jijini Dar es Salaam huku ikitarajia kuondoka nchini Novemba 9 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 35 kwenda N’Djamena kwa ajili ya mchezo huo. Timu hizo zitarudiana Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

DRAW YA AFCON 2012.


Africa Cup of Nations 2012 Groups

Group A: Equatorial Guinea, Libya, Senegal, Zambia
Group B: Ivory Coast, Sudan, Burkina Faso, Angola
Group C: Gabon, Niger, Morocco, Tunisia

Group D: Ghana, Botswana, Mali, Guinea


BALE AIPAISHA TOTTENHAM.

MABAO mawili ya Gareth Bale yalihakikishia ushindi Tottenham Hotspurs wa mabao 3-1 dhidi ya Queens Park Rangers na kuifanya timu hiyo kucheza mchezo wa saba mfululizo bila kufungwa.Katika mchezo huo uliomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Spurs, Bale aliipatia timu yake bao la kuongoza kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Aaron Lennon. Spurs waliendeleza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao ambapo Rafael van der Vaart aliweza kuvunja mtego wa kuotea na kuachia mkwaju uliompita mlinda mlango wa QPR Paddy Kenny baada ya kuuwahi mpira uliokuwa umepigwa na Ledley King
QPR walichachamaa kipindi cha pili na Jay Bothroyd aliyeingia kipindi hicho aliweza kurudisha uhai kwa timu yake kwa kufunga bao la kichwa karibu kabisa na lango.Msumari wa mwisho katika jeneza la QPR ulipigiliwa na Bale katika dakika ya 72, kwa matokeo hayo Spurs wamechupa hadi nafasi ya tano mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa wamefungana pointina Chelsea na Newcastle.

TIMU YA BECKHAM ILIVYOWAADHIBU WAKIINA HENRY.

MATUKIO MBALIMBALI YA MCHEZO BAINA YA LA GALAX NA NY RED BULL.

David Beckham wa Los Angeles Galax na Thiery Henry wa New York Red Bull wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya timu hizo ulichezwa jana usiku huko Marekani, LA Galax ilishinda bao 1-0 katika mchezo huo.

Henry akimkwatua Beckham katika mchezo.

Mchezaji wa LA Galax Robbie Kean akiwa kazini.

Wachezaji wa timu zote mbili wakizozana mara baada ya kipenga cha mwisho kupigwa.

Beckham akiwa na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Saturday, October 29, 2011

SIMBA, YANGA HAPATOSHI LEO. CHELSEA, ARSENAL NAO VITANI.


MACHO na masikio ya watanzania yataelekea katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam ambapo mtanange wa kukata na shoka katika mahasimu wawili Simba na Yanga zitakapochuana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Simba ambao wanaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 27 katika michezo 11 waliyocheza wataingia uwanjani huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wa kwanza wa ngao ya jamii dhidi ya watani wa jadi.Yanga ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo wenyewe walianza ligi hiyo kwa kusuasua kabla ya kuzinduka kipindi cha hivi karibuni wako katika nafasi ya pili mwa msimamo wakiwa wamejikusanyia pointi 21 katika michezo 11 waliyocheza hivyo mchezo huu utakuwa ni muhimu kwao kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake.

Na kimataifa huko Uingereza wapenzi wa soka wataelekeza masikio yao katika Uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea wataikaribisha Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.Mbali na mchezo huo michezo mingine itakayochezwa leo itakuwa, Everton itaikaribisha Manchester United, Manchester City na Wolveshampton, Norwich na Blackburn, Sunderland na Aston Villa, Swansea na Bolton, wigan na Fulham wakati West Bromwich wataikaribisha Liverpool.

KENYA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WA SOKA.


UCHAGUZI wa uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu wa kuchagua viongozi wapya soka nchini Kenya unatarajiwa kufanyika leo baada ya kuahirishwa zaidi ya mara tatu.Wagombea nane wanatarajiwa kugombea nafasi za juu wakiwemo Mohammed Hattimy, Sam Nyamweya, Elizabeth Shako, Hussein Mohammed, Sammy Joel Obingo, Ambrose Rachier na Ally Twaha.Wagombea wamekuwa wakijinadi tofauti kwa wapiga kura wao ambapo Nyamweya amejinadi kuwa wakati alipokuwa kiongozi nchi ilikuwa katika nafasi za 68 na 70 katika viwango vya FIFA tofauti na ilivy hivi sasa.Hivi sasa nchi hiyo iko katika nafasi ya 135 katika viwango vya ubora vya FIFA.

"ROONEY NI MSALITI KWA EVERTON." FERGUSON.

KOCHA wa Manchester United Sir Alex Feguson anaamini kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney siku zote bado anaonekana msaliti mbele ya mashabiki wa Everton ambao hawajamsamehe kwa kitendo chake kuihama klabu yake hiyo ya utotoni mwaka 2004.Akizungumza kabla ya mchezo wao wa leo dhidi ya timu hiyo katika Uwanja wa Goodison Park, Ferguson alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hawezi kusahaulika kwa kuikacha klabu hiyo kuelekea Old Traford kwa kitita cha paundi milioni 25 miaka saba iliyopita.Ferguson amesema hadhani kama wachezaji wa timu hiyo watamsumbua kwakuwa hakujawahi kutokea kitu kama hizo wakicheza na Everton huwa anaelewana nao vyema tu.Amesema tatizo liko kwa mashabiki kwakuwa huwa wanamuona ni msaliti na hilo haliweza kubadilika, na hilo huwa linajidhihirisha akifunga bao dhidi ya timu hiyo kwani mashabiki huwa wanamzomea.

TOURE KIKAANGONI TENA.


MLINZI wa Manchester City Kolo Toure ataikabili kamati ya nidhamu ya klabu hiyo wiki ijayo kuhusiana na suala la kugundulika alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu mapema mwaka huu.
Tume binafsi ya nidhamu mwezi wa Mei ilimfungia Toure kucheza kandanda kwa muda wa miezi sita, ingawa shauri hilo lilitokea tangu mwezi wa Machi, baada ya vipimo alivyofanyiwa kuonesha alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu ambazo zimekatazwa.
Tangu aliporejea uwanjani mwezi wa Septemba ameshacheza mechi nne.
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ataendelea kubakia katika ushindani mkubwa kuweza kupata nafasi ya kucheza.
Kusikilizwa kwa shauri hilo kulicheleweshwa hadi sasa kwa sababu wajumbe wa kamati hiyo ya sheria walishindwa kupanga tarehe muafaka.
Mchezaji mwenzake Toure, Carlos Tevez, ambaye alipatikana naonekana na hatia ya kukiuka vifungu vitano vya mkataba wake wiki hii, alifanya mazoezi mbali na wachezaji wa kikosi cha kwanza na hajacheza mechi yoyote ya maana wakati shauri lake lilipokuwa likiendelea likisikilizwa.
Lakini Mancini amesema suala la Toure ni tofauti. Ilikuwa ni makosa..
Toure, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2013, alisimamishwa kucheza soka baada ya kutumia dawa za kupunguza uzito za mkewe.
Alifanyiwa vipimo mwezi wa Februari wakati Manchester City ilipopambana na Manchester United ambapo alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakucheza, na alisimamishwa tarehe 3 mwezi wa Machi baada ya sampuli kuonesha ametumia dawa zilizokatazwa.