Wednesday, October 31, 2012
ARSENAL 7 READING 5.
KLABU ya Arsenal jana imefanikiwa kupigana kiume baada ya kuwa nyuma kwa mabao 4-0 mpaka muda wa mapumziko na kufanikiwa kushinda kwa mabao 7-5 katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Reading katika Uwanja wa Madejski. Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alikaririwa wiki iliopita akisema kuwa michuano hiyo anaipa umuhimu wa mwisho katika malengo yake msimu huu ambapo kauli yake ingetimia kama ukuta wa Reading ungekuwa imara baada ya timu hiyo kuongoza kwa mabao 4-0 katika dakika 37 za mchezo huo. Mara baada ya ushindi huo Reading ambao wanashika wanashika nafasi ya tatu kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza walishindwa kuhimili vishindo vya Arsenal baada ya nyota wake Theo Walcott kuipatia bao la kuongoza kabla ya mapumziko na baadae kufunga mengine mawili. Wenger aliwapongeza vijana wake kwa kutokata tamaa pamoja na kukubali wavu wao kutikiswa mara nne na kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mchezo huo muhimu.
FA YASUBIRI TAARIFA KUTOKA SERBIA JUU YA KUFUNGIWA WACHEZAJI WAKE KUTOKANA NA VURUGU.
CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimethibitisha kuwa hawajapewa taarifa juu ya uamuzi wa maofisa wa polisi nchini Serbia kuwahusisha wachezaji wawili wa timu ya taifa chini ya miaka 21 ya Uingereza kwa vurugu. Shirikisho la Soka nchini Serbia liliwafungia viungo Nokla Ninkovic na mshambuliaji Ognjen Mundrinski kucheza katika timu za taifa lakini mamlaka ya kisheria ilitangaza kuwashitaki watu 12 katika vurugu hizo yakiwemo majina mawili ya Uingereza. Katika taarifa ya FA ilithibitisha kuwa hawajapata taarifa rasmi zozote kuhusu kufungiwa kwa wachezaji wake na shirikisho la soka ya Serbia na kwamba wanasubiri maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo. Taarifa hiyo ilimalizwa kwa kusema FA itawapa msaada wachezaji pamoja na viongozi waliokumbana na sakata hilo nchini Serbia wiki mbili zilizopita.
DJOKOVIC AJIHAKIKISHIA KUMALIZA NAMBA MOJA.
MCHEZA tenisi nyota kutoka Serbia, Novak Djokovic amejihakikishia nafasi ya kumpita mpinzani wake Roger Federer na kumaliza mwaka 2012 akiwa kinara katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume. Djokovic alipoteza nafasi yake hiyo kwa Federer mwenye umri wa miaka 31 baada ya kunyakuwa michuano ya Wimbledon lakini Federer ambaye anatoka Switzerland hataweza kutetea taji la Paris Masters. Kutokuwepo kwa Federer katika michuano hiyo mikubwa ya dunia ya mwisho kwa mwaka huu ambayo itafanyika Novemba 5 kunampa nafasi Djokovic kurejea katika kiti chake. Djokovic mwenye umri wa miaka 25 anakuwa nyota wa kwanza kumaliza mwaka katika nafasi ya kwanza mfululizo toka Federer alipofanya hivyo kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007.
Tuesday, October 30, 2012
ORODHA YA WACHEZAJI NA MAKOCHA AMBAO WATAGOMBEA BALLON D'OR.
Players (in alphabetical order):
Sergio Aguero (Argentina), Xabi Alonso (Spain), Mario Balotelli (Italy), Karim Benzema (France), Gianluigi Buffon (Italy), Sergio Busquets (Spain), Iker Casillas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Didier Drogba (Ivory Coast), Radamel Falcao (Colombia), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Spain), Lionel Messi (Argentina), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Mesut Ozil (Germany), Gerard Pique (Spain), Andrea Pirlo (Italy), Sergio Ramos (Spain), Wayne Rooney (England), Yaya Toure (Ivory Coast), Robin van Persie (Netherlands), Xavi (Spain).
Coaches (in alphabetical order):Vicente del Bosque (Spain/Spain national team), Roberto Di Matteo (Italy/Chelsea), Alex Ferguson (Scotland/Manchester United), Pep Guardiola (Spain/Barcelona former coach), Jupp Heynckes (Germany/Bayern Munich), Jurgen Klopp (Germany/Borussia Dortmund), Joachim Low (Germany/Germany national team), Roberto Mancini (Italy/Manchester City), Jose Mourinho (Portugal/Real Madrid), Cesare Prandelli (Italy/Italy national team)
Sergio Aguero (Argentina), Xabi Alonso (Spain), Mario Balotelli (Italy), Karim Benzema (France), Gianluigi Buffon (Italy), Sergio Busquets (Spain), Iker Casillas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Didier Drogba (Ivory Coast), Radamel Falcao (Colombia), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Spain), Lionel Messi (Argentina), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Mesut Ozil (Germany), Gerard Pique (Spain), Andrea Pirlo (Italy), Sergio Ramos (Spain), Wayne Rooney (England), Yaya Toure (Ivory Coast), Robin van Persie (Netherlands), Xavi (Spain).
Coaches (in alphabetical order):Vicente del Bosque (Spain/Spain national team), Roberto Di Matteo (Italy/Chelsea), Alex Ferguson (Scotland/Manchester United), Pep Guardiola (Spain/Barcelona former coach), Jupp Heynckes (Germany/Bayern Munich), Jurgen Klopp (Germany/Borussia Dortmund), Joachim Low (Germany/Germany national team), Roberto Mancini (Italy/Manchester City), Jose Mourinho (Portugal/Real Madrid), Cesare Prandelli (Italy/Italy national team)
NINA NDOTO ZA KUSTAAFU SOKA NIKIWA BARCELONA - MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa ana ndoto za kustaafu kucheza soka akiwa katika klabu hiyo ambayo imemfundisha toka mdogo na kuanza rasmi kucheza soka la kulipwa 2004. Kauli ya nyota huyo imekuja wakati akipokea tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyopewa kufuatia kuongeza orodha ya wafungaji barani Ulaya msimu uliopita akiwa na mabao 50. Messi aliishukuru Barcelona kwa kumoa nafasi ya kutambua kipaji chake wakati walipomchukua katika shule yao ya michezo akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2000. Messi mwenye umri wa miaka 25 sasa ana mkataba wa miaka minne ambao una thamani ya paundi milioni 250 na maofisa wa klabu hiyo wamesema kuwa wako tayari kuuboresha zaidi mkataba huo. Mpaka sasa nyota huyo ameshafunga mabao 270 kwa klabu yake hiyo na 31 kwa timu ya taifa ya Argentina.
WAZIRI MKUU SENEGAL AMTAKA RAIS WA FSF KUJIUZULU.
WAZIRI Mkuu wa Senegal, Abdoul Mbaye amemtaka rais wa Shirikisho la Soka la Senegal-FSF Augustin Senghor kujiuzulu wadhfa wake huo kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya nchi hiyo na Ivory Coast. Maofisa watatu wa juu wa shirikisho hilo walijiuzulu Jumatatu ikiwa ni wiki moja toka makamu wa rais Lamotte Louis kujitoa katika kamati ya utendaji baada ya kukubali kuwajibika kwa vurugu zilizotokea uwanjani. Hatahivyo, Senghor alikataa kujiuzulu baada ya kujitetea kuwa serikali ilikuwa ikiingilia mambo yao ya michezo. Akihojiwa Senghor amesema kuwa haoni haja ya kujiuzulu kwani hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kuwalazimisha kujiuzulu kwasababu walichaguliwa kihalali na muda wao wa kukaa madarakani bado haujakwisha. Senghor aliendelea kusema kuwa ataitisha mkutano wa dharura kesho kwa wajumbe 23 wa kamati ya utendaji waliobakia ili kuziba pengo la wajumbe wanne waliojiuzulu.
Sunday, October 28, 2012
KUVUNJA REKODI YA PELE SIO MUHIMU KWANGU - MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa kuvunja rekodi ya Pele kwa kufunga mabao mengi zaidi katika mwaka mmoja haina umuhimu sana kwake kulinganisha na kuisaidia timu yake kupata mafanikio zaidi. Messi alifunga mabao mawili na kufikisha mabao 73 kwa mwaka huu katika mchezo dhidi ya Rayo Vallecano jana na kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwafikia nguli wa zamani Pele ambaye alifunga mabao 75 na Gerd Mullaer aliyefunga mabao 85. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi amesema kuwa kuvunja rekodi ya Pele sio suala la umuhimu sana kwake kwani wameshinda mchezo huo katika mazingira magumu na hilo ndio suala la umuhimu zaidi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kupewa kiatu chake cha dhahabu Jumatatu baada ya kumaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora Ulaya ambapo aliwashukuru wachezaji wenzake kwani bila wao asingeweza kupata zawadi hiyo.
NITAKUWA MVUMULIVU KWA WILSHERE - WENGER.
MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema atakuwa mvumilivu juu ya ujio Jack Wilshere baada ya kiungo huyo kucheza mechi yake ya kwanza baada ya miezi 17 wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Queens Park Rangers jana. Wilshere ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na kifundo cha mguu alicheza kwa dakika 67 katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Emirates baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza pasipo kutegemewa na Wenger. Wenger alionyesha kufurahishwa na kiwango alichokionyesha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza baada ya kuweka wazi kuwa hakumwambia Wilshere kama atacheza mchezo huo mpaka asubuhi. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa atakuwa akimtumia mchezaji huyo kwa tahadhari wakati akiendelea kurejea katika kiwango chake cha kawaida na amemuondoa katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa Kombe la Ligi dhidi Reading katikati ya wiki hii.
MECHI YA MAHASIMU YA LUPOPO NA MAZEMBE YASOGEZWA MBELE KUTOKANA NA VURUGU.
WATU watano wakiwemo polisi wawili wameumia vibaya wakati vurugu zilipozuka kabla ya mchezo wa Jumamosi jijini Lubumbashi ambao unawakutanisha mahasimu wawili timu za Saint-Eloi Lupopo na TP Mazembe mchezo ambao uliahirishwa kutokana na vurugu hizo. Taarifa ya polisi imesema kuwa maofisa wawili wa polisi na mashabiki watatu ndio walioumia sana lakini wapo mashabiki wengine wengi ambao walipata majeraha ya kawaida katika kdhia hiyo. Mashuhuda wanasema kuwa vurugu hizo zilizuka wakati mashabiki wa timu zote mbili walipoanza kurushiana mawe kabla ya polisi kuingilia na kuwarushia mabomu ya machozi ili kujaribu kutuliza vurugu hizo. Matukio ya vurugu sasa imeonekana kuwa kama tabia za kawaida kwa mashabiki wa soka barani Afrika baada ya kutokea kwa matukio ya aina hiyo mara kwa mara huku mengine yakichukua maisha ya watu.
LORENZO BINGWA MICHUANO YA MOTOGP.
DEREVA nyota wa mashindano ya pikipiki, Jorge Lorenzo amejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la pili la dunia la michuano ya MotoGP baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya michuano ya Australian GP. Casey Stoner wa Autralia ndio aliyeshinda mbio hizo zilizofanyika katika kisiwa cha Philip kwa mara sita mfululizo lakini dereva mwenzake kutoka timu ya Respol Honda, Dani Pedrosa akipata ajali katikati ya mashindano hayo. Pedrosa ambaye alikuwa akihitaji kumaliza mbele ya mhispania mwenzake Lorenzo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la dunia katika mashindano hayo ya mwisho kwa maka huu alipata ajali katika mzunguko wa pili. Lorenzo ambaye ni dereva wa Yamaha mara ya kwanza alishinda taji la dunia mwaka 2010.
WILLIAMS, SHARAPOVA KUKWAANA FAINALI WTA.
WANADADA nyota wa mchezo wa tenisi, Serena Williams na Maria Sharapova wanatarajiwa kukutana katika mchezo wa fainali ya michuano ya WTA jijini Istanbul baadae leo. Williams kutoka Marekani ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake alifanikiwa kutinga fainali baada ya kumfunga Agnieska Radwanska kwa 6-2 6-1 akitumia muda wa dakika 61. Sharapova ambaye anashika namba mbili alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumfunga mwanadada namba moja katika orodha hizo Victoria Azarenka kwa 6-4 6-2. Azarenka ambaye alijihakikishia nafasi ya kumaliza mwaka akiwa katika namba moja baada ya kumfunga Li Na wa China katika mchezo huo alionekana kupata majeraha katika mguu wake kulia hivyo kushindwa kuhimili vishindo vya mpinzani wake. Sharapova bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa leo aaingia uwanjani akitafuta taji lake la pili la michuano hiyo ambayo mara ya mwisho alinyakuwa mwaka 2004 lakini atakumbana na wakati mgumu kwa Williams ambaye ameshinda taji hilo mara sita na sasa yuko katika kiwango cha juu kabisa.
Friday, October 26, 2012
RATIBA YA NAKUNDI ULAYA YASOGEZWA MBELE.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeamua kusogeza mbele upangwaji wa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Europa League hatua ya mtoano. Shughuli hiyo kwa kawaida ilitakiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu lakini wamesogeza mbele kwa siku sita zaidi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao imesema kuwa ratiba ya hatua ya mtoano ya michuano hiyo ya Ulaya 2012-2013 ambayo kwa kawaida hufanyika Desemba 14 sasa imesogezwa mbele mpaka Alhamisi Desemba 20 katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Nyon, Switzerland. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika katika Uwanja wa Wembley jijino London Uingereza May 25 mwakani huku fainali ya Europa League yenyewe itafanyika jijini Amsterdam, Uholanzi katika Uwanja wa ArenA 10 siku kumi baadae.
NITASHIKANA MIKONO NA TERRY - ROBERTS.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Reading Jason Roberts amesema kuwa atashikana mikono na John Terry lakini amekataa kuweka wazi kama anafikiri nahodha huyo wa Chelsea ni mbaguzi. Terry ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza amefungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 baada ya kukutwa na hati ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Anton Ferdinand wa Queens Park Rangers mwaka jana. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Roberts amesema kuwa atashikana mikono na Terry lakini alipoulizwa kama anadhani beki huyo ni mbaguzi alikwepa swali hilo na kurudia sentensi yake ya kwanza. Ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka kutokea kwa tukio hilo la Terry lakini kumekuwa na muendelezo wa matukio ya aina hiyo sehemu tofauti likiwemo tukio la mwezi ambapo beki wa timu ya vijana wa miaka chini ya 21 ya Uingereza Danny Rose alianyiwa vitendo vya kibaguzi wakati wa mechi nchini Serbia. Roberts aliungana na wachezaji wengine weusi nchini Uingereza wakiwemo Rio na Anton Ferdinand kutovaa tisheti za kampeni ya kutokomeza ubaguzi michezoni wakidai kusuasua kwa juhudi za kupiga vita suala hilo.
VETTEL AJITENGENEZEA NAFASI NZUR YA KUNYAKUWA TAJI LA INDIAN GRAND PRIX.
DEREVA nyota wa mbio za magari za Langalanga, Sebastian Vettel amefanikiwa kupata nafasi ya kwanza kabla ya kuanza kwa michuano ya Indian Grand Prix nafasi ambayo imemuweka katika nafasi nzuri ya kushinda mashindano hayo kwa mara ya nne mfululizo Jumapili. Vettel mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ujerumani kutoka timu ya Redbull ambaye anaongoza orodha ya madereva bora kwa alama sita zaidi ya Fernando Alonso wa timu ya Ferrari alitumia muda mzuri wa dakika moja na sekunde 27. Dereva wa timu ya MacLaren Jenson Button alishika nafasi ya pili katika mbio hizo huku Alonso akikamata nafasi ya tatu na nafasi ya nne kwenda kwa Lewis Hamilton wakati tano bora ilifungwa na dereva mwenzake Vettel wa timu ya Redbull Mark Webber. Mashindano hayo yatafanyika ramsi Jumapili huku Vettel akipambana vilivyo kuhakikisha anashinda na kujiongezea alama ili aweze kuwa bingwa wa dunia mwishoni mwa msimu huu ambao kumebakiwa na mshindano manne pekee.
Thursday, October 25, 2012
TANZIA NGUMI.
KOCHA Emanuel Steward ambaye amewafundisha mabondia nguli kama Thomas Hearns, Lennox Lewis na Wladimir Klitschko amefariki dunia akiwa na miaka 68. Alianza kujizolea umaarufu wakati alipokuwa akifundisha jijini Detroit ambapo Hearns aliyekuwa mwanafunzi wake alipokuwa bingwa wa dunia mwaka 1980. Steward ambaye ni raia wa Marekani ndio bondia aliyefundisha mabondia wengi zaidi ambao ni mabingwa wa dunia kuliko kocha yoyote wa mchezo huo na alifanya kazi na bingwa wa uzito wa juu Klitschko Julai mwaka huu. Klitschko alituma salamu zake za rambirambi kwa Steward akimuelezea kama mwalimu bora wa mchezo huo kupata kutokea na kwamba ulimwengu wa masumbwi umempoteza mtu muhimu. Steward ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ya utumbo pia aliwafundisha mabondia wakubwa kama Wilfred Benitez, Julio Cesar Chavez, Oscar de la Hoya, Evander Holyfield, Mike McCallum na James Toney.
SEREA AMGARAGAZA TENA AZARENKA.
MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake mwanadada Victoria Azarenka amebakia katika mashaka kama atamaliza mwaka huu katika nafasi hiyo baada ya kufungwa na Serena Williams kwa mara ya tano katika vipindi tifauti walivyokutana mwaka huu. Azarenka ambaye anatoka Belarus alikubali kufungwa kwa 6-4 6-4 naWilliams kutoka Marekani katika michuano ya WTA inayofanyika jijini Istabul ambapo sasa itabidi ahakikishe anamfunga Li Na bingwa wa zamani wa michuano ya wazi ya Ufaransa kutoka China ili aweze kujihakikishia nafasi hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema kuwa alifanya mazoezi ya nguvu ili aweze kucheza vyema na anatarajia ataendlea kufanya vyema na kama ikishindikana atajaribu kufanya hivyo tena mwakani. Azarenka ambaye alifungwa na Williams katika michuano ya wazi ya Marekani mwezi uliopita alianza vyema mchezo huo kwa kuongoza katika seti ya kwanza lakini Williams ambaye naye alikuwa akicheza chini ya kiwango alikuja juu na kuhakikisha hapotezi mchezo huo muhimu.
MADRID, MILAN, CITY, ARSENAL ZAANGUKIA PUA CHAMPIONS LEAGUE.
KLABU za Real Madrid, Manchester City, Arsenal na AC Milan zimeshindwa kutamba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali vipigo katika michezo yao ya jana na kujiweka katika nafasi ngumu ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Timu za Ujerumani zilionyesha kiwango bora jana baada ya mabingwa wa Bundesliga Borussia Dortmund kuwafunga mabingwa mara tisa wa michuano hiyo Madrid kwa mabao 2-1 nyumbani wakati mahasimu wao Schalke 04 wenyewe walifanikiwa kupata ushindi ugenini kwa kuingamiza Arsenal kwa mabao 2-0. Mabingwa mara saba wa michuano hiyo Milan wameendelea kucheza kwa kiwango cha chini baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani kwa Malaga timu ambayo imekuwa ikisumbuliwa na ukata lakini wamekuwa wakifanya vyema katika kundi C wakiwa na alama nyingi zaidi. Mabingwa wa Ligi Kuu chini Uingereza, Manchester City ambao waliishia katika hatua ya makundi msimu uliopita nao wamejikuta wakijiweka tena katika nafasi ya hatari ya kutoka baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka Ajax Amsterdam na kujikuta wakishika mkia katika kundi D kwa kukusanya alama moja katika michezo mitatu.
IVORY COAST, TOGO, TUNISIA, ALGERIA KUNDI LA KIFO AFCON 2013.
WENYEJI wa michuano ya Mataifa ya Afrika 2013, Afrika Kusini itakata utepe wa michuano hiyo kwa kucheza na Cape Verde ambao waliwashangaza mabingwa wa zamani wa Afrika Cameroon na kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Morocco ambao watakuwa wenyeji wa michuano hiyo mwaka 2015 sambamba na Angola ndio wanakamilisha timu za kundi A. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Zambia wamepangwa kundi moja na Nigeria pamoja na Ethiopia na Burkina Faso katika kundi C huku kundi B likiwa na timu za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na Mali. Katika Kundi D ambalo wadau wengi wa mchezo wa soka wanasema ndio kundi la kifo lina timu za Ivory Coast, Togo, Tunisia na Algeria ambapo michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari 10 mwakani.
ETO'O AMPONDA SONG.
MSHAMBULIAJI nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o amemkosoa mchezaji mwenzake Alex Song kwa kudai kuwa hajafikia kiwango cha mchezaji nyota wa dunia. Eto’o mwenye umri wa miaka 31 ambaye anakipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini Urusi amekuwa na uhusiano usio wa kuridhisha na kiungo huyo wa Barcelona toka Song alipokataa kushikana mikono naye katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal mwaka uliopita. Akihojiwa na luninga moja nchini Ufaransa kama nyota hao wana mgogoro unaoendelea, Eto’o amesema kuwa hakuna mgogoro unaondelea kati ya nyota wawili kwani yeye ni mmoja wa wachezaji bora duniani na Song hata Cameroon sio mmoja wa wachezaji bora. Wachezaji hao walionekana kama wamshamaliza matatizo yao katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde lakini Eto’o ana wasiwasi kwamba hakutaweza kuwa na maridhiano baina yake na Song. Tetesi zinasema kuwa uhasama wa wachezaji umeongezeka kutokana na Song kutaka kumnyang’anya kitambaa cha unahodha Eto’o ambaye alifungiwa kwa miezi nane baada ya kushawishi wachezaji wenzake kugoma wakidai posho zao. Eto,o amenyakuwa tuzo ya mchezaji bora duniani mana nne huku akiwa ndiye mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika katika kipindi chote baada ya kufunga mabao 18.
Wednesday, October 24, 2012
UNITED YASUBIRI MKATAB MNONO WA NIKE.
Add caption |
Subscribe to:
Posts (Atom)