MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Corinthians Alexandre Pato amethibitisha kuwa Tottenham Hotspurs walishindwa ofa yao ya kutaka kumsajili katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Akihojiwa kuhisiana na hilo Pato amesema Tottenham waliwasiliana na Corinthians kuhusu uhamisho wake lakini yeye na wakala wake waliamua kuwa anahitaji kubakia hapo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil aliibukia barani Ulaya wakati akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 2007 wakati alipoifungia bao timu yake ya AC Milan katika mchezo wa Serie A dhidi ya Napoli. Pato alifanya vyema katika msimu wa 2010-2011 wakati alipoifungia Milan mabao 14 lakini aliporomoka ghafla baada ya kuanza kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara yaliyopelekea kuamua kurejea nchini kwao Brazil.
Thursday, October 31, 2013
UEFA YAMSAFISHA MWAMUZI HATEGAN.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limejiridhisha kuwa mwamuzi Ovidiu Hategan aliyechezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Manchester City na CSKA Moscow alifuata taratibu. Hatua hiyo imekuja kufuatia kiungo wa City Yaya Toure kulalamika kuwa alifanyiwa vitendo vya kibaguzi katika mchezo huo uliochezwa Octoba 23. Pamoja na UEFA kumsafisha mwamuzi lakini pia walitoa adhabu kwa CSKA kuchezwa bila ya mashabiki katika uwanja wao wa Khimki kwenye mchezo unaofuata wa michuano hiyo dhidi ya Bayern Munich Novemba 27 mwaka huu. Katika taarifa ya UEFA iliyotolewa katika mtandao wake imedai kuwa mwamuzi huyo alipopokea malalamiko alimfuata kamisaa wa mchezo kumuambia atoe tangazo uwanjani la kukanya tabia hiyo kama utaratibu unavyoelekeza. Kwa maana hiyo UEFA iliridhishwa na hatua alizofuata mwamuzi ingawa tatizo limeonekana kwa aliyekuwa msimamizi wa uwanja kwani hakutoa tangazo hilo baada ya kuona kelele hizo zimetulia.
FIFA YAIRUHUSU MISRI KUTUMIA UWANJA WAKE WA NYUMBANI.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeruhusu timu ya taifa ya Misri kucheza mchezo wake wa mkondo wa pili wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ghana katika jijini la Cairo pamoja na hofu ya hali ya usalama. Chama cha Soka cha Ghana-GFA kilituma maombi FIFA ya kutaka kutafutwa uwanja mwingine ambao utakuwa salama kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Novemba 19 mwaka huu. Hata hivyo, FIFA ilithibitisha jana kuruhusu mchezo huo uchezwe jijini Cairo baada ya wakaguzi kuhakikisha hali ya usalama. Mshindi katika mchezo huo wa mtoano atafuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil.
ANCELOTTI AMPONGEZA BALE.
KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesifu mchango wa Gareth Bale ambaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 7-3 iliyopata timu hiyo dhidi ya Sevilla jana. Katika mchezo huo Bale alianza kwa mara ya kwanza toka atue Santiago Bernabeu ambapo ndiye aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 13 kabla ya kufunga bao lingine kwa adhabu ndogo. Mabao mengine ya Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga matatu na Karim Benzema aliyefunga mawili. Ancelotti amesema alicheza vyema na kuonyesha kipaji cha hali ya juu alichonacho pamoja na kwamba imechukua muda kurudi katika kiwango chake kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yaliyokuwa yanamsumbua.
MADRID YAMNYEMELEA BENZEMA.
KLABU ya Real Madrid inajipanga kwa usajili wa dirisha dogo mwezi January kutumbukia kumnasa Luis Suarez wa Liverpool kwa dau la paundi milioni 20 pamoja na mshambuliaji Karim Benzema. Suarez bado inaelezwa anataka kuondoka Anfield, licha ya mwanzo mzuri wa msimu kwa Liverpool. Arsenal nao wanajipanga kwa dau lingine baada ya kutolewa nje kwenye usajili uliopita wa majira ya joto. Lakini Suarez inaonekana anapenda zaidi kwenda Real Madrid inayofundishwa na Carlo Ancelotti na wakali hao wa Hispania wana matumaini ya kuwashawishi Liverpool kwa kuwapa fedha na mchezaji mwenye jina kubwa Benzema.
Tuesday, October 29, 2013
FLETCHER AREJEA TENA UWANJANI BAADA YA KUKOSEKANA KWA MIEZI 10.
KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester United, Darren Fletcher amevaa jezi ya klabu hiyo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita baada ya kupoana vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua. Fletcher ambaye alikosa mechi nyingi msimu uliopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua alicheza dakika 67 katika mchezo wa vijana wa chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya Fulham ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Fletcher alianza mazoezi rasmi katikati ya Septemba na muda si mrefu anaweza kurejea katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kama hali yake ikiimarika. Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa AJ Bell uliopo Salford ulishuhudiwa na wengine wa zamani wa United kama David Beckham, Phil Neville na Nicky Butt.
FERNANDINHO AIPA NAFASI BRAZIL KUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA.
KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Brazil, Fernandinho ameipa nafasi timu ya taifa ya nchi hiyo kunyakuwa taji la Kombe la Dunia mwakani litakalofanyika katika ardhi ya nchi yao. Uhamisho wake kwenda Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya Manchester City akitokea Shakhtar Donetski umechukuliwa kama sehemu ya kunyanyua nafasi yake kama mchezaji wa kati katika timu ya taifa. Ambapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 anadhani michuano hiyo kuchezwa katika ardhi ya nyumbani kwao ni nafasi nzuri kwao kubakisha taji hilo hapohapo. Fernandinho amesema kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani ni kitu ambacho hakijashuhudiwa kwa kipindi kirefu hivyo itakuwa ni nafasi ya kuonyesha ubora wao.
VAN PERSIE AMTABIRIA MAKUBWA JANUZAJ.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Robin van Persie anaamini kuwa mchezaji mwenzake anayechipukia Adnan Januzaj ana uwezo wa kuja kuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani. Kinda huyo mwenye miaka 18 ameanza vyema msimu huu kwa kuisadia United kutoka nyuma na kushinda mchezo dhidi ya Sunderland mapema mwezi huu huku akisaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo. Akihojiwa Van Persie amesema binafsi ni mshabiki wa kinda huyo na anadhani ana kitu za ziada kitakachomfanya kuwa nyota baadae. Van Persie aliyeondoka Arsenal mwaka jana kujiunga na United aliendelea kudai kuwa kwa miaka kadhaa ameshuhudia wachezaji mbalimbali vijana wanavyoibuka hivyo hana shaka kwamba Januzaj atakuja kuisaidia United kiasi kikubwa katika siku za usoni.
MOURINHO KUREJEA CHELSEA HALIKUWA JAMBO LA KUSHANGAZA.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa hakushangazwa kuona Jose Mourinho akirejea katika klabu ya Chelsea, kauli ambayo imekuja wakati ambapo wawili wanatarajia kukutana tena katika mchezo wa Kombe la Ligi itakayofanyika Uwanja wa Emirates baadae leo. Arsenal wameshinda mechi zao tisa kati ya 10 walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini Wenger bado hajawahi kuifunga timu ambayo inanolewa na Mourinho. Wakati Mourinho alipotua Chelsea kwa mara ya kwanza alikuwa akiingia katika mzozo wa mara kwa mara na Wenger lakini meneja huyo alisistiza kuwa hilo sio tatizo tena na ana furaha kumuona amerejea tena. Wenger amesema halikuwa jambo la kungaza kumuona kocha huyo amerudi kwasababu ni suala ambalo lilikuwa likizungumziwa mara kwa mara.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
PAMBANO LA SIMBA, AZAM LAINGIZA MIL 64/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 64,261,000. Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45. Wamiliki wa uwanja walipata sh. 7,599,747.49, gharama za mchezo sh. 4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh. 4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.
SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA ALHAMISILigi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 keshokutwa (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro). Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

UNITED ITANYAKUWA UBINGWA WA LIGI - FERGUSON.
MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema klabu hiyo itajirudi baada ya kuanza vibaya na kushinda taji la Ligi la Kuu nchini Uingereza pamoja na kuwa nyuma ya vinara Arsenal kwa alama nane. Ushindi mara mbili iliyopata United katika mechi zao tatu zilizopita inamaanisha kuwa timu hiyo inayonolewa na David Moyes imeanza kurejea katika kiwango chake cha kawaida. Ferguson mwenye umri wa miaka 71 amesema United imewahi kuanza vibaya mara nyingi lakini ndio timu pekee inayoweza kutoka nyuma na kushinda taji la ligi kwasababu ya historia yao. Ferguson ambaye ambaye amebakia kama mkurugenzi wa klabu hiyo, alistaafu nafasi ya ukocha mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kushinda mataji 38 katika miaka 27 aliyokuwepo hapo.
MESSI, RIBERY, RONALDO WAONGOZA ORODHA YA BALLON D'OR.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetoa orodha ya wachezaji 23 watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or. Miongoni mwa wachezaji waliopo katika orodha hizo ni pamoja na Lionel Messi ambaye anashikilia taji hilo aliloshinda mwaka jana, Franck Ribery wa Bayern Munich na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. Bayern ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu uliopita ndio waliotoa wachezaji wengi zaidi katika orodha hiyo ambapo mbali na Ribery pia wapo Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer, Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger. Mapema Mwezi Desemba mwaka huu FIFA na France Football watatangaza orodha ya majina matatu watakaopata kura nyingi zaidi kabla ya mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa katika hafla itakayofanyika jijini Zurich, Januari 13 mwakani.
Orodha kamili ya wachezaji na timu wanazotoka ni Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris St-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris St-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).
Mbali na wachezaji pia ilitolewa orodha ya makocha watakaogombea tuzo ya kocha bora wa mwaka ambayo ni Carlo Ancelotti (Real Madrid CF), Rafael BenÃtez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson (Manchester United's former coach), Jupp Heynckes (Bayern Munich's former coach), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).

VIWANJA VYA KOMBE LA DUNIA MWAKANI KUKABIDHIWA KWA WAKATI.
WAZIRI wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo amesema viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao vitakuwa tayari kwa wakati uliopangwa Desemba mwaka huu. Rebelo aliwaambia waandishi wa habari nchini humo kuwa ana uhakika wa kukamilika kwa viwanj hivyo kwasababu bado hawajachelewa sana. Kauli ya waziri imekuja kufuatia wasiwasi uliokuwepo wa kukamilika kwa wakati kwa Uwanja wa Pantanal uliopo katika mji wa Cuiaba, na kudai kuwa uwanja huo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 85 hivyo hakuna shaka kwamba utaisha nje ya wakati uliopangwa. Rebelo pia amesema hadhani kuwa michuano hiyo itazongwa na maandamano kama ilivyokuwa michuano ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika Juni mwaka huu mwaka huu ambapo waandamanaji walikuwa wakilaumu serikali kutumia fedha nyingi katika michuano hiyo wakati bado huduma muhimu zinapatikana kwa tabu nchini humo.
Monday, October 28, 2013
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
KIM AITA 30 FUTURE YOUNG TAIFA STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya pili (Future Young Taifa Stars) kitakachoingia kambini Novemba 9 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji. Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kim kwenye kikosi hicho ambacho hukitumia kuangalia uwezo wa wachezaji kabla ya kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa. Kikosi hicho kamili ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars kinaundwa na; makipa Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Himid Mao (Azam), Issa Rashid (Simba), Ismail Gambo (Azam), John Kabanda (Mbeya City), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Said Moradi (Azam) na Waziri Salum (Azam). Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Farid Mussa (Azam), Haruni Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga), William Lucian (Simba). Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya (Mbeya City) na Paul Nonga (Mbeya City). Kim amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager chenyewe kitaingia kambini Novemba 12 jijini Dar es Salaam ambapo siku inayofuata ndipo kitakapocheza mechi na Future Young Taifa Stars. Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa wakati Taifa Stars itaondoka Novemba 14 mwaka huu kwenda Arusha ambapo itaweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu. Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga). Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam). Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
PAMBANO LA THE TANZANITE LAINGIZA MIL 6/-Pambano kati ya timu ya Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (The Tanzanite) dhidi ya Msumbiji lililochezwa juzi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 6,190,000. Washabiki waliohudhuria mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika iliyomalizika kwa The Tanzanite kuibuka na ushindi wa mabao 10-0 walikuwa 5,003. Viingilio vilikuwa sh. 1,000, sh. 2,000, sh. 5,000 na sh. 10,000. Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 944,237.29, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,247,900, gharama za mchezo sh. 599,573 wakati wamiliki wa uwanja walipata sh. 449,679. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilipata sh. 149,893 huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likipata sh. 1,798,718. Mechi ya marudiano kati ya The Tanzanite na Msumbiji itachezwa kati ya Novemba 8 na 10 mwaka huu.
YANGA, MGAMBO KUUMANA UWANJA WA TAIFA VPLLigi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha raundi ya kumi na moja kesho (Oktoba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo. Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro). Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
EL MAAMRY KUONGOZA BODI YA TFFMkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umemteua Said Hamad El Maamry kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia mali za shirikisho. El Maamry ambaye kitaaluma ni mwanasheria na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ataongoza bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe watano. Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ambaye anakuwa Makamu Mwenyekiti, Dk. Ramadhan Dau, Mohamed Abdulaziz na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga.

MALINZI NDYE RAIS MPYA TFF, ATOA MSAMAHA.
JAMAL Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita. Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele. Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu. Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji. Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39). Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19). Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo. Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46). Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11). Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2). Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
VETTEL AFIKIA REKODI ZA KINA SCHUMACHER.
DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga kutoka timu ya Red Bull Sebastian Vettel ameeleza kuwa na furaha isiyo na kifani baada ya kufanikiwa kunyakuwa ubingwa wa duniani kwa mara ya nne mfululizo kwa kushinda mbio za Grand Prix za India Jumapili. Vettel ambaye ni raia wa Ujerumani anakuwa dereva wan ne kunyakuwa ubingwa huo kwa mara ya nne baada ya Juan Manuel Fangio, Alain Prost na Michael Schumacher na kufanya hivyo katika vipindi vyao. Akihojiwa Vettel amesema amekosa cha kuzungumza kwasababu ni moja ya siku ambazo anafuraha katika maisha yake. Dereva huyo ambaye ameshinda taji hilo huku kukiwa kumebaki mashindano matatu ya kumalizia msimu, aliendelea kudai kuwa imekuwa ni heshima kwake kushindana na baadhi ya madereva bora kabisa wa langalanga.
NILIKATAA KWA MAKUSUDI KUMPA MKONO MOURINHO - PELLEGRINI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema hakutaka kumpa mkono meneja wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata. Mourinho aliruka na kwenda kwa mashabiki kushangilia baada ya mshambuliaji Fernando Torres kuifungia Chelsea bao la ushindi katika dakika za majeruhi. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo Pellegrini amesema hakutegemea kitu tofauti kutoka kwa Mourinho ndio maana akaona haina haja ya kumpa mkono. Mourinho naye alijibu mapigo na kudai kuwa kama kuna mtu anafikiri alifanya vibaya kupanda jukwaani kushangilia na mashabiki anaomba radhi kwa hilo.
HAKUNA HAJA YA WAGHANA KUMTEGEMEA BOATENG - ZAKKOUR.
OFISA mkuu wa zamani wa klabu ya Heerts ya Ghana, Harry Zakkour amewataka mashabiki wa soka wan chi hiyo kumsahau kiungo mahiri wa timu ya taifa maarufu kama Black Stars Kevin-Prince Boateng. Uhusiano wa Boateng na mashabiki wa Black Stars umekuwa mashakani kufuatia jinsi alivyostaafu mwaka 2011 na kurejea tena miezi michache iliyopita lakini mpaka sasa ameshindwa kuichezea nchi hiyo mechi yoyote. Zakkour amesema nchi hiyo ina wacheza nyota wengi wanaoweza kuipeleka mbali hivyo hawana haja ya kuendelea kumuabudu mchezaji mmoja ambaye anaonyesha hana mapenzi nayo. Zakkour aliendelea kudai kuwa hana tatizo lolote na Boateng lakini hadhani kama mchango wake ni muhimu zaidi ya wachezaji waliopo sasa walivyoonyesha. Ghana watatakiwa kung’ang’ania ushindi wao wa mabao 6-1 waliopata dhidi ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza wakati watakapokwaana tena katika mchezo wa marudiano Novemba 19 ili waweze kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014.
PLATINI ATAKA NCHI 40 KOMBE LA DUNIA.
RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini anataka michuano ya Kombe ya Dunia kuongeza timu kufikia 40 kuanzia mwaka 2018 ili kuruhusu nchi zaidi kwa upande wa bara la Afrika na Asia kushiriki michuano hiyo bila kupunguza timu kutoka bara la Ulaya. Kwasasa Ulaya inaingiza timu 13 kati ya 32 kwenye mashindano hayo ukilinganisha na tano za Afrika na nne au tano zingine kutoka Asia bara ambalo lina watu wengi zaidi ulimwenguni. Wiki iliyopita rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter aliandika kuwa Afrika na Asia wanastahili kuwa na wawakilishi zaidi katika michuano hiyo kwasababu wana vyama vingi zaidi vya uwakilishi ukilinganisha na Ulaya na Amerika Kusini. Platini ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuikwaa nafasi ya Blatter amesema kwa mahesabu aliyopiga zikiongezeka timu nane itabidi michuano hiyo iongezwe siku tatu zaidi kitu ambacho sio kibaya. Platini aliendelea kudai kuwa anakubaliana kwa asilimia mia moja na hoja ya Blatter lakini badala ya kupunguza timu kutoka bara la Ulaya ni kuongeza timu kufikia 40.
TOURE AKUTANA NA WEBB.
KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amekutana na maofisa wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kujadili tuhuma kuwa alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika nchini Urusi wiki iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikutana na makamu wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb katika Uwanja wa Stamford Bridge siku ambayo City walifungwa na Chelsea kwa mabao 2-1. Msemaji wa City alithibitisha wawili hao kukutana lakini alikataa kuzungumzia masuala ambayo walijadili katika kikao chao. Webb pia ni rais wa CONCACAF na kiongozi wa kikosi kazi cha FIFA kinachopambana na masuala ya ubaguzi katika soka.
Sunday, October 27, 2013
ANCELOTTI AMKINGIA KIFUA BALE.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amemkingia kifua Gareth Bale pamoja na kiwango cha chini alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Barcelona ambao walipoteza kwa mabao 2-1. Nyota huyo mwenye miaka 24 alipangwa katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo ikiwa ni mara ya pili msimu huu.
Ancelotti amesema Bale alicheza vyema katika muda wote katika mchezo huo pamoja na kwamba walipoteza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mashabiki wa Madrid wanapaswa kumpa muda zaidi nyota huyo azoee kuliko kuanza kumkatisha tamaa kwa kumponda hivi sasa.
BLATTER ATAKA ADHABU KALI ZAIDI ILI KUTOKOMEZA UBAGUZI.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter anataka adhabu kali zaidi ili kupambana na ubaguzi katika soka ikiwemo adhabu ya kuondoa timu mashindanoni au kuwakata alama. Kauli ya Blatter imekuja kufuatia Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuanza uchunguzi dhidi ya klabu ya CSKA Moscow baada kiungo wa Manchester City Yaya Toure kulalamika kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki. Blatter amedai faini inayotozwa na timu kucheza bila mashabiki inaonekana ni adhabu isiyotosheleza kwasasa. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kama kweli wanataka kutokomeza suala hilo michezoni basi inapaswa adhabu kama kuondoa timu katika mashindano husika au kuzikata alama ziongezwe ili kudhibiti mashabiki wasio na adabu.
INIESTA KUONGEZA MKATABA BARCELONA.
KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amebainisha kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo katika siku za karibuni baada ya kuisaidia timu hiyo kuwafunga mahasimu wao Real Madrid kwa mabao 2-1 jana. Iniesta ndiye alikuwa nyota katika mchezo huo baada ya kusaidia mabao hayo yaliyofungwa kwa umaridadi na Neymar katika kipimndi cha kwanza na lingine la Alex Sanchez. Kulikuwa na tetesi kuwa Iniesta anaweza kumfuata golikipa wa timu hiyo Victor Valdes ambaye alidai kuwa hawezi kuongeza mkataba wa kuinoa klabu hiyo. Akizungumza baada ya mchezo huo Iniesta amesema anafuraha kuwepo hapo na anataka kubakia ndio maana ameamua kuongeza mkataba wake mapema iwezekanavyo.
VILABU UFARANSA KUFANYA MGOMO MWEZI UJAO.
VILABU vya soka nchini Ufaransa vitafanya mgomo mwezi ujao kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kulalamikia mipango ya serikali kuwatoza kodi ya asilimia 75 wanaopata mapato makubwa. Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972 unatarajiwa kuandaliwa katika wikiendi ya mwisho ya Novemba baada ya vilabu hivyo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo wenye utata wa Rais wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza kiwango kikubwa cha kodi. Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel amesema hakutakuwa na mechi yoyote ya ligi Novemba 29 na Desemba 2. Chini ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi wao ambao ni wachezaji ambacho kinazidi euro milioni moja.
EL SHAARAWY ATAKA KUMKIMBIA BALOTELLI MILAN.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya AC Milan, Stephen El Shaarawy amedai kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwenda kusaka maisha mapya katika timu nyingine ili aweze kupata nafasi ya kucheza. Uamuzi wa kinda huyo mwenye miaka 20 unazifanya klabu za Chelsea, Tottenham Hotspurs na Arsenal kuingia vitani lakini Liverpool inaelezwa ndio wana nafasi kubwa zaidi ya kumnyakuwa nyota huyo. El Shaarawy ambaye alifunga mabao 16 msimu uliopita amekuwa akipata wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza toka Mario Balotelli atue San Siro. Wamiliki wa Liverpool wanapanga mipango ya kununua wachezaji wadogo na El Shaarawy anaonekana kuwemo kwenye mipango hiyo.
Wednesday, October 23, 2013
GALLAS ATIMKIA A-LEAGUE.
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, William Gallas amekubali mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na klabu ya Perth Glory na kuongeza idadi ya wachezaji nyota waliojiunga na Ligi Kuu nchini Australia maarufu kama A-League katika siku za karibuni. Gallas mwenye umri wa miaka 36 ambaye ameichezea Ufaransa mechi 84 na pia kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 na 2010, amekuwa bila timu toka amalize mkataba wake wa miaka mitatu na klabu ya Tottenham Hotspurs Julai mwaka huu.
Ofisa Mkuu wa Perth, Jason Brewer amesema ni faraja kwa klabu hiyo kuweza kumvutia mchezaji kama Gallas na ni mategemeo yao ligi yao inaweza kukua zaidi na kuwavutia wachezaji nyota wengi zaidi duniani. Mbali na Gallas nyota wengine wanaokipiga A-League ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Alessandro Del Piero, Shinji Ono wa Japan na mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Emile Heskey.
NILIMUUZA BECKHAM KWASABABU ALITAKA "KUNIPANDA KICHWANI" - FERGUSON.
MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu hiyo kwasababu nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza alidhani yeye ni mkubwa kuliko meneja. Katika kitabu chake kipya kinachoelezea maisha yake ya ukocha, Ferguson amesema aligombana na Beckham baada ya kumkosoa kwa kiwango chake alichokionyesha katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza. Katika kitabu hicho Ferguson ameandika kuwa dakika ambayo mchezaji wa United atakapodhani yeye ni mkubwa kuliko meneja ni lazima aondoke na Beckham alidhani yeye ni mkubwa kuliko Ferguson ndio maana akamuuza. Ferguson pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mtindo wa maisha ya watu mashuhuri kufuatia nyota huyo kumuoa Victoria Adams aliyekuwa nyota wa kundi la muziki la Spice Girls nchini humo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Beckham ndiye mchezaji pekee kati ya aliyowafundisha kuchagua maisha ya umaarufu na kitendo hicho hakikumfurahisha ndio maana akamuacha aondoke. Lakini Ferguson alimpongeza nyota huyo kwa mchango wake uliochangia mafanikio mengi ya United na kumtaja kama kioo cha watoto wote duniani. Katika kipindi chote cha miaka 26 aliyofundisha United, Ferguson alishinda mataji 38 na kufanikiwa kuwafundisha nyota kadhaa wakiwemo Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Kean, Jaap Stam na Ruud Van Nistelrooy.
WEBB AKANUSHA KUTAKA KUMRITHI BLATTER.
RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Soka vya Nchi za Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf, Jeffrey Webb amekanusha tetesi kuwa anataka kuchukua kugombea nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA inayoshikiliwa na Sepp Blatter. Webb amehusishwa kugombea nafasi hiyo mwaka 2015, huku Blatter akipendekeza katika mkutano uliofanyika Caribbean Jumatatu iliyopita kuwa Webb anaweza kuchukua nafasi kuchukua nafasi yake siku zijazo. Lakini Webb mwenyewe alikanusha suala hilo akidai kuwa hana mpango wa kugombea nafasi hiyo katika siku za karibuni. Blatter ambaye aiongoza FIFA toka mwaka 1998 alikuwa akizungumza kufungua mkutano wa mwaka wa Concacaf. Mwaka 2011 Blatter aliwaambia viongozi wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kwamba kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake kukalia ofisi hiyo lakini mwaka huu ameonekana kubadili uamuzi baada ya kuonyesha ishara kama anaweza kugombea kwa kipindi kingine.
USHINDI WA DORTMUND WALIFANYA KUNDI LA ARSENAL KUWA GUMU ZAIDI.
USHINDI wa mabao 2-1 iliyopata timu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana umepelekea kundi F ambalo linahesabika kama kundi la kifo kuzidi kuwa gumu na lisilotabirika. Katika msimamo kundi hilo sasa Dortmund, Arsenal na Napoli ambao nao waliifunga Marseille kwa mabao 2-1, wote wana alama sita baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja katika michezo mitatu waliyocheza mpaka sasa. Kati ya timu nne katika kundi hilo ni timu mbili pekee ndio zitapata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya timu 16 bora itakapofika Desemba mwaka huu. Mechi zitakazofuata Arsenal itakuwa na kibarua kigumu pale watakapoifuata Dortmund nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa maraudiano wakati Marseille watapata nafasi ya kujiuliza pale watakapokuwa wageni wa Napoli, mechi zote zitachezwa Novemba 6 mwaka huu. Katika baadhi mechi zingine za michuano hiyo zilizochezwa jana, AC Milan ilishindwa kuitambia Barcelona katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare ya bao 1-1, Celtic wakaifunga Ajax Amsterdam kwa mabao 2-1 huku Chelsea wakipata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Schalke.
Tuesday, October 22, 2013
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
SERENGETI BOYS YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA
Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Serengeti Boys) imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika itakayofanyika Mei mwakani. Mpira wa miguu ni kati ya michezo 22 itakayoshindaniwa katika mashindano yatakayofanyika Gaborone, Botswana chini ya Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA). Kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC), Tanzania imepewa nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika kutokana na kuwa na programu nzuri za vijana hasa chini ya umri wa miaka 17. Hiyo itakuwa ni michezo ya Pili ya Afrika kwa Olimpiki ambapo ya Kwanza ilifanyika mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.
YANGA, SIMBA VIWANJANI VPL J5Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Oktoba 23 mwaka huu) kwa mechi tatu; ambapo Yanga itaikaribisha Rhino Rangers katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Coastal Union inaikaribisha Simba katika mechi itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na kuchezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma. Tanzania Prisons ambayo imepoteza mechi mbili zilizopita ugenini dhidi ya Ashanti United na Simba inarejea uwanja wake wa Kumbukumbu ya Sokoine kwa kuikaribisha Kagera Sugar. Nayo Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea kesho (Oktoba 23 mwaka huu) kwa mechi moja ya kundi A itakayozikutanisha Tessema na Villa Squad kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
KIINGILIO MECHI YA U20 WANAWAKE 1000/-Kiingilio cha chini kwenye mechi ya wanawake chini ya miaka 20 katika ya Tanzania na Msumbiji itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 1,000. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho ni kwa ajili ya viti vya rangi ya kijani, bluu na chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Timu ya Msumbiji inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Oktoba 23 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya LAM. Msumbiji yenye msafara wa watu 25 itafikia kwenye hoteli ya Sapphire.
UCHAGUZI TPL BOARD KUFANYIKA IJUMAAUchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utafanyika Oktoba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower. Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wajumbe wanaounda Mkutano wa Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na 14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Wagombea kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.

NASSIB AWAZAWADIA MAREFA SIMBA, YANGA.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ramadhan Nassib ametoa sh. milioni moja kwa waamuzi waliochezesha mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam. Nassib ambaye alichaguliwa katika nafasi hiyo akiwakilisha klabu amesema ametoa fedha hizo ili kuwapongeza waamuzi hao kwa kuchezesha vizuri mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3. “Waamuzi wanapofanya vibaya tunawaadhibu, hivyo wakifanya vizuri wanastahili kupongezwa pia. Vilevile kuwapongeza ni kuwaongezea ari ya kuchezesha vizuri zaidi,” amesema. Israel Nkongo ndiye aliyeongoza jopo hilo ambapo mwamuzi msaidizi namba moja alikuwa Hamis Chang’walu wakati namba mbili alikuwa Ferdinand Chacha. Mwamuzi wa mezani alikuwa Oden Mbaga. Waamuzi wote hao wana beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), na watoka Dar es Salaam ukiondoa Chacha ambaye maskani yake ni Bukoba mkoani Kagera.
BRUNO METSU AZIKWA KWA HESHIMA ZOTE SENEGAL.
KOCHA wa zamani wa Senegal Bruno Metsu,ambaye alifariki Jumanne wiki iliyopita huko Ufaransa, amezikwa jana jijini Dakar, Senegal, mazishi yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali na akizikwa kwa heshima kubwa. Metsu alibadili dini na kuwa Muislam wakati alipokuwa akiwafundisha Simba wa Teranga Senegal kati ya mwaka 2000 na 2002 na akaoa mwanamke wa Senegal Viviane Dieye, ambaye amesema kocha huyo alitaka azikwe Dakar. Jeneza lake lilifunikwa na bendera ya nchi hiyo aliyoiongoza kwenye fainali za dunia za mwaka 2002 na amezikwa kwenye makaburi ya waislam ya Yoff. Metsu anaelezewa kama shujaa wa nchi hiyo ambaye moyo wake ulikuwa na mapenzi halisi na nchi hiyo. Kocha huyo kwa mara ya mwisho amefanya kazi ya ukocha huko Dubai kwenye klabu ya Al Wasl FC mwaka 2012 kabla ya kuiacha kazi hiyo na kwenda kupata matibabu ya kansa ya ini na mapafu huko Ufaransa. Amefariki kwenye sehemu alikozaliwa kijiji cha Coudekerque Kaskazini mwa Ufaransa na akasafirishwa kwa maziko yaliyofanyika hiyo jana nchini Senegal.
FA KUMCHUKULIA HATUA MOURINHO.
CHAMA cha Soka Cha Uingereza-FA kimemshitaki meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho kwa tabia isiyo ya kiungwana aliyoionyesha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Cardiff City mwishoni mwa wiki iliyopita. Mourinho aliamriwa kwenda kukaa jukwaani na mashabiki na mwamuzi Anthony Taylor zikiwa zimebaki dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika baada ya kulalamika mara kwa mara kwamba Cardiff walikuwa wakipoteza muda. Kocha huyo ambaye amepewa mpaka Alhamisi kujibu tuhuma hizo, alikataa kuomba radhi kuhusiana na tukio hilo wakati akihojiwa kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke ya Ujerumani. Mourinho amesema Cardiff ambao walifungwa mabao 4-1 katika mchezo huo walikuwa wakipoteza muda kila wakati ambao mwamuzi anakuwa amepuliza filimbi aidha kwa ajili ya faulo au mpira wa kurusha. Mourinho aliendelea kudai kuwa mashabiki wanalipia tiketi zao kwa ajili ya kutazama burudani ya soka na sio timu moja ipoteze muda ili mchezo umalizike haraka.
Monday, October 21, 2013
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
VPL YAPISHA MECHI YA U20 WANAWAKE
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji. Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. U20 tayari imehamishia kambi yake hosteli ya Msimbazi Center, Dar es Salaam kutoka JKT Ruvu mkoani Pwani tangu wiki iliyopita kujiandaa kwa mechi hiyo. Fainali za Kombe la Dunia kwa U20 wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada. Marekebisho ya ratiba ya VPL yamegusa raundi zote tatu zilizobaki kukamilisha mzunguko wa kwanza. Kutokana na marekebisho hayo mechi za raundi ya 11 zitakuwa ifuatavyo; Oktoba 28 mwaka huu ni Coastal Union vs Mtibwa Sugar, Oljoro JKT vs Ashanti United, Ruvu Shooting vs Kagera Sugar na Simba vs Azam. Oktoba 29 mwaka huu ni Tanzania Prisons vs Mbeya City, Yanga vs Mgambo Shooting na Rhino Rangers vs JKT Ruvu. Raundi ya 12 ni kama ifuatavyo; Oktoba 31 mwaka huu ni Simba vs Kagera Sugar, Novemba 1 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Yanga. Novemba 2 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Coastal Union, Tanzania Prisons vs Oljoro JKT, Azam vs Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers na Mbeya City vs Ashanti United. Raundi ya 13 ni kama ifuatavyo; Novemba 6 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu ni Azam vs Mbeya City. Mechi za kufunga raundi ya 10 zitachezwa keshokutwa (Oktoba 23 mwaka huu) kama ratiba inayoonesha. Mechi hizo ni kati ya Coastal Union vs Simba, Tanzania Prisons vs Kagera Sugar na Yanga vs Rhino Rangers.
MECHI YA SIMBA, YANGA YAINGIZA MIL 500/-Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000. Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Ni tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.
VITAMBULISHO MICHUANO YA CHALENJIBaraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limefungua maombi ya vitambulisho (Accreditation) kwa ajili ya waandishi wa habari wanaotarajia kuripoti mashindano ya Kombe la Chalenji. Mashindano ya Kombe la Chalenji yatafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu. Kwa waandishi wa habari wanaotaka kuripoti mashindano hayo wanatakiwa kutuma maombi yao kabla ya Oktoba 31 mwaka huu. Mbali ya majina, katika maombi hayo mwandishi wa habari ni lazima aoneshe chombo anachofanyia kazi na kuambatanisha na picha moja ya pasipoti.

ORLANDO PIRATES, AL AHLY KUKWAANA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.
KLABU ya Al Ahly ya Misri imejiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuifunga Coton Sport ya Cameroon kwa changamoto ya mikwaju ya penati na kutinga fainali. Al Ahly walishinda kwa matuta 7-6 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika nusu fainali ya mkondo wa pili iliyofanyika huko El-Gouna. Katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza timu hizo pia zilitoka sare ya bao 1-1 hivyo kufanya timu hizo hizo kufungana jumla ya mabao 2-2 katika mechi mbili walizokutana. Al Ahly sasa watakwaana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika fainali ya mikondo miwili itakayochezwa mwezi ujao.
GYAN AENDELEZA REKODI YA MABAO UAE.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan ameendelea kuwa katika kiwango cha juu baada ya kufikisha mabao 60 katika Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu maarufu kama Pro League. Gyan ambaye ambaye ni nahodha wa Ghana alifanikiwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-1 iliyopata timu yake ya Al Ain dhidi ya Dubai na kufikisha mabao saba katika mechi nne za ligi alizocheza msimu huu. Wiki iliyopita Gyan alifunga mabao mawili katika ushindi mnono wa mabao 6-1 iliyopata Ghana katika mchezo wa mtoano wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Mabao hao matatu aliyofunga Gyan katika Pro League yanamfanya kufikisha jumla ya mabao 60 katika mechi 44 alizocheza katika misimu miwili ambayo amekuwa huko.
KLOPP ATAMBA KUICHAPA ARSENAL.
MENEJA wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amesema ana uhakika wa ushindi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Arsenal itakayofanyika katika Uwanja wa Emirates. Dortmund watakwenda jijini London wakiwa nyuma ya Arsenal kwa alama tatu kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya Napoli ya Italia kabla ya kuzinduka na kuibamiza Olympique Marseille ya Ufaransa kwa mabao 3-0. Akihojiwa mara baada ya mchezo wa Bundesliga ambao Dortmund ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hannover, Klopp amesema ana uhakika wa kufanya vyema katika mechi yao hiyo itakayochezwa kesho. Klopp amesema anajua kwamba Arsenal wako katika kiwango cha juu hivi sasa na wanaongoza ligi lakini hilo haliwezi kuwatisha kasababu anaamini vijana wake wanaouwezo wa kukabiliana na timu yoyote.
NI MAPEMA KUIONDOA UNITED KATIKA MBIO ZA UBINGWA - WENGER.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene amekataa kuiondoa klabu ya Manchester United katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza pamoja na mabingwa hao watetezi kuwa nyuma Arsenal wanaoongoza ligi hiyo kwa alama nane. Arsenal waliongeza pengo dhidi ya United wanaonolewa na David Moyes Jumamosi baada ya kuifunga Norwich kwa mabao 4-1 wakati United wao walipoteza alama kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton. Hata hivyo Wenger amesisitiza kuwa mbio za ubingwa haziwezi kuamuliwa sasa hivyo huwezi kuwaondoa United na kuonya kuwa hata wao wanaweza kuporomoka. Wenger amesema hakuna timu inayotaka kuwa katika nafasi ya United hivi sasa lakini anaamini kutokana na uzoefu na ubora wa wachezaji walionao wanaweza kukwea na kupanda huko mbele.
HODGSON, FERDINAND WATEULIWA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO MABOVU YA UINGEREZA.
CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimewateua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roy Hodgson na beki wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand kuingia katika tume ya kuchunguza mapungufu ya timu ya taifa. Tume hiyo ambayo itakuwa na watu 10, itakuwa na jukumu la kuangalia njia za kuongeza wachezaji wa Uingereza katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na wanatarajiwa kuwasilisha ripoti yao mwishoni mwa Machi mwakani. Kuteuliwa kwa Ferdinand ambaye ni mweusi kumekuja kufuatia mjumbe wa bodi ya FA Heather Rabbatts kumponda mwenyekiti wake Greg Dyke kwa kuchagua wanaume na watu weupe pekee katika tume hiyo. Dyke amesema uteuzi wa Ferdinand umetokana na uzoefu wake katika mchezo wa soka toka alipoanza wakati akiwa West Ham United na kuja kushinda taji la Ligi Kuu naLigi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa na United huku akiiwakilisha Uingereza katika michuano kadha ya Kombe la dunia.
Friday, October 18, 2013
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
KAMATI YA UCHAGUZI YATANGAZA WAGOMBEA TFF
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa Bodi ya Ligi (TPL Board) utakaofanyika baadaye mwezi huu. Uchaguzi wa Bodi ya TPL utafanyika Oktoba 25 mwaka huu wakati ule wa TFF utafanyika Oktoba 27 mwaka huu. Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa TPL Board na ule wa TFF zimeanza leo (Oktoba 18 mwaka huu) zitamalizika siku moja kabla ya uchaguzi saa 10 kamili alasiri. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni amewataja wagombea kwa upande wa TPL Board kugombea uenyekiti ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar), Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Wanaowania ujumbe wa Bodi ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui). Wagombea kwenye uchaguzi wa TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu). Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya). James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani). Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam). Mbwezeleni amewataka wagombea kufanya kampeni bila kukashfu wenzao, kwani Kanuni ya Uchaguzi za TFF toleo la 2013 inatoa fursa kwa Kamati ya Uchaguzi kuwaondoa wagombea wa aina hiyo kwenye uchaguzi.
MAGARI MAALUMU TU MECHI YA SIMBA, YANGAMagari yenye shughuli maalumu tu ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanja wakati wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi itaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu inaruhusiwa kuingia na magari matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya viongozi. Ukaguzi wa kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huo si wa kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama. Vilevile watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na mifuko ya aina yoyote ikiwemo mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari wanaotumia mabegi hayo kwa ajili ya kubebea kamera zao. Pia hakuna wafanyabishara watakaoruhusiwa kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka uwanja. Kwa washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa kero kwa wenzao wakiwemo walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale wenye silaha kama bastola ambapo wakikamatwa wafikishwa polisi na baadaye kufunguliwa mashtaka kortini. Barabara ya Uwanja wa Taifa itafungwa kuanzia saa 2 asubuhi upande wa Chang’ombe, hivyo washabiki wanatakiwa kununua tiketi zao mapema kesho (Jumamosi) ambapo zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia saa 4 asubuhi. Vituo hivyo ni mgahawa wa City Sports Lounge, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
MBEYA CITY, JKT RUVU UWANJANI VPLLigi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kutimua vumbo kesho (Oktoba 19 mwaka huu) kwa mechi tano huku Mbeya City ikiikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mechi nyingine zitakuwa kati ya Oljoro JKT na Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Mtibwa Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Manungu, Turiani), Ashanti United na Ruvu Shooting (Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam) na Kagera Sugar dhidi ya Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba). Wakati huo huo, Ligiu Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea katika viwanja nane kesho (Oktoba 19 mwaka huu) huku Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ukiwa mwenyeji wa mchezo kati ya African Lyon na Friends Rangers. Nayo Villa Squad itacheza na Green Warriors katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Polisi Morogoro na Kimondo (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Lipuli na Kurugenzi (Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa) na Mkamba Rangers dhidi ya Majimaji (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro). Toto Africans na Mwadui (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Polisi Dodoma na Polisi Tabora (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), wakati Polisi Mara na pamba zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

LOEW AONGEZA MKATABA NA UJERUMANI.
KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amefikia makubaliano na Chama cha Soka cha nchi hiyo-DFB juu ya mkataba mpya ambao utamalizika mwaka 2016. Mkataba wa sasa wa Loew mwenye umri wa miaka 53 ulikuwa unamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 lakini sasa amemaliza tetesi juu ya mustakabali wake kwa kusaini mkataba huo wa miaka miwili. Loew alichukua mikoba ya kuinoa Ujerumani mwaka 2006 baada ya kufanya kazi kama msaidizi wa Jurgen Klinsmann katika timu hiyo. Kocha huyo ameiongoza Ujerumani kutinga fainali ya michuano ya Ulaya 2008 ambapo walifungwa na Hispania kwa bao 1-0 kabla ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 na ile ya Ulaya 2012.
BAYERN KUMPA LEWANDOWSKI PAUNDI MILIONI 10 KWA MWAKA.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Robert Lewandowski atakunja kitita cha paundi milioni 10 wakati atakapojiunga na Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu huu. Mabosi wa Bayern wamepuuza taarifa kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Poland ameamua kubadili mawazo kujiunga na klabu hiyo na kusisitiza kuwa uvumi huo utakwisha wakati watakapofanya usajili wa awali katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Katika kipindi hiki haruhusiwi kufanya mazungumzo yoyote rasmi kuhusiana na uhamisho huo mpaka Januari lakini kumekuwa na tetesi kuwa Bayern wamepanga kumpa mkataba mnono wa miaka minne ambao utamuwezesha kuwa analipwa kiasi cha paundi 150,000 kwa wiki. Taarifa zozote rasmi za Bayern kumnyakuwa nyota huyo zitakuwa ni pigo kwa vilabu vya Manchester United na Chelsea ambao nao wamekuwa wakimtolea macho kwa kutaka kumsajili.
RONALDO NDIYE MSHAMBULIAJI BORA ZAIDI - CAPELLO.
KOCHA wa timu ya taifa ya Urusi, Fabio Capello amedai kuwa nguli wa zamani wa soka wa kimataifa wa Brazil, Rolando de Lima ndio mshambuliaji bora zaidi aliyecheza chini yake. Capello amewahi kufanya kazi na washambuliaji wengi nyota akiwemo Alessandro Del Piero, Raul, Marco van Basten, Francesco Totti na Ronaldo lakini anadhani Mbrazil huyo ndiye alikuwa bora zaidi. Kocha huyo ambaye pia amewahi kuinoa timu ya taifa ya Uingereza amesema Van Basten alikuwa mshambuliaji mzuri lakini anadhani Ronaldo wakati akiwa fiti alikuwa bora zaidi. Mbali na kuzungumzia nyota hao Capello alienda mbali na kuipa nafasi klabu ya Arsenal kufika mbali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kikosi walichonacho hivi sasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)