Sunday, December 30, 2012
MILANOV MCHEZAJI BORA WA MWAKA BULGARIA.
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Bulgaria-PFC kimemteua mshambuliaji wa klabu ya Litex Lovech, Georgi Milanov kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo mbele ya wachezaji wengine nyota akiwemo Dimitar Berbatov anayecheza katika klabu ya Fulham ya Uingereza. Milanov mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji mdogo kuwahi kushinda tuzo hiyo na mchezaji wa kwanza ambaye anacheza soka chini humo kushinda tuzo hiyo toka mwaka 2001. Kiungo huyo amefunga mabao nane katika michezo 14 aliyocheza na kuwa mhimili wa kuisaidia klabu yake kukwea mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa mara baada ya sherehe hizo nyota huyo amesema ni heshima kubwa kwake kupokea tuzo huyo na kuwashukuru waandaji, wachezaji wenzake pamoja na kocha wake Hristo Stoichkov kwa kumsaidia kufikia kiwango alichonacho hivi sasa.
BOJAN ATAREJEA TENA BARCELONA - BABA
RONALDINHO ATAMANI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ameeleza kuwa anahitaji kuwamo katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitashiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona ana matumaini kuwa atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano hiyo katika kipindi cha miezi 18 ijayo ambayo itaandaliwa nchini kwake. Ronaldinho amesema hakuna kitu kinacholeta furaha kama kucheza michuano ya Kombe la Dunia mbele ya mashabiki wa nyumbani na hapendi kupoteza nafasi hiyo muhimu. Kwasasa nyota huyo ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Atletico Mineiro amekuwa akipambana kurejesha makali yake ya zamani ili aweze kuitwa katika kikosi hicho na anaamini katika kipindi cha miezi 18 ijayo atakuwa amefikia kiwango hicho. Luiz Felipe Scolari ambaye ameisaidia Brazil kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 2002 wakati huo Ronaldinho akiwa ndio nyota nchi hiyo ndio amekabidhiwa tena mikoba ya kuinoa timu ya taifa Novemba.
WALCOTT ATABAKIA - WENGER.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa mshambuliaji wake nyota Theo Walcott atabakia klabuni hapo baada ya kuisaidia kupata ushindi mnono kwa mabao matatu aliyofunga katika Uwanja wa Emirates dhidi ya Newcastle. Arsenal ilifanikiwa kuisambaratisha Newcastle kwa mabao 7-3 ambao ushindi huo unakuwa watatu mfululizo baada ya kutolewa katika Kombe la Ligi na Bradford City inayoshiriki Ligi Daraja la pili. Walcott alionyesha kuimudu vyema nafasi ambayo anaitaka ya kuwa mshambuliaji wa kati akifunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya kufunga mengine mawili katika kipindi cha pili na kukabidhiwa mpira baada ya mchezo huo kwa kufunga hat-trick. Nyota huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 23 bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo pamoja na kuahidiwa kuongezewa marupurupu. Lakini Wenger alionyeshwa kufurahishwa na kiwango cha nyota huyo na ana matumaini watafikia makubaliano kuhusu mkataba wake mpya.
DJOKOVIC ANYAKUWA TAJI LA MUBADALA.
MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba moja duniani, Novak Djokovic ameanza msimu mpya wa michuano ya tenisi baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa 6-7 6-3 6-4 katika fainali ya mashindano ya maonyesho ya Mubadala iliyofanyika jijini Abu Dhabi. Djokovic ambaye alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wa nusu fainali baada ya kumtoa David Ferrer anayeshika namba tano wakati Almagro ambaye aliziba nafasi ya Rafael Nadal aliyejitoa alimfunga Janko Tipsarevic. Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Djokovic alifurahia kunyakuwa taji la michuano hiyo ya Abu Dhabi kwa mara nyingine na kuwasifu wapinzani wake aliokutana nao kwamba walimpa changamoto kubwa ambayo itamsaidia katika michuano iliyo mbele yake. Wachezaji wote wanne walioshirki michuano hiyo wanatarajiwa kuelekea nchini Australia kwa ajili ya michuano ya wazi itakayoanza Januari 14 jijini Melbourne huku Djokovic akiwa bingwa mtetezi.
Friday, December 28, 2012
YANGA KUONDOKA ALFAJIRI DESEMBA 30 KUELEKEA UTURUKI.
WACHEZAJI 27 wa klabu ya Yanga, wanatarajia kuondoka kesho kwenda Uturuki kwa kuweka kambi ya wiki mbili. Yanga itaondoka saa 10:30 alfajiri kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki na kufika Instambul Jumatatu saa 4:30 asubuhi kabla ya kwenda katika mji wa Antarya ambapo wataweka kambi yao. Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alisema maandalizi yote kwa ajili ya safari hiyo yamekamilika na timu hiyo itafikia katika Hotel ya Sueon Beach ambayo iko katika ufukwe wa bahari. Kizuguto alisema ikiwa nchini humo iatacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa na timu ambazo zitatangazwa mara baada ya timu hiyo kufika nchini Uturuki. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Ali Mustapha 'Bartez' Said Mohamed na Yusuf Abdul, Geofrey Taita, Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Stephano Mwasika, Kevin Yondan na Nadir Haroub 'Canavaro'. Wengine ni Twite Kabange, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, George Banda, Jerry Tegete, David Luhende, Rehani Kibindu na Simon Msuva. Aliwataja viongozi wa benchi la ufundi kuwa ni Kocha Mkuu Ernest Brandts, kocha msaidizi Fred Minziro, kocha wa makipa Razack Siwa, daktari Sufian Juma, Ofisa Utawala Hafidh Salehe, Ofisa Habari Baraka Kizuguto na Mohamed Nyenye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Yanga imetumia zaidi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya kugharamai kambi ya timu hiyo.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUU
Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa. Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968. TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.
OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo. Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF. Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.
NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho. Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.
OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo. Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF. Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.
NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho. Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.
HAKUNA KILICHOBADILIKA - CAVANI.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Napoli ya nchini Italia, Edinson Cavani amesisitiza kuwa hakuna chochote kilichobadilika baada ya kugundua kuwa klabu yake hiyo ilikataa ofa ya euro milioni 55 ili wamuuze. Cavani ndiye mshambuliaji ghali zaidi katika Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A akiwa amefunga mabao 13 katika ligi bao moja nyumba Stephan El Shaarawy ambaye anaongoza kwa ufungaji kwasasa. Dau hilo kubwa ambalo lilitolewa na klabu ambayo haijajulikana halijamuathiri nyota huyo ambaye amsisitiza bidii zake katika mazoezi ndizo zilizomfanya kufikia thamani hiyo. Cavani amesema taarifa za Napoli kukataa dau hilo haziwezi kumwathiri kwani amepanga kuendelea kuisaidia klabu hiyo katika mwaka 2013 kwa bidii zote ili waweze kupata mafanikio katika kila mashindano. Napoli inashika nafasi ya sita ikiwa nyuma ya klabu za Juventus, Fiorentina, Lazio na Inter Milan katika msimamo wa Serie A.
ARSENAL YAMTENGEA VILLA PAUNDI MILIONI 16.
KLABU ya Arsenal imetangaza dau la paundi milioni 16 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Barcelona, David Villa. Meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger ameonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 lakini maofisa wa Arsenal wameambiwa kuwa watahitajika kulipa kiasi cha paundi milioni 20 kama watahitaji kumng’oa mshambuliaji hyo wa kimataifa wa Hispania. Hatahivyo kiasi hicho cha fedha kilichotajwa na Barcelona kinaweza kuwa kikubwa kwa Arsenal kwasababu ya umri wa Villa. Mbali na Arsenal Chelsea nao wameonesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo ambaye ni mfungaji wa kihistoria nchini Hispania ili aweze kusaidiana na Eden Hazard na Fernando Torres katika safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo.
NIPO FITI - ABIDAL.
BEKI wa Barcelona Eric Abidal amesema anajisikia vyema na yuko tayari kurejea tena uwanjani ikiwa ni miezi nane imepita toka afanyiwe upasuaji wa kupandikizwa ini jingine. Akihojiwa Abidal mwenye umri wa miaka amesema ni muda mwingi umepita toka afanyiwe upasuaji na amekuwa akipambana ili aweze kurejea katika hali yake kawaida. Abidal alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine April 10 ikiwa ni mwaka mmoja toka alipoondolewa uvimbe wa kansa katika ini lake Machi 2011. Beki huyo alianza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake Desemba 19 siku ambayo ndiyo taarifa za kocha wa klabu Tito Vilanova kurudiwa na tatizo la kansa ya koo zilipotangazwa. Vilanova naye alifanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa uvimbe huo wa kansa na baadae kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo kwasasa anaendelea na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita.
MACLEISH KUINOA NOTTINGHAM FOREST.
MMILIKI wa klabu ya Nottingham Forest, Fawaz Al Hasawi raia wa Kuwait amemteua kocha wa zamani wa klabu ya Aston Villa Alex MacLeish kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ikiwa zimepita saa 24 toka amtimue aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sean O’Driscoll. Al Hasawi amesisitiza kuwa alikuwa anataka kocha mwenye uzoefu wa Ligi Kuu nchini Uingereza wakati alipotoa uamuazi wa kushangaza kwa kumfukuza O’Driscoll kufuatia ushindi wa mabao 4-2 iliyopata timu hiyo dhidi ya Leeds United Jumatano. Tajiri huyo alifuata uamuzi wake kwa kumuajiri McLeish ambaye ameisaidia klabu ya Birmingham kupanda kutoka Ligi Daraja la Pili walipokuwa lakini alitimuliwa na Villa msimu uliopita baada ya kuifundisha kwa mwaka mmoja. Al Hasawi amesema amefanya uamuzi wa kumchukua McLeish kutokana na uzoefu wake wa ligi kuu hivyo anaamini atawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea.
MEIRELES APUNGUZIWA ADHABU.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Fenerbahce, Raul Meireles amepunguziwa adhabu ya kufungiwa michezo 11 mpaka kubakia mchi nne kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya Shirikisho la Soka nchini Uturki kukata rufani. Tume iliyokuwa ikisimamia suala ilitumia muda wa saa sita kuangalia picha za video za tuko hilo wakati wa mchezo dhidi ya mahasimu wao Galatasaray uliofanyika Desemba 16 na kufikia muafaka kwamba nyota huyo wa zamani wa klabu za Chelsea na Liverpool alizozana na mwamuzi lakini hamkumtemea mate kama ilivyoonekana mara ya kwanza. Katika taarifa yake tume hiyo imesema wakati mchezaji huyo akiendelea kuongea muda wote wa tukio isingeweza kuwa rahisi kudhamiria kumtemea mate mwamuzi huyo. Meireles mwenye umri wa miaka 19 tayari alikuwa amefungiwa mchezo mmoja baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Galatasaray na tume ilibadilisha uamuzi kwa kumtoza paundi 20,000.
Wednesday, December 26, 2012
AFCON 2013: ZAMBIA, ANGOLA ZAWA TIMU ZA KWANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI.
Timu za taifa za Angola na mabingwa wa Afrika Zambia zimekuwa za kwanza kuwasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika ambapo zimebaki wiki tatu kabla ya kuanza. Timu zote mbili zimefikia jijini Johannesburg na zitabakia hapo katika kipindi chote watakachokuwa wakifanya maandalizi yao kabla ya kuanza michuano hiyo Januari 19, 2013. Angola imesafiri na wachezaji wake wote 20 ambao wanacheza katika ligi ya nyumbani huku waliopo Ulaya wakitegemewa kuungana na wenzao wiki mbili kabla ya michuano hiyo. Shirikisho la Soka nchini Angola limedai kuwa wakiwa nchini humo wanatarajia kucheza michezo kadhaa ya kirafiki dhidi ya timu za Msumbiji, Tanzania na Zambia wakiwa hapohapo jijini Johannesburg lakini bado wako katika mazungumzo juu ya tarehe za kuchezwa mechi hizo. Algeria na Morocco zinatarajiwa kuwa timu zitakazofuata kuwasili nchini humo kwa ajili ya michuano hiyo siku baada ya kuanza mwaka mpya.
ODIMWINGIE AMALIZIA HASIRA ZAKE KWA IKPEBA.
Ikpeba |
FOMENKO KOCHA MPYA UKRAINE.
SHIRIKISHO la Soka nchini Ukraine-FFU limemtaja kocha Mikhail Fomenko kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Nafasi hiyo ambayo iliachwa wazi toka Septemba mwaka huu baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Oleg Blokhin kuondoka na kwenda kuifundisha klabu ya Dynamo Kiev baada ya michuano ya Ulaya kumalizika. Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester Ciy, Sven-Goran Eriksson ndio alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa kocha wan chi hiyo lakini mwishoni Fomenko ndio amethibitishwa kuchukua nafasi hiyo. Fomenko aliwashukuru maofisa FFU kwa kumwamini kumpa kibarua hicho na kwamba anatambua jukumu lake na changamoto zinazoikabili timu ya taifa ya nchi hiyo ambapo kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs aliwahi kukiri kuitaka nafasi hiyo kabla ya kukubali kuinoa Queens Park Rangers wakati mshambuliaji nyota wa zamani wa nchi hiyo Andriy Shevchenko alikataa nafasi ya kuifundisha nchi yake.
MWAMUZI HAKUWA FITI - MANCINI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini ameponda kiwango alichochezesha mwamuzi Kevin Friend katika mchezo dhidi ya Sunderland ambao umepelekea kufungwa bao 1-0 jana. Winga wa zamani wa City Adam Johnson ndiye aliyeipatia Sunderland bao la ushindi katika mchezo huo lakini Mancini anaamini kuwa kabla ya bao hilo kufungwa Pablo Zabaleta alitakiwa apewe mpira wa adhabu baada ya kuchezewa vibaya na Graig Gardner. Mancini amedai kuwa labda mwamuzi pamoja na mshika kibendera wake pengine walikula chakula kingi wakati wa sikukuu ya Noel ndio maana hawakuwa katika kiwango bora wakati wakichezesha mchezo huo. Kipindi hicho kimeifanya City kubakia nyuma mbele ya vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa alama saba na Mancini anamlaumu mwamuzi kwa kipigo hicho ambacho ni cha kwa klabu hiyo msimu huu.
ROONEY NJE WIKI MBILI.
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney anatarajiwa kukaa nje ya uwanja wa kipindi cha wiki mbili hadi nne baada ya kuumia mguu wakati wa mazoezi ya timu hiyo kabla ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Newcastle United. Rooney hakuwemo katika kikosi kilichoanza katika mchezo ambao walishinda mabao 4-3 dhidi ya Newcastle katika Uwanja wa old Trafford na meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson amesema kuwa mshambuliaji huyo atakosa michezo yote kwa mwaka huu. Kocha huyo aliiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa nyota huyo aliumia dakika za mwisho mazoezini wakati akijaribu kuruka juu ndipo alipojiumiza kifundo cha mguu wake wa kulia. United inakabiliwa na mchezo dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi kabla ya kusafiri kufuata Wigan Athletic Januari Mosi ambapo wanajipanga kujizatiti kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
MABAO YANGU SIO MUHIMU KAMA TIMU HAISHINDI - MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa mabao anayofunga hayatakuwa na maana yoyote kama timu yake itakuwa haiwezi kushinda`mechi zake. Mshambuliaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri miezi 12 ambapo amefunga mabao 91 na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller aliyefunga mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja lakini nyota huyo amesema ushindi wa timu yake ndio wenye umuhimu kuliko rekodi binafsi. Messi ambaye yuko nchini kwao Argentina kwa mapumziko ya kipindi cha baridi katika La Liga amesema amefurahi kufunga mabao mengi na kuvunja rekodi lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama wangishinda mataji kwani siku zote amekuwa akisisitiza mabao hayani maana yoyote kama timu haishindi chochote. Messi ambaye pia mwaka huu alipata mtoto wake wa kwanza aitwae Thiago amesema ujio wa mtoto huyo umemfanya awe mtu mwenye furaha na kuwashukuru wapenzi wote wa soka wa Argentina ambao husafiri kwenda kumshangilia wakati akicheza.
HODGSON ATAKA CHANGAMOTO YA MIKWAJU YA PENATI KATIKA MICHEZO YA KIRAFIKI.
KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson anaamini kuwa changamoto ya mikwaju ya penati katika michezo ya kirafiki ambayo watatoa sare inaweza kuisadia timu hiyo kuondokana na jinamizi la kupoteza nafasi katika michuano mikubwa. Uingereza imekuwa mhanga mkubwa wa kutolewa katika michuano mikubwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati wakiwa wamepoteza mara sita kati ya saba mara mwisho ikiwa katika robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Italia iliyofanyika Juni mwaka huu. Wakiwa katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, Hodgson amesema kuwa katka mojawapo ya mechi za kirafiki watakazotoka sare atashauri wapinzani wake wamalize mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Amesema kwa kufanya hivyo kutawaongezea uzoefu zaidi wachezaji mbele ya mashabiki wengi kuliko kufanya hivyo wakiwa mazoezini peke yake. Mwaka 2013 Uingereza itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil na baadae dhidi ya Ireland kabla ya kucheza na Scotland katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
MICHU KUITWA HISPANIA.
MSHAMBULIAJI nyota wa Swansea City Michu anatarajiwa kuitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Hispania mapema mwakani kufuatia kucheza katika kiwngo cha juu katika msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Kocha wa Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia, Vicente del Bosque anatarajia kumuita mchezaji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uruguay Februari 26 mwakani mchezo ambao utafanyika jijini Doha, Qatar. Katika kikosi hicho Michu ataungana na Iago Aspas ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Celta Vigo na amekuwa akihusihwa na tetesi za kwenda Swansea. Michu amekuwa akionyesha kiwango cha juu kwa upachikaji mabao toka liponunuliwa kwa ada ya dola milioni 3.2 kutoka klabu ya Rayo Vallecano katika kipindi cha majira ya kiangazi ambapo kwasasa anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 18.
Tuesday, December 25, 2012
CASILLAS IS A PRIDE OF MADRID - DEL BOSQUE.
KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amedai kuwa nahodha wa Real Madrid Iker Casillas ni mchezaji wa kujivunia wa klabu hiyo. Casillas ambaye amecheza michezo 143 akiwa na timu ya taifa aliachwa katika kikosi cha kocha wa Madrid Jose Mourinho katika safari Malaga na badala yake nafasi ilichukuliwa na golikipa namba mbili Antonio Adan. Real Madrid ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga walifungwa katika mchezo dhidi ya Malaga mabao 3-2 lakini Del Bosque ambaye ana umri wa miaka 61 alimtetea Casillas na kudai kuwa bado ana uwezo. Del Bosque amedai kuwa Casillas ni mchezaji aliyeanza kucheza klabuni hapo toka akiwa na umri wa miaka na ameifanyia mengi klabu hiyo hivyo inatakiwa kujivunia mchezaji wa aina yake.
MASHABIKI ANAPASWA KUHESHIMU TIMU ZINGINE - LOEW.
KOCHA wa timu taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amewataka mashabiki wa soka wan chi hiyo kuheshima viwango vya timu nyingine na kutotegemea makubwa kutoka kwa timu yao ya taifa. Katika mahojiano yake na wavuti wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB Loew amesema kuwa anaamini mashabiki wa soka nchini humo watakuwa wamepata somo kwa mwaka huu kuelekea katika mwaka mpya. Amesema timu ya taifa ya Hispania imekuwa ikifanya kazi ili ishinde vikombe kwa miaka mingi hivyo Ujerumani nayo anafikiri inaweza kufanya vizuri kama ikiheshimu wapinzani wake kwani sio wao pekee wenye ndoto za kunyakuwa vikombe. Kocha huyo alimalizia kuwa ni mapema mno kwa mashabiki wa nchi hiyo kuzungumzia michuano ya Kombe la Dunia 2014 itakayofanyika nchini Brazil hivi sasa badala kusaidia kuandaa timu bora ambayo italileta kombe hilo wakati ukifika.
EVERTON KUIKADIA RUFANI KADI NYEKUNDU YA GOBSON.
KLABU ya Everton imetangaza kuwa itakata rufani kufuatia kadi nyekundu aliyopewa nyota wake Darron Gibson katika mchezo ambao walishinda mabao 2-1 dhidi West Ham United. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United alitolewa na mwamuzi Anthony Taylor aliyechezesha mchezo huo kwa kumchezea vibaya Mark Noble wa West Ham katika dakika za majeruhi. Mshambuliaji wa West Ham Carlton Cole naye alitolewa nje mapema kutokana na tukio kama hilo alilofanya kwa beki wa Everton Leighton Baines. Rufani hiyo hiyo kama ikifanikiwa itamaanisha kuwa Gibson ambaye ni raia wa Jamhuri ya Ireland ataweza kucheza katika mchezo dhidi ya Wigan Athletic utakaochezwa katika siku ya maboksi Desemba 26.
Monday, December 24, 2012
MERRY XMASS & HAPPY NEW YEAR.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
MTIGINJOLA KUONGOZA KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Idd Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF iliyoundwa kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika hivi karibuni. Mtiginjola ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kabla ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu zitajazwa hivi karibuni. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wajumbe wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria. Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
MECHI YA STARS, CHIPOLOPOLO YAINGIZA MIL 109/-
Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000. Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000. Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070. Mapato ya mechi nyingine za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000. Taifa Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni 45.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Idd Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF iliyoundwa kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika hivi karibuni. Mtiginjola ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kabla ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu zitajazwa hivi karibuni. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wajumbe wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria. Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
MECHI YA STARS, CHIPOLOPOLO YAINGIZA MIL 109/-
Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000. Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000. Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070. Mapato ya mechi nyingine za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000. Taifa Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni 45.
CASILLAS AKATAA KUMKOSOA MOURINHO.
NAHODHA wa klabu ya Real Madrid, Iker Casillas amekataa kukosoa maamuzi ya kocha wake Jose Mourinho baada ya kumuweka benchi katika mchezo wa Jumamosi ambao walifungwa mabao 3-2 na Malaga. Uamuzi wa kumuacha Casillas ulielezewa na kocha huyo Mreno kama la kiufundi lakini ilisababisha Madrid kupoteza alama tatu muhimu katika mchezo huo wa La Liga. Akihojiwa Casillas amekiri kuwa hakuzoea hali hiyo ya kutocheza lakini siku zote kocha ndio anachagua nani acheze na asicheze hivyo akiwa kama mchezaji lazima aheshimu maamuzi yao kocha. Amesema wachezaji wenzake wote wamekuwa wakimfariji kama walivyokuwa wakimfariji Antonio Adan ambaye ni golikipa namba mbili aliyechukua namba ya Casillas katika mchezo dhidi ya Malaga. Suala la Mourinho kumuacha Casillas limechukuliwa tofauti na wadau wengi wa soka mmojawapo akiwa mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Madrid Jorge Valdano ambaye anaamini kuwa kocha huyo alikuwa akifikisha ujumbe kwamba yeye ndiye bosi katika klabu hiyo.
CHELSEA YAVUTA PAUNDI MILIONI 12 KWA STURRIDGE.
KLABU ya Chelsea imekubali kumuuza mshambuliaji wake Daniel Sturridge kwenda Liverpool kwa ada ya paundi milioni 12. Mshambuliaji huyo ambaye alifanyiwa vipimo vya afya Jumapili anategemewa kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na Liverpool katika muda wa saa 24 zijazo. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akitaka kupigania namba Chelsea mpaka mkataba wake utakapomalizika mizei 18 ijayo, atakuwa akilipwa na Liver mshahara wa paundi 60,000 kwa wiki. Chelsea itakuwa imepata faida kubwa kwa kumuuza mshambuliaji huyo ambaye walimnunua kwa ada ya paundi milioni 1.5 akitokea klabu ya Manchester City mwaka 2009.
MDOGO WAKE BALOTELLI AKAMATWA.
KAKA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Italia, Mario Balotelli alikamatwa Jumapili kwa tuhuma za kujeruhi maofisa wawili wa polisi wakati wa vurugu zilizotokea mtaani. Enoch Barwuach ambaye ni mdogo wake Balotelli ambaye anacheza katika klabu ya Manchester City anakabiliwa na mashtaka ya kushambulia na kukataa kukamatwa baada ya kujihusisha na ugomvi katika klabu ya usiku Jumamosi huko Brescia, Italia. Barwuah mwenye umri wa miaka 20 ambaye amezaliwa tumbo moja na Balotelli alilala lupango kabla ya kuhamishwa ambapo anatarajiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili. Mdogo wake Balotelli ameonyesha kufuata nyendo za kaka yake ambaye amekuwa akikumbwa na matukio mbalimbali ya vurugu ndani na nje ya uwanja.
HUNTERLAAR AKUBALI KUONGEZA MKATABA SCHALKE.
KLABU ya Schalke 04 ya Ujerumani imethibitisha kuwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uholanzi, Klaas-Jan Hunterlaar amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo. Hunterlaar mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa kuhamia katika vilabu mbalimbali vya Ulaya ikiwemo Inter Milan, Arsenal na Liverpool lakini sasa tayari amesaini mkataba mpya utakaombakisha hapo mpaka 2015. Mhsmabuliaji huyo aliwaambia wavuti wa klabu hiyo kuwa amefikiri kwa muda mrefu na makini kabla ya kuamua kusaini mkataba mpya na anajisikia furaha kuendelea kuwepo katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili mingine. Hunterlaar alijunga na Schalke akitokea AC Milan mwaka 2010 akiwa pia amepitia katika vilabu vya Real Madrid ya Hispania na Ajax Amsterdam ya nyumbani kwao.
VAN ANA BAHATI KUWA HAI - FERGUSON.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai kuwa beki wa Swansea City Ashley Williams angewewa kumuua Robin van Persie wakati wa mchezo baina ya timu hizo uliochezwa katika Uwanja wa Liberty jana. Beki huyo wa kimataifa wa Wales alipiga mpira uliomgonga kichwani Van Persie katika kipindi cha pili na kupelekea mshambuliaji huyo kunyanyuka kwa hasira na kumvaa Williams na wote kupelekea kupewa kadi nyekundu. Ferguson amesema kuwa tukio hilo ni bay asana kwani lingeweza kusababisha madhara makubwa kama kifo hivyo aliomba Chama cha Soka cha Uingereza-FA kuchunguza na kutoa adhabu. Williams akihojiwa mara baada ya mchezo huo alidai kuwa lilikuwa tukio la bahati mbaya hakudhamiria kumbutua na mpira kichwani Van Persie na kusababisha nyota huyo kushikwa na jazba. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 hiyo ikiwa ni sare ya kwanza United katika michezo 21 waliyocheza ambapo bado wamebakia kileleni mwa Ligi Kuu nchini humo wakiongoza kwa alama 43.
Sunday, December 23, 2012
ARSENAL KUPOTEZA PAUNDI MILIONI 30 WAKISHINDWA KUSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE MWAKANI.
KLABU ya Arsenal inaweza kupoteza kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka wanazopata kutoka kwa wadhamini wao Emirates kama klabu hiyo ikishindwa kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Meneja wa klabu hiyo Arsenal Wenger ameiongoza kushiriki michuano hiyo kila msimu toka amechukua mikoba ya kuinoa ya kuinoa timu hiyo. Lakini hivi sasa Arsenal inakabiliwa na msimu mgumu chini ya kocha huyo Mfaransa na wako katika hatari ya kukosa taji lolote katika kipindi cha miaka nane mfululizo huku wakiwa bado wanapigania nafasi nne za juu ili washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Emirates wadhamini wa klabu hiyo ambao wako katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpaka msimu wa mwaka 2014-2015 wameamua kuionya klabu hiyo kwa kuchukua tahadhari kama ikishindwa kushiriki michuano ya klabu bingwa. Kwasasa Arsenal wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutoka katika nafasi hiyo kama Chelsea ambao walikuwa katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Japan wakishinda mechi zao mbili za viporo walizonazo.
Lionel Messi ● All 91 Goals in 2012 ● New World Record
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amefunga bao la mwisho katika rekodi ya mwaka aliyoivunja wakati timu yake ikishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Valladolid jana usiku. Bao alilofunga Messi katika kipindi cha pili linamfanya kufikisha mabao 91 kwa mwaka huu baada ya kuipita rekodi iliyowekwa kwa kipindi cha miaka 40 na Gerd Muller aliyefunga mabao 85 mwaka 1972. Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa tofauti ya alama tisa na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili huku pia wakiwapita mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya tatu kwa alama 16. Katika mchezo huo timu zote mbili ziliingia uwanjani zikiwa na fulana maalumu zilizokuwa na ujumbe mahsusi kwa ajili ya kocha wao Tito Vilanova aliyefanyiwa upasuaji wa koo Alhamisi iliyopita.
STURRIDGE KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA LIVERPOOL.
MSHAMBULIAJI wa Chelsea Daniel Sturridge anatarajiwa kwenye Merseyside baadae leo kwa ajili ya vipimo vya afya ikiwa ni sehemu ya hatua ya kutaka kuhamia katika klabu ya Liverpool. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Melwood lakini inaaminika kuwa tayari wameshafikia makubaliano juu ya masuala ya mkataba. Liverpool wanatarajiwa kulipa kiasi cha euro milioni 14 kwa ajili ya mshambuaji huyo mwenye umri wa miaka 23. Klabu hiyo ilikuwa ikihitaji mshambuliaji mapema katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani baada ya kucheza nusu ya msimu wakimtegemea mshambuliaji mmoja Luis Suarez.
VILANOVA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.
MENEJA wa Barcelona, Tito Vilanova ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upauji kuondoa uvimbe wa kansa uliokuwa umeota kwenye koo. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji huo Alhamisi iliyopita na kwasasa anakabiliwa na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita ili kudhibiti kabisa tatizo hilo linalomkabili. Huo ni upasuaji wa pili kufanyiwa baada ya ule aliofanyiwa mwaka 2011 kipindi hicho akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pep Guardiola. Barcelona ilifanikiwa kuifunga Valladolid mabao 3-1 jana usiku na baada ya hapo Xavi Hernandez ambaye alifunga bao la kwanza amesema wanamzawadia ushindi huo kocha wao huo ambaye anapitia kipindi kigumu hivi sasa katika maisha yake. Kwasasa kocha msaidizi Jordi Roura ambaye amekuwa benchi la ufundi la klabu hiyo toka mwaka 2009 ndiye aliyekabidhiwa timu wakati wa kipindi hiki ambacho Vilanova hayupo.
SIJIUZULU NG'O - MOURINHO.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa hatajiuzulu wadhfa huo pamoja na timu yake kufungwa mabao 3-2 na Malaga ambao umewafanya kuachwa alama 16 na vinara wa La Liga Barcelona. Kufungwa kwa Madrid kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho kufuatia uamuzi wake wa kumuacha golikipa ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo Iker Casillas katika kikosi cha kwanza. Akihojiwa kama anahofu kibarua chake kitakuwa kimefikia ukingoni mara baada ya mchezo Mourinho amesema hahofii chochote na hawezi kuachia ngazi kwani kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo la msingi ni kujipanga na kuangalia wapi walikosea. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Casillas katika kipindi cha miaka 10 kupumzishwa benchi na kumpisha golikipa namba mbili Antonio Adan mwenye umri wa miaka 25.
Thursday, December 20, 2012
YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA MWAKA.
KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo na kumpita mwenzake ambaye wanatoka nchi moja Didier Drogba. Toure mwenye umri wa miaka 29 alipata kura nyingi zaidi za makocha wa timu za taifa pamoja na wakurugenzi wa benchi la ufundi na kushinda tuzo hiyo ambayo pia aliinyakuwa mwaka 2011. Nyota huyo alikuwa akifuatiwa kwa karibu na Drogba ambaye aliisaidia klabu yake ya zamani Chelsea kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga penati ya ushindi huku Toure yeye akiwa ameisaidia Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika pamoja na kuisaidia klabu yake kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya miaka 35. Mbali na Toure wengine waliopata tuzo katika sherehe hizo zilizofanyika jijini Accra, Ghana ni pamoja na Mohammed Abou Trika alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa Afrika, Genoveva Anomna wa Equatorial Guinea alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake. Mabingwa wa Afrika Zambia ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka huku kocha wake Herve Renard naye akitunukiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka na tuzo ya klabu bora ya mwaka ilikwenda kwa mabingwa wa Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika Al Ahly.
ARSENAL, BAYERN MUNICH ZOTE ZINA NAFASI YA KUTINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE - PODOLSKI.
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski anaamini kuwa klabu yake hiyo ina nafasi kubwa ya kusonga katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupangwa na mabingwa wa zamani wa michuano hiyo Bayern Munich. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alicheza katika klabu hiyo kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2006 mpaka 2009 kabla ya kurejea klabu ya nyumbani kwao ya Koln. Podolski amekiri kuwa hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora na uzoefu wa Bayern Munich katika michuano hiyo lakini anaamini kuwa timu zote mbili zina nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali. Bayern ilifungwa katika mchezo wa fainali na Chelsea May mwaka jana na pia walipoteza mchezo dhidi ya Inter Milan katika hatua kama hiyo mwaka 2010.
UPASUAJI WA VILANOVA WAFANIKIWA.
KLABU ya Barcelona imesema kuwa upasuaji wa koo aliofanyiwa meneja wake Tito Vilanova umemalizika salama na kocha huyo anaendelea vyema. Klabu hiyo ilitangaza Jumatano kuwa Vilanova alikuwa akihitaji uapsuaji wa pili baada ya kufanyiwa upasuaji mara ya kwanza kuondoa Novemba mwaka 2011. Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo imesema Vilanova anatarajiwa kubakia hospitalini kwa kipindi cha siku tatu mpaka nne na baada ya hapo atakuwa akiendelea na matibabu ya mionzi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alipumzika kwa kipindi cha wiki baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka jana kabla ya kurejea tena katika kazi yake kama msaidizi wa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola. Kikosi cha Barcelona ambacho kwasasa ndio kinaongoza Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga kitakuwa chini ya kocha msaidizi Jordi Roura mpaka hapo Vilanova atakaporejea tena baada ya kupona.
MBINU MBAYA ZA UFUNDISHAJI WA MOURINHO NDIO ZINAIYUMBISHA MADRID KWASASA.
NGULI wa zamani wa klabu ya Barcelona, Johan Cruyff amedai kuwa klabu ya Real Madrid inayumba kwasasa`kutokana na mbinu za ufundishaji za meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho. Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga wamekuwa wakisuasua katika wiki za karibuni na Cruyff ambaye ni raia wa Uholanzi anadhani kuwa klabu hiyo ingefanya vizuri kama ingekuwa inavuna wachezaji katika shule yake ya soka. Cruyff amesema tabia hasi aliyonayo Mourinho lazima iwe na madhara kwani anadhani mbinu anazotumia kufundisha ziko sawa kutokana na matokeo ya nyuma lakini yeye anaamini haziko sawa. Amesema hashangazwi na yanayotokea klabuni hapo hivi sasa kwani vitu kama hivyo hutokea wakati falsafa yako ni kusaini na kutegemea majina makubwa badala ya wachezaji uliowatengeneza mwenyewe. Cruyff alimalizia kuwa kikosi cha Barcelona ambacho kitamkosa kocha wake Tito Vilanova aliyefanyiwa upasuaji wa koo ili kondoa uvimbe wa kansa kwa kipindi cha miaezi mitatu mpaka minne kitaendelea kufanya vizuri pamoja na kutokuwepo kwa kocha wao huyo.
SINA MAJIVUNO - RONALDO.
MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid , Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa hana majivuno kama vyombo vya habari vinavyodai. Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akishutumiwa kukosa ubinadamu kulinganisha na nyota wa Barcelona Lionel Messi na baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania. Hatahivyo suala hilo limeonekana kutomsumbua Ronaldo ambaye ameelezea furaha yake ya kuwa na familia ambayo imemfanya kutulia na kuwa mchezaji wa kiwango cha juu na aliyekomaa. Ronaldo amesema pindi awapo uwanjani huwa mchezaji ambaye hufanya vitu kwa umakini na huwa hapendi kucheka mara kwa mara na hilo ndio tatizo watu wanadhani pengine ana dharau lakini sivyo wanafikiria hata kidogo. Nyota huyo aliongeza pia anapenda kuongeza mtoto mwingine kwani kuwa na familia kubwa ni kitu anachokipenda.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE DRAW.
Galatasaray v Schalke 04
Celtic v Juventus
Arsenal v Bayern Munich
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
AC Milan v Barcelona
Real Madrid v Manchester United
Valencia v Paris St Germain
Porto v Malaga
Celtic v Juventus
Arsenal v Bayern Munich
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
AC Milan v Barcelona
Real Madrid v Manchester United
Valencia v Paris St Germain
Porto v Malaga
Wednesday, December 19, 2012
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
SUALA LA AKINA MORRIS, CANNAVARO KWENDA KAMATI YA NIDHAMU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.
MTIBWA YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53. Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya. Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni. Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam. Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.
MTIBWA YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53. Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya. Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni. Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam. Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
TANZANIA YAPAA VIWANGO FIFA.
TANZANIA imekwea kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 130 katika viwango vya ubora duniani vinavyotolewa leo na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambavyo ndio vitakuwa vya mwisho kwa mwaka 2012 huku ikishika nafasi ya 38 kwa upande wa Afrika. Katika orodha hizo Ivory Coast imeendelea kuongoza kwa upande wa Afrika kwa kukupanda nafasi moja mpaka nafasi ya 14 ikifuatiwa na Algeria waliopo katika nafasi ya 19 huku Mali wakiwa katika nafasi ya 25 baada ya kupanda kwa nafasi tatu. Nafasi ya nne kwa Afrika inashikwa na Ghana ambao wameporomoka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 30 wakifuatiwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao ndio wanafunga orodha ya tano bora, ambapo wamepanda nafasi nne mpaka nafasi ya 34. Kwa upande wa tano bora duniani Hispania bado wako katika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina nafasi ya tatu wakati nafasi ya nne inashikiliwa na Italia ambao wamepanda nafasi moja tofauti na mwezi uliopita. Nafasi ya tano katika orodha hizo inashikiliwa na Colombia ambao wamekwea kwa nafasi tano toka nafasi ya 10 waliyokuwepo mwezi uliopita huku mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil nao wakizidi kuporomoka mpaka nafasi ya 18 kutoka nafasi ya 13 walioyokuwepo mwezi uliopita.
MESSI ANASTAHILI BALLON D'OR - IBRAHIMOVIC.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSV, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa Lionel Messi anastahili tuzo ya Ballon d’Or pamoja na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona ameshashinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo. Akihojiwa na gazeti moja nchini Ufaransa Ibrahimovic alimsifu Messi na kumfananisha kama mchezaji wa kwenye michezo ya luninga inayojulikana kama PlayStation na kudai kuwa anayeponda uwezo wa mchezaji huyo hajui mchezo wa soka. Ibrahimovic pia alisifu uwezo kiungo nyota wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa ni wa kipekee kwani pindi anapoingia uwanjani wachezaji wenzake wote hubadilika na kucheza vyema na kupelekea timu yao kupata matokeo mazuri. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alifika mbali na kudai kuwa hadhani kama kutatokea mchezaji wa aina ya Zidane huko mbele katika ulimwengu wa soka.
Monday, December 17, 2012
BRAZIL YAZINDUA UWANJA WA KWANZA UTAKAOTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA.
UWANJA wa Castelao Arena uliopo kaskazini-mashariki mwa Brazil katika mji wa Fortaleza umekuwa uwanja wa kwanza kukamilika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini humo mwaka 2014. Sambamba na Uwanja wa Mineirao uliopo jijini Belo Horizonte ambao utafunguliwa Desemba 21 ndivyo vinakuwa viwanja pekee kukamilika kwa wakati kabla ya michuano ya Kombe la shirikisho itakayochezwa Juni mwakani. Rais wan chi hiyo Dilma Rousseff alihudhuria sherehe za ufunguzi wa uwanja wa Castelao ambao umekamilika kwa kutumia gharama za dola milioni 249 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 67,000. Rousseff amesema kuwa kukamilika kwa uwanja huo kwa ajili ya michuano ya 2014 na ushindi wa timu ya Corinthians katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia jana unaonyesha jinsi gani Brazil ilivyokuwa na uwezo ndani na nje ya uwanja. Amesema nchi hiyo inauwezo wa kufanya vyote viwili kushinda mataji uwanjani na kujenga uwanja bora kama huo uliofunguliwa jana.
BOLT ASHINDA TUZO YA BBC.
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi Usain Bolt ameteuliwa kupewa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kutoka nje tuzo ambayo imetolewa na BBC. Bolt mwenye umri wa miaka 26 raia wa Jamaica aling’ara katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London mwaka huu baada ya kufanikiwa kutetea medali zake mbili katika mbio za mita 100 na 200 pamoja na zile za kupokezana vijiti za mita 400. Mafanikio hayo aliyopata katika olimpiki yanamfanya kuwa mwanaridha pekee aliweza kutetea medali zake katika michuano ya olimpiki miwili tofauti. Mbali na hivyo Bolt pia anakuwa mwanariadha pekee kuwahi kutokea kwa kunyakuwa medali sita katika olimpiki huku hiyo ikiwa ni mara ya tatu kunyakuwa tuzo hiyo katika kipindi cha miaka mitano.
BARCELONA YAJIKITA ZAIDI KILELENI.
KLABU ya Barcelona imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kuisambaratisha Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa jana usiku. Ushindi huo unaifanya timu hiyo kuongoza La Liga kwa tofauti ya tisa dhidi ya Atletico ambao wanashika nafasi ya pili huku wakiwaacha wapinzani Real Madrid kwa alama 13 baada ya timu hiyo kupata sare ya kushangaza ya mabao 2-2 dhidi ya Espanyol jana. Barcelona mbao wananolewa na kocha Tito Vilanova ilibidi wapambane katika mchezo wa jana baada ya mshambuliaji nyota wa Atletico Radamel Falcao kuipa timu yake bao la kuongoza kabla yaAdriano kusawazisha bao hilo na Sergio Busquest akiongeza lingine huku mabao mengine mawili yakifungwana Messi. Barcelona sasa inaongoza La Liga ikiwa na alama 13 baada ya kucheza michezo 16 wakifuatiwa na Atletico wenye alama 37 huku mabingwa watetezi Madrid wakiwa katika nafasi ya tatu kwakuwa na alama 33.
Sunday, December 16, 2012
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.
WARAKA WA MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF WAPITA
Waraka wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umepita baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura. Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba. Kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46, wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni kumi na moja. Kamati ya Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba. Vipengele vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais. Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF. Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
MIKOA SITA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI TWFA
Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora. Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Waraka wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umepita baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura. Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba. Kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46, wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni kumi na moja. Kamati ya Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba. Vipengele vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais. Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF. Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
MIKOA SITA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI TWFA
Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora. Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
MESSI KUSAINI MKATABA MNONO BARCELONA.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi anatarajia kusaini mkataba wa maisha na klabu hiyo ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi kuliko mchezaji yoyote wa ligi kubwa barani Ulaya. Baba wa nyota huyo, Jorge tayari amekwishaanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu suala la kuongeza mkataba wa sasa na hiyo inamaanisha kuwa Messi atabakia Barcelona mpaka atapofikisha umri wa miaka 31. Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amepanga kumuongeza mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo ili kuhakikisha anabakia klabuni hapo kabla ya kumpa mkataba mrefu nyota huyo wa Argentina kabla hajastaafu wadhifa huo. Messi kwasasa anachukua kitita kabla ya posho paundi milioni tisa kwa mwaka akiwa nyumba ya mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic anayechukua paundi milioni 12 kwa mwaka na Samuel Eto’o ambaye anachukua kitita paundi milioni 16 kwa mwaka akiwa na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
WILSHERE KUONGEZA MKATABA ARSENAL.
KIUNGO Jack Wilshere anatarajia kuipa ahueni klabu yake ya Arsenal pamoja na meneja Arsene Wenger aliyekalia kuti kavu kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao una thamani ya paundi milioni 20. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, aliapa kuwa kizazi kipya cha wachezaji wa Arsenal kitaleta furaha katika klabu hiyo ambayo sasa imefikisha miaka saba na nusu bila kunyakuwa taji lolote. Wilshere ambaye anatarajia kukubali kusaini mkataba mpya hivi karibuni ikiwemo mshahara unaoanzia paundi 80,000 kwa wiki pia alibainisha nia yake ya kuja kuwa nahodha wa klabu hiyo katika siku za usoni. Mbali na Wilshere lakini pia winga Alex Oxlade-Chamberlain aye anatarajiwa kusaini mkataba mpya hivyo habari hizo kuwapoza mashabiki wa klabu hiyo ambao wiki iliyopita walishuhudia klabu yao ikitolewa katika Kombela Ligi na Bradford City.
WEST HAM KUIPA WAKATI MGUMU ARSENAL KWA KUMUONGEZA MSHAHARA DIAME.
KLABU ya West Ham United inajipanga kumuongeza mshahara mara mbili ya kiwango anachopata hivi sasa kiungo wake Mohamed Diame ili kuizuia Arsenal kumchukua mchezaji huyo katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwaka huu. Kiungo huyo alijiunga na West Ham kama mchezaji huru akitokea Wigan Athletic katika kipindi cha majira ya kiangazi na amekuwa akionyesha kiwango bora toka atue katika klabu hiyo mpaka kuifanya Arsenal ianze kumnyatia. Diame ambaye ni raia wa Senegal anakadiriwa kuwa thamani ya paundi milioni 4.5 lakini maofisa wa West Ham wanajiamini kumbakisha mchezaji huyo kwa kumpa mshahara wa paundi 75,000 ambapo watasababisha na thamani ya mchezaji huyo kupanda pia. Klabu za Newcastle United, Fulham na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Arsenal ndio wenye uhitaji zaidi wa kiungo katika safu yake baada ya Abou Diaby kukaa nje kutokana na majeruhi mara kwa mara.
Subscribe to:
Posts (Atom)