Friday, January 30, 2015

COSTA AFUNGIWA MECHI TATU KWA KOSA LA KUMKANYAGA CAN WA LIVERPOOL.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Liverpool Emre Can. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu yake na Manchester City utakaochezwa Stamford Bridge kesho pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kilimtwanga adhabu hiyo ambayo Costa aliipinga kuhusiana na tukio lake alilofanya katika dakika ya 12 ya mchezo wa nusu fainali ya mkondo ya pili wa Kombe la Ligi uliofanyika Jumanne iliyopita. Costa aliyesajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 32, ameshafunga mabao 17 katika mechi 19 za Ligi Kuu alizocheza simu huu. Tukio hilo halikuonwa na waamuzi lakini lilinaswa katika picha video.

LIVERPOOL YAPANIA KUMCHUKUA DANNY INGS KABLA YA KUFUNGWA KWA USAJILI WA DIRISHA DOGO.

KLABU ya Liverpool inatarajia kumsajili mshambuliaji wa Burnley Danny Ings kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mdogo Jumatatu ijayo. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers yuko tayari kumchukua kwa mkopo nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa msimu uliobakia ili aweze kumalisha dili hilo. Ings ambaye anamalizia mkataba wake miezi sita uliobakia Burnley pia amekuwa akiwindwa na vilabu vya Tottenham Hotspurs na Real Sociedad. Hata hivyo, Burnley wanataka kuendelea kubakia na nyota huyo mpaka mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. Liverpool bado watatakiwa kulipa ada kama watamsajili Ings mwishoni mwa mkataba wake kutokana na kuwa chini ya umri w amiaka 24.

CHELSEA IKO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUMNASA MCOLMBIA CUADRADO.

KLABU ya Chelsea iko katika hatua za mwisho kukamilisha dili la paundi milioni 23.3 kwa ajili ya usajili wa winga wa Fiorentina Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka 26. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia tayari ameshafikia makubaliano kuhusu mambo yake binafsi na vinara hao wa Ligi Kuu na sasa klabu ziko katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho huo. Inakadiriwa kuwa Chelsea watatoa kitita cha paundi milioni 26.8 kwa ajili ya winga huyo kiasi ambacho ndio kilichowekwa na klabu yake hiyo ya Italia. Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 22 anaweza kwenda kwa mkopo Fiorentina ikiwa ni sehemu ya kukamilisha dili hilo. Hata hivyo, winga huyo wa kimataifa wa Misri bado hajaamua kama anataka kwenda kuchheza Serie A au la.

MICHUANO YA AFCON YAFIKIA PATAMU WIKIENDI HII.

MICHUANO ya Mataifa ya Afrika-Afcon inaingia katika robo fainali ya mwishoni mwa wiki hii baada ya kumalizika kwa hatua makundi ambayo imetoa timu nane. Timu zilizotinga hatua hiyo ni pamoja na wenyeji Guinea ya Ikweta na Congo Brazzaville zilizofuzu kutoka kundi A, Tunisia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC zilizofuzu kutoka kundi B huku Algeria na Coast na Ghana zenyewe zikitoka kundi C. Ivory Coast wenyewe walifuzu kutoka kundi D sambamba na Guinea ambao wao walifuzu kwa njia ya bahati nasibu baada ya kulingana alama na Mali. Kesho katika Uwanja wa Bata, wenyeji Guinea ya Ikweta itachuana na timu ngumu na wakongwe wa michuano hiyo Tunisia baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza utakaowakutanisha majirani Congo Brazzaville na DRC. Jumapili vinara wanaopewa nafasi ya kutwaa taji hilo Algeria na Ivory Coast watakwaana huko Malabo kugombea nafasi ya kuingia nusu fainali, mchezo ambao utatanguliwa na Ghana ikichuana na Guinea.

MILAN YAMCHUKUA DESTRO KUTOKA KWA MAHASIMU WAO AS ROMA.

KLABU ya AC Milan imetangaza kumsajili kwa mkopo mshambuliaji nyota wa kimataifa wa wa Italia Mattia Destro kutoka kwa mahasimu wao wa Serie A AS Roma. Nyota huyo alifaulu vipimo vyake vya afya leo huku akitarajiwa kupewa mkataba wa moja kwa moja utakaoigharimu Milan euro milioni 16. Milan iko katika mchakato wa kuimarisha kikosi chake kufuatia kusuasua katika nusu ya kwanza ya msimu. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anarejea katika jiji la Milan akiwa mchezaji kamili baada ya kuanza soka lake katika shule ya vpaji ya Inter huku pia akiwa amewahi kuvaa jezi za Genoa na Siena kabla ya kujiunga na Roma Julai mwaka 2012. Toka atue Roma amefunga mabao 24 katika mechi 57 alizocheza lakini alishindwa kabisa kupata namba katika kikosi cha kwanza msimu huu hivyo kuruhusiwa kuondoka.

PIQUE NA SHAKIRA WAPATA MTOTO WA PILI.

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique na mwanamuzi nyota Shakira wamefanikiwa kupata mtoto wao wa pili aliyezaliwa jana usiku. Shakira alijifungua mtoto wa kiume bila matatizo yeyote katika hospitali ya Quiron Tecknon iliyopo jijini Barcelona. Pique mwenye umri wa miaka 27 na mwanamuziki huyo wa Pop kutoka Colombia mwenye umri wa miaka 27, walitoa taarifa hizo muda mfupi kabla ya usiku wa manane. Jina la mtoto ambaye amezaliwa miaka miwili baada ya wawili hao kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Milan bado halijawekwa wazi. Wawili hao wamekuwa pamoja toka mwaka 2010 walipokutana katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

LEVANTE YAMCHUKUA MKONGWE UCHE.

KLABU ya Levante imetangaza kumsajili kiungo wa ushambuliaji wa kimataifa wa Nigeria Kalu Uche. Uche mwenye umri wa miaka 32 ambaye pia anaweza kucheza nafasi ya ushambuliaji amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miezi sita akiwa mchezaji huru. Nyota huyo ataweza kuongezwa mkataba mwingine kulingana na jinsi msimu utakavyokwenda kwa klabu hiyo ambayo inapambana isishuke daraja. Uche aliondoka katika klabu ya Al Rayyan ya Qatar na kurejea nchini Hispania kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka miwili. Levante imechukua kiungo huyo ili kuimrisha safu yake ya ushambuliaji ambayo msimu huu imefanikiwa kufunga mabao 13 pekee katika mechi 16 walizocheza. Kabla ya kutimkia Qatar Uche aliwahi kuzichezea klabu za Almeria na Espanyol.

ETO'O AAHIDI KUISAIDIA SAMPDORIA KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o ameeleza matamanio yake ya kuisaidia Sampdoria kufuzu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutambulishwa mbele ya wanahabari jana. Nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu katika klabu hiyo ya Serie A na kumaliza kipindi chake kifupi alichokaa Everton. Toka alipoichukua klabu hiyo mwaka jana, mmiliki Massimo Ferrero amekuwa akielezea matamanio yake ya kuinoa Sampdoria ikifuzu michuano hiyo na Eto’o anafikiri ni malengo yanayowezekana. Eto’o mwenye umri wa miaka 33, amesema ameonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii na kufuata ndoto zake kila kitu kinawezekana kwani amefanikiwa na kuwa mmoja kati ya wachezaji wakubwa kabisa duniani. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na hilo raia wa klabu hiyo ana haki ya kuwa na ndoto na kutimiza ndoto zake.

URENO YAMUUNGA MKONO FIGO KWA UAMUZI WAKE.

UAMUZI wa Luis Figo kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imepokewa vyema nchini kwake Ureno pamoja na kukabiliwa na kibarua kigumu mbele ya rais wa sasa Sepp Blatter katika uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu. Figo mwenye umri wa miaka 42 ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia na mmoja kati ya wachezaji bora katika kipindi chake akiwa Real Madrid na Barcelona alitangaza nia yake hiyo Jumatano iliyopita baada ya kukamilisha vigezo vilivyohitajika. Muda wa mwisho wa kutuma maombi utakuwa leo usiku huku huku Figo akiwa sambamba na wagombea wengine wasiomtaka Blatter na kutangaza nia akiwemo Prince Ali Bin Al-Hussein kutoka Jordan, Michael van Praag kutoka Uholanzi na Jerome Champagne na David Ginola wote kutoka Ufaransa. Rais wa Shirikisho la Soka la Ureno-FPF, Fernando Gomes amesema jana kuwa kujitokeza kwa FIGo kugombea nafasi hiyo ni heshima kubwa kwa soka la nchi hiyo hivyo watamuunga mkono mpaka mwisho wa safari yake. Waziri wa michezo wa Ureno Emidio Guerreiro pia alitangaza serikali kumuunga mkono kiungo huyo wa zamani ambaye ameliletea taifa hilo sifa kemkem.

WEST HAM YADAI KUFUATA TARATIBU ZOTE KWA KUMTUMIA SAKHO.

MENEJA wa West Ham United, Sam Allardyce hategemei Diafra Sakho kufungiwa kwa kuitumikia klabu hiyo baada ya kujitoa katika kikosi cha Senegal kilichoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika. Mshambuliaji huyo alishindwa kuwepo katika cha nchi hiyo kilichokuwa Guinea ya Ikweta kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya mgongo. Hata hivyo, alitokea benchi na kuifungia West Ham bao la ushindi mwishoni mwa wiki katika mchezo wa Kombe la FAdhidi ya Bristol City huku nchi yake ikiwa bado inashiriki Afcon kwa wakati hu. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limethibitisha kupokea malamiko kutoka Shirikisho la Soka la Senegal kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo, Allardyce amesema hana shaka kama nyota huyo atapewa adhabu yeyote kwani wamefuata sheria na taratibu zote zilizopo.

AFCON 2015: CAF KUANGALIA UPYA UTARATIBU WA KUPATA MSHINDI KWA BAHATI NASIBU ULIOWATOA MALI JANA.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limesema litaupitia upya utaratibu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu baada ya timu kuwa sawa katika hatua ya makundi. Hatua hiyo inakuja kufuatia jana Guinea kutinga robo fainali kwa ushindi wa mezani baada ya kubahatika kwenye bahati nasibu hiyo huku Mali ikifungasha virago baada ya timu zote mbili kumaliza mechi za makundi zikiwa zote zina alama tatu sawa na mabao matatu ya kufunga. Katika mechi za kundi D zilizomalizika juzi ni Ivory Coast pekee ndio waliokuwa wamesonga mbele baada ya kuifunga Cameroon kwa bao 1-0. Wadau wengi na mashabiki wa soka wameukosoa utaratibu huo wa bahati nasibu wakidai kuwa hautendi haki. Mkurugenzi wa habari wa CAF Junior Binyam amesema pamoja na kwamba walipaswa kusimamia kanuni za mashindano hayo lakini anadhani ipo haja ya kuboresha utaratibu wa kumpata mshindi pindi tukio kama hilo linapotokea. Binyam aliendelea kudai kuwa sio haki kwa timu kurudi nyumbani kama ilivyofanyika kwa Mali.

Thursday, January 29, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: MADRID WAPANGA KUCHUKUA DE GEA BURE KUTOKA MAN UNITED, PSG WAMTAKA ADEBAYOR KWA MKOPO.

KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Real Madrid imepanga kumsajili golikipa wa Manchester United David De Gea mwenye umri wa miaka 24 wakati mkataba wake utakapoisha katika kipindi cha miezi 18 ijayo ili waweze kumchukua kama mchezaji huru. Klabu ya Paris Saint Germain imefanya mazungumzo na Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wao Emmanuel Adebayor mwenye umri wa miaka 30 kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Klabu ya Swansea City wanafikiria kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Blackburn Ridy Gestede mwenye umri wa miaka 26 lakini mpaka sasa hakuna klabu yeyote iliyofikia dau la paundi milioni sita liliwekwa na timu hiyo ya daraja la kwanza. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anafikiria kuwasajili viungo wa klabu ya Hannover Lars Stindl mwenye umri wa miaka 26 na Leonardo Bittencourt mwenye umri wa miaka 21 katika kipindi cha usajili wa kiangazi. Rodgers pia anajiandaa kutoa kitita cha paundi milioni 29 ili kuzizidi maarifa Paris Saint-Germain, Real Madrid na Juventus kwa ajili ya kiungo mwenye umri wa miaka 17 Ruben Neves ambaye anajulikana kama Sergio Busquets mpya akiwa katika klabu yake ya Porto. Wakala wa mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez mwenye umri wa miaka 28 amesema mteja alikataa uwezekano wa kwenda Tottenham Hotspurs, Liverpool na Everton ili aweze kupata nafasi ya kucheza Serie A. Klabu ya Aston Villa imeanza tena mazungumzo ya kutaka kumsajili winga wa Manchester City Scott Sinclair mwenye umri wa miaka 25, ikiwa imepita siku chake baada ya kuonekana kama dili hilo halitawezekana.

ARSENAL YAMSAJILI RASMI PAULISTA KWA EURO MILIONI 15.

KLABU ya Arsenal imemsajili rasmi beki wa Villarreal Gabriel Paulista kwa kitita cha euro milioni 15 huku wakimtoa mshambuliaji Joel Campbell kujiunga na timu hiyo kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Villarreal msimu huu na anaweza kupangwa katika mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Aston Villa. Akihojiwa Paulista amesema alifanya mazungumzo na familia yake na kuwaambia kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika Ligi Kuu hivyo mashabiki wa Arsenal wategemee mtu ambaye atajituma kadri ya uwezo wake ili kuisadia timu kushinda vitu muhimu. Arsenal walipewa kibali cha kufanyia kazi cha Paulista Jumatatu pamoja na ukweli kuwa nyota huyo hajawahi kuitumikia timu yake ya taifa na pia hatoki katika umoja wan chi za Ulaya. Paulista alijiunga na Villarreal akitokea klabu ya Vitoria ya nchini kwao Brazil mwaka 2013.

AFCON 2015: KOCHA WA IVORY COAST ADAI NDIO KWANZA KIKOSI CHEK KIMEANZA AFCON.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Herve Renard amesema michuano ya Mataifa ya Afrika sasa ndio inaanza kwa timu yake baada ya kuichapa Cameroon kwa bao 1-0 na kumaliza vinara wa kundi D. Ivory Coast sasa wanakabiliwa na kibarua kizito mbele ya Algeria wakati watakapokwaana katika hatua ya robo fainali Jumapili hii. Renard amesema kama huwezi kupenya mbele ya timu kama Cameroon au Senegal lazima watu wakunyooshee vidole kuhusiana na uwezo wake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ukiwa na timu kama Ivory Coast mashindano huwa yanaanzia robo fainali kwasababu ukitoka mapema utakuwa umeshindwa. Renard amesema hatua hiyo itakuwa ngumu kwani kila timu inataka kufika fainali na wamebakisha hatua tatu pekee kulifikia taji la michuano hiyo.

AFCON 2015: YAYA TOURE AZUSHA HOFU KUTOKANA NA MAJERUHI.

KIUNGO wa Ivory Coast Yaya Toure amezusha hofu kuhusiana na afya yake baada ya kulazimika kutolewa nje katika dakika za mwisho kwenye mchezo wa dhidi ya Cameroon. Kiungo huyo wa Manchester City alitolewa nje baada ya kukanyagwa na Stephane M’Bia lakini amesisitiza baada ya mchezo huo kuwa uwepo wake katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Algeria hauna mashaka yeyote. Toure amesema hakuna tatizo lolote kubwa la kutisha hivyo kuwaondoa hofu mashabiki wao ambao tayari waliingiwa woga wa kumkosa shujaa wao huyo katika mchezo unaofuata. Katika mchezo huo bao pekee la Ivory Coast lilifungwa na Max Gradel katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza na kuipa uongozi wa kundi D.

SIMEONE AGOMA KUKOSOA TABIA ZA WACHEZAJI WAKE.

MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amekataa kukosoa nidhamu ya kikosi chake baada ya mchezo wa jana wa Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona, akisisitiza anajivunia ari iliyoonyeshwa na wachezaji wake. Atletico walimaliza mchezo huo war obo fainali ya mkondo wa pili wakiwa wako tisa baada ya Gabi kutolewa nje kwa tukio alilofanya kipindi cha mapumziko kabla ya Mario Suarez naye kulimwa nyekundu katika dakika mwishoni na mchezo. Naye Arda Turan pia alilimwa kadi ya njano kwa kumtupia mwamuzi wa pembeni kiatu wakati Raul Garcia yeye alipewa kadi ya njano kwa kujibizana na wajumbe walikuwa katika benchi la ufundi la Barcelona wakati wa mapumziko. Hata hivyo, wakati akiulizwa kuhusiana na tabia za wachezaji wake baada ya kufungwa mabao 3-2 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2, Simeone alijibu kuwa anajivunia wachezaji wake. Simeone amesema kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri kwani walicheza vyema na kukiri kuwa Barcelona walicheza vyema kwani wako katika kiwango cha juu toka Desemba.

UWANJA WA MADRID KUBADILISHWA JINA.

KLABU ya Real Madrid inajipanga kubadili jina la Uwanja wake wa Santiago Bernabeu ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya udhamini na Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Petroli-IPIC yenye maskani yake Umoja wa Falme za Kiarabu. Wawili walikubali kushirikiana katika mkataba unaoaminika kuwa na thamani ya euro milioni 500 itakazovuna Madrid katika kipindi cha miaka 20 ijayo kuanzia Octoba mwaka huu. Mkataba huo unajumuisha haki ya kubadili jina la uwanja ambao umekuwa nyumbano kwa timu hiyo toka mwaka 1947.
Uwanja huo pia ndio uliochezewa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1982. Sasa inaaminika uwanja huo utakuwa ukiitwa The Abu Dhabi Santiago Bernabeu. Rais wa klabu hiyo Florentino Perez amesizitiza kuwa urithi wa uwanja huo utaheshimiwa kwa kuendelea kubaki na neno Santiago Bernabeu. Perez amesema dhumuni kubwa la udhamini huo ni pamoja na kuukarabati upya uwanja huo na kuuongeza mpaka kufikia uwezo wa kubeba mashabiki 91,000 kutoka 81,000 wa hivi sasa.

Wednesday, January 28, 2015

FIGO NAYE AJITOSA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS FIFA.

NGULI wa soka wa Ureno, Luis Figo ametangaza uamuzi wake wa kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu. Figo amechukua uamuzi huo wa kugombea nafasi ya hiyo siku muda kabla ya muda wa mwisho wa kutuma maombi baada ya kukusanya vielelezo vyake vikiwemo vyama vitano vya soka vinayomuunga mkono. Akihojiwa na CNN, Figo amesema anajali mpira hivyo anachikiona sasa katika taswira ya FIFA hakubaliani nacho ndio maana ameamua kugombea nafasi hiyo ili kumng’oa rais wa sasa Sepp Blatter ambaye amepanga kugombea kwa kipindi cha tano. Figo aliendelea kudai kuwa kama utaitafuta FIFA katika mtandao jambo la kwanza litakalokuja ni kashfa mbalimbali zinazoiandama katika miaka ya karibuni jambo ambalo sio zuri kwa ukuaji wa soka. Figo amesema amezungumza na watu wengi muhimu katika soka, wachezaji, mameneja, marais wa mashirikisho na wote wanadhani kunatakiw akufanyka mabadiliko. Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Barcelona, Real Madrid na Inter Milan ameungana na Jerome Champagne, Prine Ali Bin Hussein, David Ginola na Michael van Praag ambao tayari wametangaza nia hiyo ya kupambana na Blatter.

MOURINHO ALIMWA FAINI KWA UTUKUTU.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho ametozwa faini ya paundi 25,000 kwa kauli yake aliyodai kuna kampeni za makusudi zinazofanywa na waamuzi kuidhoofisha timu yake. Mourinho alitoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kukataliwa penati katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton Desemba 28 mwaka jana. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kimemtoza faini kwa kauli hiyo ambayo inaweza kuleta mkanganyiko katika soka huku akionywa kutofanya kosa kama hilo katika siku za usoni. Mbali na hilo Mourinho pia alionywa kwa kauli yake aliyotoa kabla ya mchezo kati ya Chelsea na Stoke City Desemba 22 ambao walikuja kushinda kwa mabao 2-0.

TETESI ZA USAJILI ULAYA: MADRID WATAKA KUZIBA PENGO LA COENTRAO KWA KUMCHUKUA GAYA, LIVERPOOL YAKARIBIA KUMCHUKUA LAVEZZI, PARDEW AMTAKA ZAHA MOJA KWA MOJA.

KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Real Madrid imedaiwa kutaka kuziba nafasi ya Fabio Coentrao na kuripotiwa kuwa wanajipanga kumuwinda chipukizi wa Valencia Jose Luis Gaya mwenye umri wa miaka 19. Kama Madrid watahitaji saini ya chipukizi huyo watalazimika kutoa kitita cha euro milioni 18 kilichowekwa na Valencia. Klabu ya Liverpool inakaribia kufikia makubaliano ya euro milioni 20 na Paris Saint Germain kwa ajili ya kumsajili Ezeguiel Lavezzi. Kiungo wa klabu ya Hannover Lars Stindl ameripotiwa kukaribia kukamisha usajili wake wa kujiunga na Schalke 04. Stindl mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuondoka Hannover katika majira ya kiangazi kwa kitita cha paundi milioni tatu kitakachotolewa na Schalke. Kiungo wa West Ham United Ravel Morrison anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Lazio lakini klabu hiyo ilimzuia nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 kusafiri kwenda jijini Rome jana kusaini mkataba wa awali. Gabriel Paulista anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Arsenal haraka kufuatia kuwasili kwake kutoka Villarreal na anaweza kuwepo katika mchezo dhidi ya Aston Villa utakaochezwa Jumapili. Tetesi za Darren Fletcher kuondoka Manchester United zimezaa matunda baada ya sasa klabu za West Ham United, West Bromwich Albuon na Valencia kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30. Klabu ya Crystal Palace inataka kumsajili Wilfried Zaha kwa mkataba wa moja kwa moja huku kocha Alan Pardew akitaka kutanguliza kwanza kiasi cha paundi milioni tatu na baadae kumalizia paundi milioni tatu zilizobakia.

BALE AIZODOA MAN UNITED KWA KUDAI HANA MPANGO WA KUIKACHA MADRID.

WINGA mahiri wa Real Madrid, Gareth Bale amesisitiza kuwa anafuraha kuwepo katika klabu hiyo na haoni kama anaweza kuja kuichezea Manchester United katika siku za karibuni kama inavyoripotiwa na vyombo vya habari. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea katika Ligi Kuu Uingereza kwa miezi ya hivi karibuni huku United ikitajwa ndio klabu atakayoitumikia. Hata hivyo, Bale mwenye umri wa miaka 25 ameweka wazi hana mpango wowote wa kwenda United na badala yake anataka kushinda mataji akiwa na Madrid. Bale amesema amekuwa akiulizwa mara kwa mara kama hana furaha kuwepo Madrid, jambo ambalo amekuwa akilikanusha kwani anafurahia kuitumikia timu hiyo nab ado ana miaka kadhaa katika mkataba wake. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa wanshinda mataji na anataka kuendelea kufanya hivyo akiwa Madrid. Bale amefunga mabao 12 katika mechi 26 za mashindano yote alizoichezea Madrid msimu huu.

STOKE YAPATA PIGO, BAADA YA BOJAN KUTAKIWA KUKAA NJE YA UWANJA MSIMU WOTE ULIOBAKIA.

MSHAMBULIAJI wa Stoke City Bojan Krkic anatarajiwa kuukosa msimu mzima uliobakia baada ya kuumia goti katika mchezo wa Kombe la FA mzunguko wa nne dhidi ya Rochdale uliochezwa Jumatatu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 24 ndiye aliyefunga bao la kuongoza katika mchezo huo ambao Stoke waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 lakini yeye alitolewa katika dakika ya 32 baada ya kuumia. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo huku ikidai kuwa vipimo vinaonyesha kuwa nyota huyo alichanika msuli wa ndani ya goti lake la kushoto. Stoke walimsajili mshambuliaji huyo ambaye ameitwa mara moja kuitumikia Hispania, kutoka Barcelona kwa mkataba wa miaka minne Julai mwaka jana.

FABREGAS HATIHATI KUIKOSA CITY JUMAMOSI.

KUNA wasiwasi mkubwa wa kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas kuukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya mahasimu wao katika mbio za ubingwa Manchester City Jumamosi hii kutokana na majeruhi ya msuli wa paja yanayomsumbua. Fabregas alilazimika kutolewa katika mchezo wa Kombe la Ligi ambao Chelsea ilifanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Liverpool na kutinga hatua ya fainali. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema Fabregas alitoa taarifa ya kukazkwa msuli wake wa paja na kudai kuwa alikuwa hajaumia bado ila angeweza kuumia kama angeendelea kucheza. Mbali na Fabregas pia mabeki Filipe Luis na Branislav Ivanovic na wanahofiwa kuwa majeruhi na kuukosa mchezo huo muhimu. Chelsea ndio vinara wa ligi wakitofautiana kwa alama tano na City wanaoshika nafasi ya pili.

MESSI ADAI LEO KUFA NA KUPONA LAZIMA WAITANDIKE ATLETICO.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi ameapa kufanya kila wawezalo kuifunga Atletico Madrid ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Mfalme. Timu hizo zinatarajiwa kukwaana katika Uwanja wa Vincente Calderon kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya mkondo wa pili huku Barcelona wakiongoza kwa bao 1-0 walilopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa camp Nou. Messi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook kuwa ana hamu kubwa ya mchezo huo na kwamba yeye na wachezaji wenzake wamepania kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanatinga hatua ya nusu fainali. Barcelona ilitinga hatua ya fainali ya michuano hiyo msimu uliopita lakini walijikuta wakichapwa na Real Madrid.

BARCELONA YAFIKIRIA KUWAPIGA CHINI WADHAMINI WAO QATAR.

RAIS wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema klabu hiyo inafikiria kusitisha udhamini wa fulana zao na Qatar kwasababu ya wasiwasi wa mambo ya kijamii katika taifa hilo. Akizungumza katika mahojiano Bartomeu amesema kwasasa Barcelona inaangalia uwezekano wa kupata wadhamini wengine pindi mkataba wao na Qatar utakapomaliza mwakani. Bartomeu aliendelea kudai kuwa walisaini mkataba huo miaka minne iliyopita kutokana na sababu za kiuchumi na kuongeza hivi sasa kuna masuala ya kijamii yanapaswa kuangaliwa kabla ya kusaini mkataba mpya. Barcelona walitengeneza vichwa vya habari Desemba mwaka 2010 wakati walipomaliza mgomo wao kutovaa nembo yeyote ya mdhamini katika fulana zao kwa kusaini mkataba uliokuwa na thamani ya euro milioni 30 kwa mwaka na Qatar Foundation.

ARSENAL YAMPELEKA CAMPBELL KWA MKOPO VILLARREAL ILI WAMCHUKUE PAULISTA.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Joel Campbell amejiunga na klabu ya Villarreal kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Uhamisho wa nyota huyo wa kimataifa wa Costa Rica kwenda Hispania ni sehemu ya mpango ambao Arsenal wanajipanga kumsajili beki wa Villarreal Gabriel Paulista ambaye tayari ameshafaulu vipimo vya afya katika klabu hiyo ya London kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza. Campbell alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ukiwa sambamba na picha yake akiwa amevaa skafu ya Villarreal akiwashukuru wanafamilia wa Arsenal kwa ujumbe wao wa kumtakia heri na kuahidi kuwaletea sifa. Paulista mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Arsenal katika kipindi hiki cha Januari baada ya kusajiliwa kwa mchezaji kinda kutoka Poland Krystian Bielik.

ASIA CUP 2015: AUSTRALIA KUKWAANA NA KOREA KUSINI FAINALI.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Australia, Tim Cahill anatarajiwa kuingoza timu hiyo katika mchezo wa fainali wa Kombe la Asia dhidi ya Korea Kusini utakaochezwa Jumamosi hii. Cahill ambaye katika kipindi cha maiak 17 ya usakataji kabumbu hajawahi kushinda taji lolote kubwa, hii itakuwa nafasi pekee ya kufanya hivyo kabla ya kustaafu soka. Mbele ya mashabiki 80,000 watakaohudhuria fainali hiyo itakayofanyika jiji Sydney, Cahill ataingoza Australia mbele ya mashabiki wa nyumbani kupambana na timu hiyo ngumu ya Korea Kusini. Akihojiwa mara baada ya kuitandika Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE kwa mabao 2-0 katika mchezo nusu fainali, Cahill aliwashukuru wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki wote waliokuwa wakiwaunga mkono kuanzia mwanzo. Cahill amesema ilikuwa ni safari ndefu lakini sasa wana kibarua kimoja cha kuzingatia mechi kubwa katika historia ya soka la Australia.

BAADA YA KUTINGA FAINALI KOMBE LA LIGI, MOURINHO AMKINGIA KIFUA COSTA ADAI ALIWAKANYAGA WACHEZAJI WA LIVERPOOL KWA BAHATI MBAYA.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amedai kuwa tukio la Diego Costa kuwakanyaga wachezaji wa Liverpool katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ligi, kilikuwa cha bahati mbaya. Katika mchezo huo war obo fainali Chelsea walishinda kwa bao pekee lililofungwa na Branislov Ivanovic mwanzoni mwa dakika za nyongeza baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida. Costa aliwakanyaga Emre Can na Martin Skrel katika mchezo huo wa mkondo wa pili uliofanyika katika Uwanja wa Stamford Bridge. Mourinho amesema wakati mchezaji wa upinzani akiwa amelala chini, Costa alimkanyaga kwa bahati mbaya wakati akiwajaribu kuchukua mpira. Hata hivyo kauli hiyo inapingwa vikali na meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers ambaye amesema kwa ushahidi wa picha za video inaonyesha wazi kabisa kuwa Costa aliwakanyaga wachezaji hao kwa makusudi. Chelsea sasa wanasubiria mshindi kati ya Sheffield United na Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kucheza naye fainali itakayofanyika machi mwaka huu.

AFCON 2015: BAADA YA GAHAN NA ALGERIA KUSONGA MBELE KUNDI C, LEO NI KUFA NA KUPONA KWA TIMU ZA KUNDI D.

TIMU kongwe za Ghana na Algeria jana zilifanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kushinda mechi zao za mwisho za kundi C. Ghana wenyewe walisonga mbele baada ya kutoka nyuma na kuibugiza Afrika Kusini kwa ju mla ya mabao 2-1 huku Algeria wao wakiichakaza Senegal kwa kwa mabao 2-0. Mabao ya Ghana katika mchezo huo yalifungwa na John Boye na Andre Ayew huku lile la kufutia machozi la Afrika Kusini likifungwa na Mandla Misango wakati kwa upande wa Algeria wao mabao yake yalifungwa na Riyadhi Mahrez na Nabil Bantaleb. Leo kutakuwa na mtanange mwingine wa mwisho wa makundi ambapo timu za kundi D zitakuwa uwanjani kuchuana ili kutafuta nafasi ya mbili za kwenda robo fainali zilizobakia. Katika michezo hiyo ambayo yote itachezwa kwa pamoja kuepuka upangaji matokeo wakongwe Cameroon watamenyana na Ivory Coast wengi wakifananisha mchezo huo kama fainali huku Guinea wao wakitoana jasho na Mali.

Tuesday, January 27, 2015

KINYANG'ANYIRO CHA URAIS FIFA CHAZIDI KUSHIKA KASI, RAIOLA AJITOA BAADA YA VAN PRAAG KUTANGAZA NIA.

WAKALA wa kimataifa Mino Raiola ameamua kujitoa katika mbio za kuwania urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA baada ya mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uholanzi-KNVB Michael Van Praag kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo inayoshikiliwa na Sepp Blatter. Wakala huyo ambaye anawawakilisha wachezaji kama Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic, Mario Balotelli na Henrikh Mkhitaryan, alitangaza kugombea nafasi hiyo wiki iliyopita akidai kuwa FIFA inahitajika kubadili uongozi wake. Hata hivyo, Raiola sasa anedhani Van Praag ndio mgombea mzuri katika kinyang’anyiro hicho na kujitolea kumuunga mkono. Akihojiwa Raiola amesema kugombea urais FIFA haukua kwa ajili yake kwani ilikuwa ni kwasababu ya kupata mgombea mgombea mzuri ambaye anaweza kumpa changamoto Blatter na sasa amepatikana. Raiola amesema Van Praag ni mtu ambaye yuko vizuri kimtandao huku akiwa na subira zaidi ndio maana amefurahishwa kuachia nafasi hiyo kwa mtu kama huyo. Kujitoa kwa Raiola kunamaanisha kuwa Blatter sasa atakuwa aanapata upinzani kutoka kwa wagombea wanne akiwemo Jerome Champagne, Prince Ali Bin Al Hussein, Van Praag na David Ginola.

TETESI ZA USAJILI ULAYA: COSTA AGOMA KWENDA CHELSEA JANUARI HII, ALLEGRI AZIWASHIA TAA ZA KIJANI MAN UNITED NA CHESLEA KUHUSIANA NA POGBA.

KATIKA habari za tetesi za usajili, mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Douglas Costa mwenye umri wa miaka 24 ameitaka klabu yake ya Shakhtar Donetsk kutomuuza kwenda Chelsea katika kipindi hiki cha Januari. Klabu za Manchester United na Chelsea wamepata ahueni katika mbio zao za kuwania kumsajili kiungo Paul Pogba mwenye umri wa miaka 21 baada ya meneja wa Juventus Massimiliano Allegri kudai kuwa itakuwa ngumu kukataa ofa ya paundi milioni 75 kwa ajili ya nyota huyo. Kwingineko klabu ya Man United inaweza kurudi nyuma katika mbio zao za kumsajili Kevin Strootman mwenye umri wa miaka 24 baada ya kiungo huyo wa Roma kupata majeruhi katika mchezo dhidi ya Fiorentina. Naye wakala wa winga Adnan Januzaj mwenye umri wa miaka 19 amebainisha kuwa meneja wa Man United Louis van Gaal amezuia kuondoka kwa mchezaji huyo kwenda klabu ya Paris Saint-Germain au nyingine yeyote katika kipindi hiki cha usajili wa Januari. Klabu ya Southampton inafikiria kutoa ofa kwa ajili ya kusajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Jordy Clasie mwenye umri wa miaka 23 kutoka klabu ya Feyenoord. Kwa upande mwingine Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kukosekana katika kikosi cha Chelsea kwenye mchezo wa maruadiano wa Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool. Hatua hiyo inatokana na klabu ya Wolfsburg kuwa mbioni kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anafikiria kuwasajili beki wa kulia wa Valencia Joao Pereira na beki wa kati wa AC Milan Adil Rami kabla ya kufungw akwa dirisha dogo la usajili mwezi huu.

AFCON 2015: WASIWASI WATANDA KUHUSIANA NA HALI YA USALAMA BAADA YA WENYEJI KUPENYA ROBO FAINALI.

KUFUZU kwa wenyeji Guinea ya Ikweta katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kumetengeneza wasiwasi juu ya usalama kwa waandaaji wa michuano hiyo. Wenyeji waliwashangaza majirani zao Gabon kwa kuwachapa mabao 2-0 Jumapili iliyopita na kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi A. Guinea ya Ikweta sasa itachuana na Tunisia katika hatua ya robo fainali Jumamosi hii huko Ebibeyin. Lakini kuna wasiwasi kuwa uwanja huo mpya wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 5,000 pekee utakuwa mdogo kwa ajili ya mashabiki wengi wanaotegemewa katika mchezo huo. Michuano hiyo tayari imeshashuhudia mashabiki wakibomoa na kupita katika uzio katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika Bata Januari 17 ambapo uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 ulifurika. Katika viwanja vingine mara kadhaa maeneo ya maalumu na sehemu za wanahabari zimekuwa zikivamiwa mara kadhaa na mashabiki huku polisi wakipambana kurejesha hali ya utulivu. Waandaaji sasa inabidi waangalie uwezekano wa kuupeleka mchezo huo katika Uwanja wa Bata ambao ndio mkubwa katika nchi hiyo ambapo tayari Guinea ya Ikweta wameshacheza mechi zao tatu huku mashabiki wakiwa wamejaa. Uwanja huo pia ndio utakaotumiwa kwa ajili ya mchezo wa fainali Februari 8.

RODRIGUEZ AMKINGIA KIFUA RONALDO.

KIUNGO mahiri wa Real Madrid, James Rodriguez amedai kumhusudu Cristiano Ronaldo na kupuuza taarifa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno ni mkorofi. Rodriguez alijiunga na Madrid akitokea Monaco kwa kitita cha euro milioni 80 mwanzoni mwa msimu huu na amekuwa akivutiwa na maadili ya kazi aliyonayo Ronaldo. Akihojiwa Rodriguez amesema Ronaldo ni mchezaji mwenye tabia nzuri ndani na nje ya uwanja na kwake anadhani ndio alistahili tuzo ya Ballon d’Or aliyopata kwa mafanikio aliyopata mwaka 2014. Rodriguez aliendelea kudai kuwa wamekuwa na mahusiana mazuri na nyota huyo na amekuwa akimvutia kwa jinsi anavyojituma mazoezini.

MADRID YADAI HAIKUVUNJA SHERIA KATIKA KUSAJILI WACHEZAJI WALIO CHINI UMRI.

KLABU ya Real Madrid imetoa taarifa jana ya kudai kuwa walifuata taratibu zote za kisheria zilizowekwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika usajili wa wachezaji walio chini umri wa miaka 18. Kauli hiyo imekuja kufuatia FIFA kudai kufanya uchunguzi kuhusiana na usajili wa wachezaji kadhaa walio chini umri waliosajiliwa na klabu hiyo. Mapema wakati wakimtambulisha Lucas Silva, mkurugenzi wa klabu hiyo Emilio Butragueno amesema wanajua kuwa FIFA ililiomba Shirikisho la Soka la Hispania taarifa zinazohusiana na uhamisho wa aina hiyo uliofanywa na Madrid katika kipindi cha miaka mitano. Mkurugenzi huyo amesema wataipa FIFA ushirikiano wowote watakaotaka katika uchunguzi wao kwani hawani wasiwasi kuhusu kuvunja sheria kuhusiana na suala hilo. Alhamisi iliyopita Madrid ilimsajili rasmi kiungo wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 16 kutoka klabu ya Stroemgodset. Mahasimu wao Barcelona wapo katika kifungo cha kufungiwa kusajili misimu miwili baada ya FIFA kuwakuta na hatia ya kukiuka sheria katika usajili wa wachezaji walio chini umri wa miaka 18.

MWENYEKITI WA BAYERN ADAI GUARDIOLA NI ZAIDI YA WAJERUMANI WENYEWE.

MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Pep Guardiola na kutani kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona anafanana na Wajerumani kuliko Wajerumani wenyewe. Rummenigge amesema kutokana na bidii ya kazi aliyokuwa nayo Guardiola anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wote. Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa wakati wachezaji wote wamerejea nyumbani na kupumzika katika masofa yao, Guardiola yeye huendelea na kazi akipanga mikakati kwa ajili ya mchezo ujao. Kuhusu tetesi za Guardiola kuondoka na kurejea Barcelona, Rummenigge alipuuza taarifa hizo na kudai kuwa kocha huyo ataendelea kuinoa Bayern hata katika msimu ujao wa Bundesliga.

NEYMAR ADAI HAWEZI KUMPA USHAURI SUAREZ.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar anafikiri hana nafasi ya kumpa ushauri Luis Suarez kufuatia mwanzo mgumu katika maisha yake mapya Camp Nou. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa akipambana kurejea katika kiwango chake toka atue Barcelona akitokea Liverpool mwanzoni mwa msimu huu na kupelekea kuachwa katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa La Liga mwishoni mwa wiki dhidi ya Elche. Suarez toka atue Camp Nou amezifumania nyavu mara mbili pekee katika mechi 11 alizocheza. Neymar ambaye alipitia wakati kama huo katika msimu wake wa kwanza Barcelona wa 2013-2014, haamini kama yeye ni mtu sahihi wa kumpa ushauri mchezaji mwenzake huyo kukabiliana na hali hiyo. Akihojiwa Neymar amesema suala hilo litakuwa gumu kwake kwakuwa mchezaji huyo kwanza amemzidi umri na pia ana uzoefu mkubwa kuliko yeye hivyo anadhani nyota huyo anapaswa kumpa ushauri yeye.

VAN PERSIE ADAI HAJUI HATMA YAKE UNITED.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Robin van Persie amekiri hajui kama atapewa ofa ya mkataba mpya wakati ule wa sasa utakapomalizika mwaka 2016. Akihojiwa nyota huyo wa wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 31, amesema hilo sio suala lake kujua kwani anachofahamu kwasasa atakuwepo Old Trafford kwa miezi 18. Van Persie amesema baada ya kumaliza makataba wake hajui kitakaochoendelea baada ya hapo kwani anaweza kuwepo au kuondoka kwenda kwingine. Nyota huyo pia hadhani kama amefunga mabao ya kutosha toka kuanza kwa msimu huu hivyo amepania kuongeza bidii na kuhakikisha anafunga mabao mengi zaidi ili kuisadia timu yake. Van Persie mpaka sasa amefunga mabao nane katika mechi 21 za mashindano yote alizocheza msimu huu na kumaanisha kuwa itakuwa ngumu kufikia rekodi yake ya mabao 18 katika mechi 30 alizocheza katika msimu wake wa kwanza akitokea Arsenal mwaka 2012.

AFCON 2015: DRC, TUNISIA ZAUNGANA NA GUINEA YA IKWETA NA CONGO KATIKA ROBO.

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo-DRC imekuwa timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kusonga hatua ya robo fainali ya michuano Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia. DRC imesonga mbele wakiwa washindi wa pili wa kundi B nyuma ya Tunisia ambao wao nao wamepita kama vinara wa kundi hilo. Pamoja na DRC kumaliza wakiwa na alama sawa na Cape Verde idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga ndio yaliyowavusha. Mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2012 Zambia ambayo ndio timu nyingine inayotoka katika ukanda wa huu walishindwa kufurukuta mbele ya Cape Verde na kutoka sare ya bila kufungana hatua ambayo imewafanya kumaliza wakiburuza mkia wa kundi hilo. Leo kutakuwa na kinyang’anyiro kingine cha kugombea nafasi mbili za juu kutinga robo fainali katika kundi C ambapo Senegal watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Algeria huku Afrika Kusini nao wakipepetana na Ghana. Kundi kama ilivyo mengine liko wazi ambao timu itakayoibuka na ushindi itakuwa imejiwekea nafasi nzuri yakusonga mbele.

Monday, January 26, 2015

RATIBA YA FA: ARSENAL WAPANGWA NA WABABE WA CITY, MAN UNITED KUENDELEA KUPETA KAMA WAKISHINDA MECHI YAO YA MARUDIANO DHIDI YA CAMBRIDGE.

MABINGWA watetezi Arsenal wamepangwa na timu ya daraja ya kwanza la Middlesbrough katika mzunguko wa tano wa michuano ya Kombe la FA. Middlesbrough ambao waliing’oa Manchester City katika mzunguko wa nne wataifuata Arsenal katika uwanja wao wa Emirates mwishoni mwa wiki ya Februari 14 na 15 mwaka huu. Bradford City waliopo ligi daraja la pili wao wamezawadiwa kwa kuitoa Chelsea kwa kupewa mchezo wa nyumbani dhidi ya aidha Sunderland au Fulham. Mshindi katika mchezo kati ya Cambridge United na Manchester United anatarajiwa kukutana na aidha Preston au Sheffield United. Katika michezo mingine ya mzunguko wa tano Crystal Palace wao watakuwa wenyeji wa mshindi kati ya Liverpool au Bolton Wanderers wakati Aston Villa watakwaana na Leicester City na West Bromwich Albion wao watachuana na West Ham United.

Saturday, January 24, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: JUVENTUS KUMUUZA POGBA KWA EURO MILIONI 100 KIANGAZI, CHELSEA YAONGEZA DAU KWA COSTA.

KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Juventus imepanga kumuachia Paul Pogba kama watapewa ofa ya paundi milioni 100 katika kipindi cha majira ya kiangazi. Klabu za Manchester City, United na Chelsea zinamfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kama ilivyo kwa klabu za Paris Saint-Germain na Bayern Munich. Chelsea wameongeza ofa yao kufikia euro milioni 25 kwa ajili ya kumsajili Douglas Costa huku wakijipanga pia na kumsajili Juan Cuadrado wa Fiorentina. Nyota hao wa Amerika Kusini wanategemewa kutua Stamford Bridge kuja kuziba nafasi ya za Andre Schurrle na Mohamed Salah ambao wanatarajiwa kuondoka katika kipindi hiki cha usajili wa Januari. Manchester United wameamua kumvalia njuga beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne ambapo wamemua kumtengea ofa ya kitita cha euro milioni 27. Meneja wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp anajipanga kumfukuzia mshambuliaji wa Monaco Dimitar Berbatov katika kipindi hiki cha usajili wa Januari. Nyota huyo alimuambia Redknapp kuwa anataka kurejea katika Ligi Kuu huku akidaiwa kuigharimu QPR euro milioni 1.3 kama wakimchukua. Klabu za Manchester United na Arsenal zinapigana vikumbo katika kumfukuzia nyota wa klabu ya Dinamo Moscow Aleksandar Dragovic ambapo meneja Arsene Wenger ameamua kutuma maskauti wake kumuangalia katika mchezo wa kirafiki. Wenger anamchukulia mchezaji huyo kama karata yake ya pili kama akishindwa kumsajili Gabriel Paulista.

Friday, January 23, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: CHELSEA YAKUBALI KUIPA FIORENTINA PAUNDI MILIONI 23 KWA AJILI YA CUADRADO, MAN UNITED YAMVIZIA ALVES KIANGAZI.

KATIKA habari tetesi za usajili, klabu ya Chelsea hatimaye imefikia makubaliano na klabu ya Fiorentina kwa ajili ya kumsajili Juan Cuadrado kwa kitita cha paundi milioni 23. Chelsea sasa wameruhusiwa kuzungumza na nyota huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 26 kwa ajili ya makubaliano binafsi wakati wakijipanga kumuuza Mohamed Salah. Arsenal wameingia katika kinyang’anyiro cha kumuwania kiungo wa Roma Radja Nainggolan lakini wanakabilwia na kibarua kizito kutoka na klabu za Manchester United na Chelsea nazo kumuwinda kiungo huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 26. Manchester United wanazidisha kupata uhakika wa kumsajili Dani Alves kutoka Barcelona kwa uhamisho huru katika majira ya kiangazi. Kocha wa United Louis van Gaal amepania kumsajili beki huyo wa kulia na anamatumaini Victor Valdes anaweza kumshawishi mchezaji mwenzake wa zamani kuhamia Old Trafford. Kiungo Yann M’Vila amerejea katika klabu yake ya Rubin Kazan baada ya Inter Milan kuamua kutengua mkpo wa mchezaji huyo kufuatia kuonyesha kiwango kibovu. Liverpool nao wanajipanga kutoa ofa kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez kabla ya dirisha la usajili wa Januari halijafungwa. Winga huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua wiki hii. Manchester United wanajipanga kufanya usajili wa wachezaji watatu wakubwa katika majira ya kiangazi ambapo kocha Louis Van Gaal amepanga kuwasajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels na beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne.

MADRID YAMNASA LUCAS SILVA.

MAKAMU rais wa klabu ya Cruzeiro Marcio Rodriguez amedai kuwa uhamisho wa Lucas Silva kwenda Real Madrid umeshafikia hatua nzuri ya makubaliano. Kwa kipindi kirefu Madrid iliyo chini Carlo Ancelotti imekuwa ikimfukuzia kiungo huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 21. Rodriguez amesema uhamisho wa Silva tayari umekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni Madrid wenyewe kutangaza rasmi. Rodriguez aliendelea kudai kuwa hawata pata tabu kutafuta mbadala wake kwani kuna wachezaji wengi ambao wako tayari kupandishwa.

TER STEGEN AAPA KUPIGANIA NAMBA BARCELONA.

GOLIKIPA wa kimataifa wa Ujerumani Marc-Andre Ter Stegen amekiri kuwa hana furaha katika nafasi yake kama gilikipa namba mbili na amejipanga kuhakikisha anakuwa kinara wa klabu ya Barcelona. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na Barcelona akitokea Borussia Monchengladbach Mei mwaka jana lakini kocha Luis Enruque anamtegemea zaidi Claudio Bravo kama kipa namba moja. Hata hivyo, Ter Stegen bado anamatumaini kuwa ataweza kumzidi uwezo golikpa huyo wa kimataifa wa Chile wakati wowote katika msimu huu unaondelea. Akihojiwa Ter Stegen amesema anafurahia anavyoungwa na mkono na mashabiki na kazi anayofanya na wachezaji wenzake lakini hafurahishwi na kuwa kwake chaguo la pili.

WENGER ADAI ALISHINDWA KUMSAJILI DI MARIA AKIWA KINDA KUTOKANA NA KANUNI ZA VIBALI VYA KAZI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye Umoja wa Ulaya zifutwe. Wenger anajaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambaye atahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake. Kocha huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezaji toka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya katika Ligi Kuu Uingereza msimu ujao. Kwasasa kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo Umoja wa Ulaya kinahitaji mchezaji awe anatoka katika nchi zilizo ndani ya nafasi 70 za viwango vya FIFA na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili. Chama cha Soka cha Uingereza kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa Umoja wa Ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi. Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora zaidi kwa ajili ya wachezaji chipukizi wa nchi hiyo. Wenger amesema alitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria wakati akiwa na umri wa miaka 17 lakini kibali cha kazi kikaleta shida.

BENITEZ ASISITIZA KUBAKIA NAPOLI.

MENEJA wa Napoli Rafa Benitez amesisitiza anafurahi kuwepo katika klabu hiyo na anatarajia kufanya mazungumzo kuhusiana na mustakabali mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa sasa kocha huyo na klabu hiyo unatarajiwa kumalizika Juni mwaka huu. Benitez amesema anatarajia kuzungumzia mustakabali wake na rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis mwanzoni mwa kiangazi huku akidai kuwa hajafanya mazungumzo na klabu yeyote. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anafurahi kuinoa Napoli ndio maana anataka kuendelea kubakia hapo na kuiwezesha timu hiyo kunyakuwa mataji.

AUBAMEYANGA AKIRI KUCHEZA CHINI YA KIWANGO.

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amekiri kuwa chini ya kiwango katika mchezo waliofugwa dhidi ya Congo Brazzaville juzi. Baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wao wa ufunguzi Jumamosi iliyopita, Gabon walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo lakini mambo yalibadilika baada ya Congo kuwafunga bao 1-0. Aubemeyang ambaye alikuwa nyota katika mchezo wao wa kwanza amekiri kuwa hakuwa katika kiwango chake katika mchezo dhidi ya Congo. Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani amesema walishindwa kutengeza na kutumia mchezo wao hali ambayo iliwafanya kuiga mchezo wa wapinzani jambo lililokuwa baya kwao. Hata hivyo, Aubameyang anaamini wanaweza kuamka katika mchezo wa mwisho na kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Gabon itamaliza mechi zake za makundi kwa kucheza na wenyeji Guinea ya Ikweta Jumapili hii.

RONALDO ANAWEZA KUITUMIKIA MADRID KWA MIAKA 10 ZAIDI - MENDES.

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amedai kuwa mteja wake huo bado ana miaka 10 zaidi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mapema mwezi huu alinyakuwa tuzo yake ya tatu ya Ballon d’Or ikiwa ni ya pili toka atue Santiago Bernabeu lakini hivi karibuni amekaririwa akidai kuwa anafikiria kuhamia nchini Brazil kabla ya kutundika daruga zake. Hata hivyo wakala huyo Jorge Mendes ana uhakika Ronaldo atamalizia soka lake akiwa Madrid huku akidai kuwa nyota huyo bado ana miaka 10 zaidi ya kucheza soka katika kiwango cha juu. Mendes amesema ana uhakika Ronaldo atastaafu akiwa Madrid na umri wa miaka 38 au 39 kwasababu bado ana miaka mingi ya kucheza soka. Mendes aliendelea kudai kuwa kikubwa kinachomfanya kuamini kwamba anaweza kufikia huko ni kutokana na jinsi anavyojiweka fiti mpaka kuwa mfano kwa wachezaji wenzake.

Thursday, January 22, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: CHELSEA YAMTENGEA PAUNDI MILIONI 40 WINGA WA FIORENTINA, UNITED NAO WAINGIA KATIKA MBIO ZA KUMUWANIA PAULISTA.

KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Chelsea inaripotiwa kuanza mazungumzo na Fiorentina kwa ajili ya kumsajili winga wa kimataifa wa Colombia Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka 26 katika kipindi hiki cha usajili. Vinara hao wa Ligi Kuu wanadaiwa kuongeza nguvu katika harakati zao za kumsajili winga huyo baada ya ofa yao ya paundi milioni 20.6 kukataliwa jana. Chelsea wanadaiwa kutaka kufidia gharama za Cuadrado kwa mauzo ya winga Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 22 au mshambuliaji Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24. Schurrle anaripotiwa kujipanga kurejea katika klabu ya Wolfsburg ya nchini kwake Ujerumani. Mbali na hayo Chelsea pia inahusishwa na taarifa za kutenga kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili ya kumuwania kiungo wa Juventus Paul Pogba mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliondoka Manchester United mwaka 2012. Klabu ya Valencia nayo imejipanga kuizidi kete Liverpool kwa kusajili kiungo wa Manchester James Milner mwenye umri wa miaka 26. Arsenal wanatarajiwa kuchuana na Manchester United katika kuwania kumsajili beki wa kati wa Villarreal Gabriel Paulista ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 16.

MAN UNITED YAKWEA MPAKA NAFASI YA PILI KATIKA ORODHA YA VILABU TAJIRI DUNIANI.

KLABU ya Manchester United imerejea tena katika orodha za juu za vilabu tajiri ambapo sasa wamepaa mpaka nafasi ya pili katika klabu zinazoingiza fedha nyingi wakiwa nyuma ya vinara ya Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo, mapato ya vilabu 20 tajiri vilivyomo katika orodha hiyo yamepanda mpaka kufikia euro bilioni 6.79 kwa msimu wa 2013-2014 ikiwa ni ongezeko la euro milioni 873 ukilinganisha na misimu ya nyuma. Mabingwa Ulaya Madrid wao wanaongoza orodha hiyo kwa miaka 10 mfululizo lakini Ligi Kuu Uingereza imeendelea kuonyesha kwamba wana nguvu za kiuchumi kwa nane kutoka huko kuingia katika orodha hiyo. Pamoja na msimu mbovu waliokuwa nao msimu uliopita United bado imepaa kwa nafasi mbili na kuwa klabu ya pili duniani inayoingiza fedha nyingi zaidi duniani kutokana na mapato ya euro milioni 565. Klabu za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zote zimechomoza katika orodha ya 10 bora wakati Tottenham Hotspurs wao wapo katika nafasi ya 20 bora sambamba na Newcastle United na Everton wanaongia katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza. Barcelona waliokuwa wakishika nafasi ya pili safari hii wameanguka mpaka nafasi ya nne kwa kuingiza mapato ya euro milioni 528 huku mabingwa Bayern Munich wao wakiwa nafasi ya tatu kwa kuingiza euro milioni milioni 531. Paris Saint-Germain wako katika nafasi ya tano wakiingiza kiasi cha milioni 517 wakifuatiwa na Manchester City katika nafasi ya sita wakiliongiza euro milioni 452, nafasi ya ssaba inakwenda kwa Chelsea waliongiza euro milioni 423. Wengine ni Arsenal katika nafasi ya nane waliongiza euro milioni 412.3 wakifuatiwa na Liverpool katika nafasi ya tisa waliongiza kiasi cha euro milioni 334 na Juventus ndio wanaofunga orodha ya 10 bora kwa kuingiza euro milioni 279.4. Kwa upande wa timu nyingine za Uingereza zilizopo katika orodha ya 20 bora, Spurs wao wako katika nafasi ya 12 kwa kuingiza kiasi cha euro milioni 104.9 wakati Newcastle waliongiza euro milioni 169.4 na Everton euro milioni 157.3 wako katika nafasi ya 19 na 20.

RONALDO AZIKATA MAINI MAN UNITED NA CHELSEA KWA KUDAI HANA MPANGO WA KWENDA UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amewanyong’onyesha mashabiki wa klabu za Manchester United na Chelsea baada ya kudai kuwa amepanga kwenda kumalizia soka lake nchini Brazil mara baada ya kuondoka Hispania. Wadau wengi walikuwa akitabiri kuwa Ronaldo anaweza kurejea United mara baada ya kumaliza mkataba wake Madrid lakini mwenyewe amekaririwa na gazeti la Metro akidai kutimkia Brazil katika klabu za Corinthians au Flamengo. Ronaldo ambaye ameitumikia United kwa muda wa miaka sita kabla ya kuhamia Madrid mwaka 2009 amekuwa akieleza mapenzi yake kwa mashabiki wa timu hiyo huku akihusihwa pia na kwenda Chelsea. Ronaldo alikaririwa akidai kuwa Corinthians na Flamengo ni vilabu vikubwa ambavyo anaweza kucheza katika mojawapo kwani amekuwa na marafiki wengi sana Brazil.