RAIS wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesisitiza kuwa nahodha Philipp Lahm bado ni mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kufuatia tetesi kuwa anaweza kustaafu mwakani. Tetesi zimeibuka kuwa beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kupewa nafasi ya ukurugenzi wa michezo wa klabu hiyo kama akitundika daruga zake mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo, Hoeness anataka Lahm amalize mkataba wake ambao utaishia mwaka 2018 kabla ya hajafikiria kibarua kingine Allianz Arena. Hoeness ambaye alichaguliwa tena kuiongoza Bayern wiki iliyopita, amesema anadhani Lahm bado ni mchezaji mzuri awapo uwanjani ana angependa amalize kwanza mkataba wake ndio afikirie suala la kustaafu.
Wednesday, November 30, 2016
BOSI WA PIRELLI ATAKA KUMPELEKA MESSI INTER MILAN.
MWENYEKITI wa kampuni ya Kutengeneza matairi ya Pirelli, Marco Tronchetti Provera ambao ndio wadhamini wakubwa wa Inter Milan amesema bado ana matumaini ataweza kutimiza ndoto za kumleta Lionel Messi katika klabu hiyo kutoka Barcelona. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kwa mara nyingine mustakabli wake umeleta mjadala mkubwa katika wiki za karibuni huku kukiwa na tetesi kuwa mazungumzo hayaendi kama yalivyotarajiwa Camp Nou. Taarifa zinadai kuwa mkurugenzi wa michezo wa Paris Saint-Germain-PSG Patrick Kluivert ameshazungumza na baba yake ya Messi kujadili uwezekano wa nyota huyo kwenda kwa mabingwa hao wa Ligue 1. Pamoja na hayo, Messi mwenyewe mara zote amekuwa akisisitiza kuwa anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Newell’s Old Boys ya Argentina wakati muda wake Barcelona utakapomalizika. Provera amesema lengo lake ni kumshawishi nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 kufikiria kuichezea Inter.
KLOPP AAPA KUMLINDA WOODBURN.
BARCELONA YAMUWANIA MKONGWE WA CROATIA.
KLABU ya Barcelona inadaiwa kukaribia kukamilisha usajili wa Darijo Srna kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu. Mabingwa Hispania wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi upande wa kulia lakini wanakabiliwa na ukata katika bajeti yao ya usajili wa dirisha dogo lakini Srna anaweza kuondoka Shakhtar Donetsk bure. Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia alikuwa akitaka kuondoka Ukraine kipindi kirefu na mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona Robert Fernandez amekuwa akifanya naye mawasiliano. Barcelona wanaweza kusajili kumsajili mchezaji ghali kama wakiuza mchezaji huku Aleix Vidal akiwa mchezaji pekee ambaye anaweza kuwapatia fedha hizo wanazohitaji.
ATLETICO NACIONAL YAIOMBA CONMEBOL KUWAPATA TAJI CHAPECOENSE.
KLABU ya Atletico Nacional jana wamelitaka Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL kuwapa taji la Copa Sudamericana wapinzani wao klabu ya Chapecoense ya Brazil kama heshima kwa wachezaji wa timu hiyo waliokufa katika ajali ya ndege. Klabu hiyo ya Colombia imetuma maombi hayo CONMEBOL kwa maandishi wakilitaka shirikisho hilo kuwapata taji hilo kwa heshima ya wale waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Chapecoense na Atletico Nacional zilikuwa zikutane leo katika fainali ya mkondo wa kwanza wa michuano ya Copa Sudamercana, michuano ya pili kwa ukubwa katika bara la Amerika Kusini baada ya ile ya Copa Libertadores. Taarifa kutoka CONMEBOL zilizotoka mapema ziliahirisha shughuli zote ikiwemo mchezo huo mpaka watakapotoa taarifa zaidi. Mamlaka nchini Colombia zinadai kuwa watu sita kati ya 81 ndio waliopona katika ajali hiyo.
Thursday, November 24, 2016
BALE KUIKOSA EL CLASICO.
KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa Gareth Bale anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki ijayo kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu yanayomsumbua na anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi kirefu. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alipata matatizo hayo katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata Madrid dhidi ya Sporting Lisbon katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika juzi. Mapema jana Madrid walibainisha kuwa bado wanafuatilia hali ya nyota huyo lakini leo zimekuja habari mbaya zaidi kufuatia taarifa kuwa atalazimika kufanyiwa upasuaji. Katika taarifa yao Madrid wamedai kuwa jopo la matabibu wa klabu hiyo wameamua kufamyia upasuaji nyota huyo ili kutibu tatizo lake hilo. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Bale atafanyiwa upasuaji huo Jumanne ijayo.
JELA YANUKIA KWA ETO'O KUFUATIA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI.
VYOMBO vya habari vya Hispania vimedai kuwa, mshambuliaji nyota wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o anaweza kukabiliwa na kifungo jela cha miaka zaidi ya 10. Taarifa hizo zinadai kuwa waendesha mashitaka nchini humo wanamtuhumu Eto’o kwa makosa ya ukwepaji kodi wakati akiwa Barcelona. Eto’o mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki anatuhumiwa kuwa alikwepa zaidi ya euro milioni 3.46. Tuhuma zinakuja kufuatia Eto’o kudaiwa kukataa kuweka wazi mapato yake aliyokuwa akipata kupitia kwa wadhamini wake ikiwemo kampuni ya iliyokuwa ikimtengenezea viatu.
GERRARD ATUNDIKA DALUGA ZAKE.
NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na Liverpool, Steven Gerrard ametangaza kustaafu soka baada ya kucheza kwa miaka 19. Gerrard mwenye umri wa miaka 36, ameichezea Liverpool mara 710 akishinda mataji nane makubwa lakini alijiunga na klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani mwaka 2015. Nguli pia anashika nafasi ya nne miongoni mwa wachezaji walioichezea Uingereza mechi nyingine zaidi akiwa amecheza mechi 114 huku akiwa nahodha mara tatu kati sita alizocheza katika michuano mikubwa. Akihojiwa Gerrard amesema anajiona mwenye bahati kupata uzoefu huo mkubwa katika kipindi chote alichokuwa akicheza soka. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa akiwa chipukizi alitimiza ndoto zake za kuvaa jezi nyekundu maarufu za Liverpool wakati alipoitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Blackburn Rovers Novemba 1998.
TANANIA YASHUKA VIWANGO FIFA.
TANZANIA imeendelea kuporomoka zaidi katika viwango vya ubora vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Mwezi uliopita Tanzania iliporomoka kwa nafasi 12 mpaka kufikia nafasi ya 144 lakini safari hii hali imezidi kuwa mbaya kufuatia kushuka kwa nafasi 16 zaidi mpaka kufikia nafasi ya 160 duniani na nafasi ya 48 kwa upande wa Afrika. Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki Uganda bado wameendelea kuwa vinara kwa kushika nafasi ya 73 duniani na 18 kwa Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 89 na 21 kwa Afrika. Rwanda wao wamepanda kwa nafasi sita mpaka nafasi ya 101 duniani na ya 27 kwa Afrika, wanafuatiwa na Burundi waliopo nafasi ya 133 duniani na 39 kwa Afrika. Kwa upande wa Afrika Orodha hizo zinaongezwa na Senegal walioko nafasi ya 33 baada ya kushuka nafasi moja wakifuatiwa na Ivory Coast walioshuka nafasi nne mpaka ya 34 na kulingana na Tunisia waliopanda kwa nafasi nne. Kwa upande mwingine Misri wamerejea tena katika tano bora baada ya kupata kwa nafasi 10 mpaka nafasi ya 36 wakifuatiwa na Algeria ambao wameshuka kwa nafasi tatu mpaka nafasi ya 38.
Wednesday, November 23, 2016
IBRAHIMOVIC KUPEWA MSIMU MMOJA ZAIDI UNITED.
MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amethibitisha kuwa Zlatan Ibrahimovic ataendelea kubakia katika klabu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2017-2018. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Mourinho amesema wanafurahia kuwa na Ibrahimovic hivyo wana mpango wa kumuongeza msimu mwingine wa pili. Mourinho aliendelea kudai kuwa baada ya miaka miwili anaweza kufanya anachotaka kwasababu atakuwa huru ila kwasasa bado wataendelea kuwa naye. Ibrahimovic alisajiliwa United kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Paris Saint-Germain huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine.
PICHA ZA VIDEO ZAMUWEKA MATATANI DRINKWATER.
KIUNGO wa Leicester City, Danny Drinkwater ameshitakiwa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa tuhuma za kumpiga kiwiko mchezaji wa Watford Valon Behrami. Tukio hilo lilitokea wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ambao Leicester walichapwa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita, lakini mwamuzi wa mchezo huo hakuling’amua tukio hilo. Drinkwater amepewa muda mpaka leo usiku awe amejibu tuhuma za tukio hilo ambalo lilichunguzwa na jopo la waamuzi kupitia picha za video. Jopo la waamuzi hao kila mmoja atapata nafasi ya kulitizama tukio kwa makini kabla ya kuamua kutoa uamuzi wao.
ISCO ATAKA MKATABA MWINGINE MADRID.
KIUNGO wa Real Madrid, Isco amedai kutaka kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu. Nyota huyo amewahi kukaririwa kipindi cha nyuma akidai kuwa anaweza kuondoka Madrid ili aweze kupata nafasi zaidi ya kucheza seemu nyingine lakini katika wiki za karibuni ameimarika na kuwa mchezaji muhimu katika timu hiyo. Isco mwenye umri wa miaka 24 ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo yake na sasa anataka kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo. Akihojiwa Isco ambaye alikuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa Tottenham Hotspurs, amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Madrid lakini yeye pamoja na klabu wanataka kuongeza mkataba hivyo ana matumaini kila kitu kitakwenda sawa. Isco aliendelea kudai kuwa kwasasa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo anafurahia kwani anaisaidia timu.
KINDA LA GENK LATOA MASHARTI MAZITO KWA MAN UNITED.
WINGA wa klabu ya Genk, Leon Bailey amesisitiza kuwa atakataa nafasi ya kusaini Manchester United kama timu hiyo haitamuhakikishia nafasi ya kuwepo katika kikosi cha kwanza. Chipukizi huyo wa kimataifa wa Jamaica mwenye umri wa miaka 19, anatajwa kama mmoja wa wachezaji wanaovutia nchini Ubelgiji na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na klabu kubwa. Paris Saint-Germain-PSG na Ajax Amsterdam zote zinatajwa kuwa zilijaribu kumsajili majira ya kiangazi wakati United nao pia wanaaminika kumfuatilia kwa karibu chipukizi huyo. Lakini Bailey mwenyewe ameweka wazi kuwa hana haraka yeyote ya kuondoka Genk kwasasa na kama akiondoka basi atakwenda katika klabu itakayoweza kumuhakikishia naafsi ya kucheza. Bailey amefunga mabao nane katika mechi 25 za mashindano yote alizocheza msimu huu.
POCHETTINHO AWATUPIA LAWAMA WACHEZAJI WAKE.
MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amedai kuwa wachezaji wake walikosa ubora uliohitajika ili kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka kwa Monaco kilitosha kuwaengua katika michuano hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Pochettino amesema wanahitaji kuimarika zaidi kiakili na kuwa tayari kwa kila mechi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kutokea mwanzoni mwa msimu alisema changamoto yao kubwa sio nguvu bali ni ufundi wa kuweza kuziweka akili tayari kucheza Jumamosi na baadae Jumanne au Jumatano.
BAADA YA KUFUZU CHAMPIONS LEAGUE LEICESTER SASA NGUVU ZOTE LIGI KUU.
MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amedai kuwa kikosi chake sasa kinapaswa kuhamishia ubora wao walioonyesha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenda katika Ligi Kuu. Leicester walifuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo huku wakiwa wamebaki na mechi moja mkononi ka kuitandika Club Brugge ya Ubelgiji kwa mabao 2-1 jana. Lakini pamoja na kufanya vyema Ulaya hali imekuwa tofauti nyumbani kufuatia kupoteza mechi sita kati ya 12 za Ligi Kuu walizocheza msimu huu huku wakishika nafasi ya 14. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ranieri amesema kuwa sasa mawazo yao yanahamia katika Ligi Kuu. Leicester walikwenda katika mchezo huo wakihitaji alama moja ili wafuzu lakini walifanikiwa kuondoka na alama zote tatu na kuongoza kundi G.
HISTORIA YAWEKWA MCHEZO WA DORTMUND NA LEGIA.
KLABU ya Borussia Dortmund jana ilifanikiwa kuigaragaza Legia Warsaw ya Poland kwa mabao 8-4 na kuweka historia ya kuwa mchezo uliofungwa mabao mengi zaidi katika historia ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Jumla ya mabao 12 yalifungwa katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Westfalen na kuipita rekodi ya ya mabao 8-3 ya Monaco dhidi ya Deportivo La Coruna mwaka 2003. Mpaka dakika ya 22 kipindi cha kwanza tayari yalikuwa yameshafungwa jumla ya mabao saba, wakati Marco Reus akiifungia hat-trick Dortmund. Legia pia inakuwa klabu ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kufunga mabao manne halafu kuja kupoteza mchezo.
Tuesday, November 22, 2016
CAF YATOA ORODHA YA MWISHO YA WACHEZAJI BORA AFRIKA.
For the African Player of the Year, they are;
1. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borrusia Dortmund)
2. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
3. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)
5. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)
For the African Player of the Year (Based in Africa), the top five are;
1. Khama Billiat (Mamelodi Sundowns & Zimbabwe)
2. Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns & South Africa)
3. Rainford Kalaba (TP Mazembe & Zambia)
4. Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns & South Africa)
5. Denis Onyango (Mamelodi Sundowns & Uganda)
*Sherehe za kutangaza mshindi zitafanyika huko Abuja, Nigeria Januari 5 mwakani.
1. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borrusia Dortmund)
2. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
3. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)
5. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)
For the African Player of the Year (Based in Africa), the top five are;
1. Khama Billiat (Mamelodi Sundowns & Zimbabwe)
2. Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns & South Africa)
3. Rainford Kalaba (TP Mazembe & Zambia)
4. Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns & South Africa)
5. Denis Onyango (Mamelodi Sundowns & Uganda)
*Sherehe za kutangaza mshindi zitafanyika huko Abuja, Nigeria Januari 5 mwakani.
IBRAHIMOVIC KUTENGENEZEWA SANAMU LAKE SWEDEN.
MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kutengenezewa sanamu kwa heshima yake baada ya kutajwa mchezaji bora wa Sweden kwa miaka 10 mfululizo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alitwaa tuzo hiyo ya Mpira wa Dhahabu jana katika sherehe zilizofanyika jijini Stockholm. Sanamu hilo linatarajiwa kukaa nje ya Uwanja wa Friends Arena uliopo Stockholm ambako Ibrahimovic alifunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Uingereza mwaka 2012. Akihojiwa Ibrahimovic amesema jambo hilo ni kubwa sana kwake kwani watu wengi huwa hawapati heshima ya kutengenezewa sanamu mpaka wanafariki dunia. Ibrahimovic ambaye alistaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya Ulaya mwaka huu, amefunga mabao 62 katika mechi 116 alizochezea Sweden huku akishinda mataji la ligi katika nchi nne tofauti.
JUSTIN BIEBER AVAMIA MAZOEZI YA BARCELONA.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic kesho kufuatia kurejea mazoezini baada ya kuugua. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amefanikiwa kupona maradhi yaliyomlazimu kushindwa kucheza mchezo wa La Liga dhidi ya Malaga Jumamosi iliyopita. Lakini mapema jana Messi alifanya mazoezi na wenzake ambako waliungana na mwanamuziki wa mashuhuri duniani wa muziki wa pop Justin Bieber. Barcelona wanaongoza kundi C kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Manchester City na wanahitaji ushindi katika mchezo wao wa kesho ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya timu 16 bora.
DESCHAMPS KUMUITA TENA BENZEMA UFARANSA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amekiri kuwa Karim Benzema anaweza kumuita tena katika kikosi chake lakini amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid atarejea pale tu atakapoona ana umuhimu. Benzema hakuitwa katika kikosi cha nchi hiyo katika michuano ya Euro 2016 ambapo Ufaransa ilitinga fainali katika ardhi yao ya nyumbani, kufuatia kashfa iliyokuwa ikimkabili dhidi ya mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 hajaiwakilisha nchi yake toka Octoba mwaka 2015 lakini Deschamps sasa yuko tayari kumjumuisha katika kikosi chake siku zijazo. Akihojiwa Deschamps amesema hana tatizo lolote na Benzema kwani ni mchezaji muhimu kwa Ufaransa lakini uamuzi aliochukua huko nyuma wa kumuacha ilikuwa ni kwa manufaa ya timu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anaweza kumuita tena Benzema siku za usoni lakini ni kama tu ataona kutakuwa na manufaa kwa timu.
BAYERN KUMKOSA NEUER KESHO.
KIPA wa Bayern Munich, Manuel Neuer anatarajia kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho watakaocheza dhidi ya Rostov nchini Urusi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amepata majeruhi ambayo yatamlazimu kubakia Munich kwa ajili ya matibabu huku Tom Starke na Sven Ulreich mmojawapo akitarajiwa kuchukua nafasi yake. Bayern ambao walitandikwa bao 1-0 na Borussia Dortmund katika mchezo wa Bundesliga Jumamosi iliyopita, tayari wameshafuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo na wanashikilia nafasi ya pili katika kundi D wakiwa na alama tisa baada ya kucheza michezo minne. Atletico Madrid ya Hispania ndio wanaoongoza kundi hilo kwa kuwa na alama 12 wakati Rostov na PSV Eindhoven ya Uholanzi wao wakiwa na alama moja kila mmoja huku kukiwa kumebaki michezo miwili.
MASHABIKI WA SEVILLA NA JUVENTUS WAPIGANA.
MASHABIKI wa Juventus na Sevilla jana usiku wamepigana na kupeleka shabiki mmoja Muitaliano kuumia vibaya baada ya kuchomwa kisu na wengine watatu kuumia. Taarifa kutoka nchini Hispania zinadai kuwa kundi la watu wapatao 30 lilikwenda katika bar moja iliyoko kituo cha kihistoria cha jiji hilo la Sevilla ambapo kulikuwa na mashabiki wa Juventus. Picha za video zimeonyesha ugomvi mkubwa ukizuka miongoni mwa mashabiki hao ikiwemo shabiki mmoja akirusha kiti baada ya kutoka nje ya bar hiyo kabla ya polisi hawajaingilia kati na kuwatuliza. Sevilla na Juventus zinatarajiwa kukwaana katika Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan baadae leo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
LEICESTER MBIONI KUANDIKA HISTORIA NYINGINE.
KLABU ya Leicester City baadae leo inaweza kuweka historia nyingine kwa kutinga hatua ya 16 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama wakiepuka kufungwa na Club Brugge. Leicester pamoja na kusuasua katika Ligi Kuu msimu huu, hali imekuwa tofauti Ulaya kwani ndio wanaongoza kundi G kwa tofauti ya alama tatu huku wakifanikiwa kuzuia nyavu zao kutikiswa katika mechi zote nne. Akihojiwa meneja wa Leicester, Claudio Ranieri amesema msimu uliopita walifanya kitu muhimu na msimu huu wanafanya kitu muhimu pia. Ranieri aliendelea kudai kuwa kutinga hatua ya timu 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia yao ni mafanikio makubwa hivyo watajitahidi kufanya bidii ili kuhakikisha wanapata matokeo katika mechi zao zote mbili zilizobakia.
MASHABIKI WA UNITED WAJIFICHA CHOONI KUONA MECHI DHIDI YA ARSENAL.
MASHABIKI wawili wa Manchester United walijificha na kulala katika choo cha Uwanja wa Old Trafford kwa madhumuni ya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal uliochezwa Jumamosi iliyopita. Mashabiki hao walikuwa katika ziara ya kuutembelea uwanja huo lakini walifanikiwa kutoroka katika kundi ya watu waliokuwa wakitembezwa kuona maeneo mbalimbali ya uwanja huo. Hata hivyo, wawili hao walikamatwa Jumamosi asubuhi wakati wa ukaguzi wa usalama wa uwanja kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa polisi ambao waliamua kutowachukulia hatua. Taarifa ya United imedai kuwa hakukuwa na hatari yeyote kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo dhidi ya Arsenal.
Monday, November 21, 2016
NEYMAR, MESSI WATAJWA TUZO ZA BAO BORA LA MWAKA.
Mario Gaspar (ESP) - 13.11.2015, Spain v England, international friendly
Hlompho Kekana (RSA) - 26.03.2016, Cameroon v South Africa, Africa Cup of Nations qualifier
Marlone (BRA) - 21.04.2016, Corinthians v Cobresal, Copa Libertadores
Lionel Messi (ARG) - 21.06.2016, USA v Argentina, Copa America Centenario semi-final
Neymar (BRA) - 08.11.2015, Barcelona v Villarreal, La Liga (Spain)
Saul Niguez (ESP) - 27.04.2016, Atletico Madrid v Bayern Munich, Champions League
Hal Robson-Kanu (WAL) - 01.07.2016, Wales v Belgium, EURO 2016
Daniuska RodrÃguez (VEN) - 14.03.2016, Venezuela v Colombia, South American U-17 Women’s Football Championship
Simon Skrabb (FIN) - 31.10.2015, Gefle v Atvidaberg, Allsvenskan league, Sweden
Mohd Faiz Subri (MAS) - 16.02.2016, Penang v Pahang, Malaysia Super League
Hlompho Kekana (RSA) - 26.03.2016, Cameroon v South Africa, Africa Cup of Nations qualifier
Marlone (BRA) - 21.04.2016, Corinthians v Cobresal, Copa Libertadores
Lionel Messi (ARG) - 21.06.2016, USA v Argentina, Copa America Centenario semi-final
Neymar (BRA) - 08.11.2015, Barcelona v Villarreal, La Liga (Spain)
Saul Niguez (ESP) - 27.04.2016, Atletico Madrid v Bayern Munich, Champions League
Hal Robson-Kanu (WAL) - 01.07.2016, Wales v Belgium, EURO 2016
Daniuska RodrÃguez (VEN) - 14.03.2016, Venezuela v Colombia, South American U-17 Women’s Football Championship
Simon Skrabb (FIN) - 31.10.2015, Gefle v Atvidaberg, Allsvenskan league, Sweden
Mohd Faiz Subri (MAS) - 16.02.2016, Penang v Pahang, Malaysia Super League
HOENESS AUTAKA TENA URAIS BAYERN.
RAIS wa zamani wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesisitiza kuwa hawezi kukaa mbali na klabu hiyo wakati akijiandaa kuiwinda tena nafasi yake ya urais kwa mabingwa hao wa Bundesliga. Hoeness alilazimika kuachia ngazi mwaka 2014 wakati akitumikia adhabu ya kifungo jela kwa kosa la kukwepa kodi lakini bado ameendelea kupigiwa upatu wa kuingoza tena klabu hiyo. Nguli huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani alidai kuwa anafurahia kuungwa mkono na wafanyakazi wote w Bayern na mke wake katika hatua zake za kuitaka tena nafasi hiyo. Hoeness alidai kuwa aliiomba familia yake kugombea tena nafasi hiyo na wakamkubalia kwani wanafahamu furaha yake ni kuiongoza klabu hiyo anayoipenda.
YANGA YAMUANIKA LWANDAMINA.
HATIMAYE uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi ujio wa kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina toka Zambia anayekuja kurithi mikoba ya mholanzi Hans Van De Pluijm anayekuwa mkurugenzi wa benchi la Ufundi. Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Redio cha EFM, Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema kuwa ni kweli wameingia mkataba na George Lwandamina aliyekuwa akiifundisha Zesco United nchini Zambia na rasmi ataanza kuinoa timu hiyo mzunguko wa pili wa ligi kuu. Sanga mbali na kuweka wazi suala hilo ambalo lilikuwa ni gumzo kwa vyombo vya habari nchini, pia ametoa maelezo ya kina kwa mustakabali wa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm na kusema kuwa bado wataendelea kuwa nae kama mkurugenzi wa benchi la ufundi kwani ni mwalimu mzoefu na anaijua vyema Yanga hivyo ushauri wake na uzoefu utakuwa chachu ya mafanikio katika benchi letu la ufundi na klabu kiujumla. Hans Van Pluijm ameridhia nafasi hiyo baada ya uongozi wa klabu hiyo kukaa nae chini na kumwomba aendelee kubaki klabuni kwa nafasi hiyo adhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo kimbinu na kiufundi na mabadiliko hayo hayana maana kwamba kiwango cha kocha wa awali kilikuwa kibaya bali uongozi katika hatua ya kuiboresha klabu yake umeamua kuleta changamoto mpya ili kujiweka bora zaidi katika michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo.
AC MILAN WAMUWINDA WILSHERE.
KLABU ya AC Milan inadaiwa kuwa na matumaini ya kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere mwishoni mwa msimu huu. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza alipata nafasi ya kujiunga na timu hiyo kongwe nchini Italia majira ya kiangazi lakini aliamuakwenda kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth. Toka atue Bournemouth Wilshere amefanikiwa kucheza mechi nane za ligi na anadaiwa kuwa tayari ameshakubali kuwa mustabali wake wa baadae unaweza kuwa nje ya Arsenal. Wilshere mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara na kumfanya kufanikiwa kucheza mechi 105 pekee katika misimu tisa aliyocheza Arsenal. Milan wamepania kumsajili Wilshere kwa dili la moja kwa moja kipindi cha usajili wa kiangazi mwakani wakati ambao kiungo huyo atakuwa ameshamaliza mkataba wake.
CONTE AMMWAGIA MISIFA COSTA.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amemuhabalisha Diego Costa kuendelea kufanya anayofanya baada ya kuipeleka Chelsea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Bao pekee alilofunga Costa katika mchezo huo dhidi ya Middlesbrough uliofanyika katika Uwanja wa Riverside lilitosha kuipa Chelsea ushindi wake wa sita mfululizo katika ligi na kuzipita Liverpool na Manchester City. Nyota huyo kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 28, hilo linakuwa bao lake la 10 msimu huu. Akihojiwa Conte amesema Costa ni mmoja wa washambuliaji bora duniani na anadhani amewaonyesha kwa vitendo wale wote waliokuwa wakimkosoa na kuhoji uwezo wake.
ROMA, GALATASARAY WAMUWANIA DEBUCHY.
KLABU za AS Roma na Galatasaray zinadaiwa kumuwania beki wa Arsenal, Mathieu Debuchy ambaye anaonekana kutokuwa na nafasi katika klabu hiyo. Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, amecheza mechi mbili pekee za Ligi Kuu katika misimu miwili iliyopita katika kikosi cha Arsene Wenger, kufuatia kupelekwa kwa mkopo katika Bordeaux Januari mwaka huu. Hata hivyo, anaweza kupewa nafasi ya kurejea katika kikosi cha kwanza huku Roma na Galatasaray zote zikidaiwa kumuwania nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Debuchy alirejea kutoka katika majeruhi kwa kufunga bao katika mchezo wa kikosi cha wachezaji chini ya miaka 23 na anaweza kurejeshwa katika mipango ya Wenger kufuatia kuumia kwa Hector Bellerin.
GUARDIOLA AKIRI KUKOSEA KUMUACHA TOURE.
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amedai kuwa pengine alifanya makosa kumuacha Yaya Toure na yuko tayari kumrejesha kiungo huyo katika kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toure aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Guardiola katika ushindi wa mabao 2-1 iliyopata City dhidi ya Crystal Palace huku akifunga mabao yote mawili. Awali ilionekana kama maisha ya Toure Itihad yamefikia ukingoni kutokana na sintofahamu iliyojitokeza baina ya Guardiola na wakala wake Dimitri Seluk lakini baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast kuomba radhi mambo yanaonekana kwenda sawa. Akiulizwa kama Toure anaweza kuongezwa katika kikosi chake Januari, Guardiola alikubali na kudai inawezekana na kama wakifanikiwa kufuzu hatua ya timu 16 bora atakutana na jopo lake la kuamua.
SPURS YAMGEUKIA TENA SANDRO BAADA YA JANSSEN KUSHINDWA KUNG'AA.
KLABU ya Tottenham Hotspurs inatarajiwa kwa mara nyingine kutupa ndoano kumuwania mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Sandro katika usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Spurs walikuwa wameonyesha nia ya kumsajili wakati wa kiangazi lakini waliamua kumchukua Vincent Janssen badala yake huku Sandro mwenyewe akichagua kubakia Malaga ambako alisaini mkataba wa miaka mitatu. Hata hivyo, Spurs wameanza tena kumuwania nyota huyo kufuatia Janssen kushindwa kung’ara vyema katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Sandro mpaka sasa ameshafunga mabao matano katika mechi 10 alizoichezea Malaga toka kuanza kwa msimu huu.
NAPOLI KUMUWANIA ZOUMA JANUARI.
KLABU ya Napoli inadaiwa kuwa matumaini Chelsea wanaweza kuwaruhusu kumchukua kwa mkopo Kurt Zouma katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 bado anajiuguza baada ya kupata majeruhi mabaya ya goti katika mchezo wa Ligi Kuu waliokutana na Manchester United Februari mwaka huu. Zouma hajacheza mecho yeyote ya kimashindano chini ya meneja mpya Antonio Conte na tayari tumeshuhudia kina David Luiz, Gary Cahill na Cesar Azpilicueta wakionyesha kuelewana vyema katika safu ya ulinzi ya timu hiyo. Chelsea wanadaiwa kuwa wanaweza kumruhusu beki huyo kuondoka kwa muda mfupi Januari ili aweze kupata muda zaidi wa kucheza na Napoli wanataka kumsajili ili aweze kuziba nafasi ya Kalidou Koulibaly atakayekwenda kushiriki michuano ta Mataifa ya Afrika mapema mwakani.
Saturday, November 19, 2016
Friday, November 18, 2016
CONTE, HAZARD WATWAA TUZO ZA MWEZI.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte ameteuliwa kuwa meneja bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Octoba. Meneja huyo wa zamani wa Juventus ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuiongoza Chelsea kushinda mechi tano mwezi uliopita na kuwafanya kukwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi. Kwa upande mwingine Winga wa klabu hiyo Eden Hazard yeye alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kufunga mabao matatu na kusaidia lingine moja. Akihojiwa mara baada ya kupokea tuzo hiyo Hazard amesema watu walisema hapigi sana mashuti hivyo amejirekebisha kwa kujaribu kupiga mashuti na na kufunga wakati akiwa uwanjani.
SOUTHGATE KUFANYIWA USAILI JUMATATU.
CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kinatarajiwa kukutana na Gareth Southgate kwa ajili ya kufanywa usaili wa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza. Southgate alikamilisha mechi zake nne bila kufungwa akiinoa timu hiyo kwa muda baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce. Southgate anatarajiwa kukutana na jopo likalosimamiwa na mwenyekiti wa FA Gregg Clarke, Ofisa Mkuu Martin Glenn, Mkurugenzi wa Ufundi Dan Ashworth na wajumbe wengine wawili huru kwenye jopo hilo, Howard Wilkinson na Graeme Le Saux. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika huko St George Park huku uamuzi wa mwisho ukitarajiwa kutoka wakati wowote baada ya usaili huo.
SCHWEINSTEIGER ASISITIZA KUPIGANIA NAFASI YAKE OT.
KIUNGO wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger amesisitiza bado anajituma ili kupata nafasi katika kikosi cha timu hiyo pamoja na Jose Mourinho kumuondoa katika mipango yake. Nahodha huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani aliambiwa mapema Agosti kuwa hatakuwa katika mipango ya meneja huyo na kulazimishwa kufanya mwenyewe kwa kipindi kirefu. Mourinho alimuita tena kiungo huyo kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza mwishoni mwa mwezi uliopita lakini bado anategemewa kuondoka klabuni hapo Januari huku klabu ya Chicago Fire ya Marekani ikitajwa kumuwania. Akihojiwa Shweinsteiger amesema kuwa malengo yake bado ni kucheza United na ataendelea kujituma kadri awezavyo mazoezini kwa matumaini ya kupewa tena nafasi.
GRIEZMANN HAENDI KOKOTE - ATLETICO.
RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amedai kuwa hakuna nafasi kwa mshambuliaji wao Antoine Griezmann kujiunga na Real Madrid au Manchester United. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa jina lake limehusishwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya katika miezi ya karibuni kufuatia kuimarika kwa kiwango chake. Tetesi za kuhamia Old Trafford nazo zilizuka huku Griezmann akikiri kuwa angefurahi kucheza sambamba na Mfaransa mwezake Paul Pogba huku Madrid nao wakitajwa katika mbio za kumuwania. Hata hivyo, tetesi hizo zimezimwa na Cerezo akidai kuwa haamini kama mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ataweza kwenda Madrid au klabu nyingine yeyote ile. Cerezo aliendelea kudai kuwa wamekuwa na uhusiano mzuri na Madrid na wanaheshimiana kama majirani. Atletico wanatarajiwa kuikaribisha Madrid katika mchezo wa La Liga kesho, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana toka Atletico walipofungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa matuta Mei mwaka huu kule San Siro.
KOSCIELNY KUONGEZA MKATABA ARSENAL.
BEKI wa Arsenal, Laurent Koscielny anadaiwa kukaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na Arsenal mwaka 2010 akitokea Lorient na toka kipindi hicho ameimarika na kuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo. Arsenal inataka kumuongeza mkataba wa muda mrefu na taarifa zinadai kuwa tayari wameshafikia makubaliano ya kumuongeza mkataba mpaka mwaka 2020. Mkataba wa sasa wa beki huyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na mkataba wake mpya unatarajiwa kutangazwa kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain Jumatano ijayo.
GUARDIOLA AMUWANIA BEKI WA BENFICA.
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kuimarisha zaidi safu yake ya ulinzi kwa kumuania beki wa kushoto wa Benfica Alex Grimaldo. Lakini meneja huyo anaweza kushindwa kunasa saini ya beki huyo kufuatia taarifa kuwa Benfica wanaweza kutaka paundi milioni 38.5. Guardiola amekuwa akimfahamu Grimilo kwa kipindi kirefu toka alipokuwa Barcelona. Hata hivyo, uhusiano wao huo haudhaniwi kama unaweza kuwa ushawishi wa kumng’oa nyota huyo nchini Ureno.
AC MILAN YAMLENGA STURRIDGE JANUARI.
KLABU ya AC Milan, inadaiwa kujipanga kumuwania mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge Januari mwakani. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akishindwa kupata nafasi katika kikosi cha meneja Jurgen Klopp. Lakini uwezo mkubwa alionao mchezaji huyo unadaiwa kumvutia meneja wa Milan Vincenzo Montella ambaye anaweza kutoa ofa ya paundi milioni 30 ili kumnasa. Hata hivyo, uhamisho huo unadaiwa kuwa utategemea kuondoka kwa Carlos Bacca.
FIFA KUZICHUKULIA HATUA UINGEREZA NA SCOTLAND.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limefungua mashitaka ya kinidhamu dhidi ya Uingereza na Scotland kwa kuvaa beji zenye kiua katika mechi yao ya kufuzu Kombe la Dunia ambayo iliangukia katika siku ya kuwakumbuka mashujaa wao. Wachezaji wa timu zote mbili walivaa beji nyeusi zenye kiua katika mchezo huo ambao Uingereza ilishinda mabao 3-0 katika Uwanja wa Wembley Ijumaa iliyopita. Sheria za shirikisho hilo zinakataza fulana za wachezaji kuwa na ujumbe wa kisiasa, kidini, picha au kauli zozote binafsi zisizohusiana na masuala ya soka. Wazo la wachezaji kuvaa beji yenye viua lilikuja kabla mataifa hayo mawili hayakutana Novemba 11, ambayo ndio siku ya kuwakumbuka mashujaa wao waliopoteza maisha katika vita mbalimbali.
Thursday, November 17, 2016
KOCHA AIPONZA KLABU HUKO BRAZIL.
KLABU ya Gremio ya Brazil imeadhibiwa baada ya binti wa kocha Renato Gaucho kuingia uwanjani baada ya timu hiyo kushinda mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Ligi nchini humo. Binti huyo Carolina Portaluppi mwenye umri wa miaka 22, alikwenda kukaa katika benchi la ufundi mwishoni mwa mchezo huo kabla ya kuingia uwanjani kuungana na wachezaji kushangilia. Mahakama ya Michezo nchini humo imeambia klabu hiyo kuwa watacheza mechi yao ya fainali ya mkondo wa pili ugenini kama adhabu ya tukio hilo. Katika hukumu yake mahakama hiyo ilidai kuwa hawahoji mapenzi ya baba kwa binti yake lakini tukio lililofanyika haliruhusiwi ndio maana imechukuliwa hatua hiyo. Klabu hiyo pia imelimwa faini ya dola 6,995, wakati gaucho ameonywa kuwa anaweza kuchukuliwa hatua zaidi. Mara baada ya maamuzi hayo, mashabiki wenye hasira walianza kumshambuliaji binti huyo katika mitandao ya kijamii huku wengine wakimtetea. Baada ya kuichapa Cruzeiro kwa jumla ya mabao 2-0 katika mechi mbili za nusu fainali walizokutana, Gremio sasa watachuana na Atletico Maneiro katika fainali ya mikondo miwili baadae mwezi huu.
BOLIVIA WAKATA RUFANI KUPINGA KUNYANG'ANYWA ALAMA.
CHAMA cha Soka cha Bolivia-FBF kimekata rufani kupinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwakata alama katika mechi zao za kufuzu Kombe la Dunia kwa kosa la kumchezesha beki mzaliwa wa Paraguay Nelson Cabrera. Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Peru Septemba mosi na sare ya bila kufungana na Chile siku tano baadaye ziliondolewa katika rekodi na badala yae wapinzani wao hao wote walipewa ushindi wa mabao 3-0. FBF pia ililimwa faini ya dola 12,250 kwa kosa hilo. Cabrera alikuwa akicheza katika klabu ya Bolivar inayoshiriki Ligi Kuu ya Bilivia toka mwaka 2012 na pia aliitwa katika timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Marekani Mei mwaka 2016 kabla ya kuiwakilisha katika michuano ya Copa Amerika Juni. Hata hivyo, Cabrera anadaiwa aliwahi kuiwakilisha pia timu ya taifa ya Paraguay mwaka 2007 hivyo ushiriki wake katika mechi hizo za kufuzu Kombe la Dunia iligundulika kuwa sio halali ndio maana wakachukuliwa hatu hiyo. Baada ya kuthibitisha kukata rufani, FBF wamedai kuwa kamwe FIFA haijawahi kujifanyia uchunguzi yenyewe bila kupokea malalamiko kutoka upande wowote.
BELLERINI KUIKOSA UNITED.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Hector Bellerin anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne kufuatia majeruhi aliyopata katika mchezo wa dhidi ya Tottenham Hotspurs. Beki huyo wa kimataifa wa Hispania, alipata majeruhi hayo ya goti katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa. Mapema leo Wenger aliwaambia wanahabari kuwa Bellerin anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki nne baada ya kuumia katika sekunde 10 za mwisho kwenye mchezo huo. Taarifa hizo sasa zitamfanya Wenger kufanya mabadiliko katika safu yake ya ulinzi katika safari yao ya Old Trafford kupambana na Manchester United Jumamosi hii. Mbali na kukosa mechi hiyo ya Old Trafford, Bellerini pia atakosa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain na Basel, mechi za ligi dhidi ya Bournemouth, West Ham United, Stoke City na Everton na robo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Southampton.
MOURINHO AMTAKA DEMBELE.
MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho anadaiwa kutaka kumleta nyota wa Celtic Moussa Dembele kwani anadhani anaweza kuwa Didier Drogba ajaye. Taarifa zinadai kuwa Mourinho amekuwa akimfuatilia chipukizi huyo mara tatu msimu uliopita kabla hajaondoka Fulham na kwenda Celtic. Hata hivyo, Celtic wanadaiwa kuwa hawataweza kumuachia Dembele, ambaye amefunga mabao matatu katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, katika kipindi cha usajili wa Januari. Manchester City, Arsenal, Chelsea na Bayern Munich zote pia zinadaiwa kumfuatilia nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, wakati Tottenham Hotspurs walishindwa kumsajili Januari mwaka huu.
FA YADAI HAITAFANYA HARAKA KUCHAGUA KOCHA MPYA.
OFISA mkuu wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Martin Glenn amesema hawatafanya uamuzi wa haraka katika kuchagua kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Gareth Southgate kupewa nafasi kubwa. Southgate mwenye umri wa miaka 46 aliteuliwa kuwa meneja wa muda Julai kwa ajili ya mechi nne za mwisho za Uingereza kwa mwaka huu na kufanikiwa kushinda mechi mbili na kutoa sare zingine mbili. Toka alipopewa mikoba hiyo baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce kocha huyo ameonyesha ukaribu mkubwa na wachezaji huku mwenyewe akisema ameonyesha thamani baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hispania Jumanne. Pamoja na hayo, FA wamedai watachukua muda kabla ya kutoa maamuzi ya kocha gani atapewa mikoba ya kuiongoza timu hiyo. Glenn amesema anafahamu kuwa Southgate anapewa nafasi kubwa lakini hawataweza kufanya maamuzi ya haraka kutokana na uzoefu walipata huko nyuma.
Wednesday, November 16, 2016
BARCELONA WAPATA MDHAMINI MPYA WA JEZI ZAO.
KLABU ya Barcelona inatarajiwa kuwa na jina jipya mbele ya fulana zao kuanzia msimu wa mwaka 2017-2018 baada ya kupata wadhamini wapya kampuni ya Rakuten ya Japan. Kampuni hiyo imesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo wenye thamani ya euro milioni 220. Kampuni hiyo kubwa ya biashara kwa njia ya mtandao nchini Japan ilizinduliwa mwaka 1997 na kuanza kujitanua nje ya nchi hiyo kuanzia mwaka 2005 na sasa wanataka kuendelea kujitanua zaidi kwa kujitangaza kupitia klabu hiyo yenye jina kubwa duniani. Rakuten watachukua nafasi ya Qatar Airways waliokuwa wadhamini wakubwa wa Barcelona toka mwaka 2013. Qatar Airways wao waliongeza mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa msimu wa 2015-2016.
TIMUATIMUA YA MAKOCHA WA AFRIKA YAENDELEA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Congo, Pierre Lechantre ametimuliwa kibarua chake na kumfanya kuwa kocha wan chi kutimuliwa toka kuanza kwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia hatua ya makundi kwa upande wa Afrika mwezi uliopita. Congo walitandikwa na Uganda bao 1-0 Jumamosi iliyopita na kufuatia kupoteza pia mchezo wao wa kwanza dhidi ya Misri Octoba umewafanya kuburuza mkia wa kundi E wakiwa hawana alama yeyote. Nchi hiyo pia imeshindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika Januari mwakani nchini Gabon. Uamuzi wa kutimuliwa umetangazwa baada ya Mfaransa kukutana na maofisa wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo jana. Lechantre amekuwa akiinoa Congo kwa karibu mwaka mmoja lakini amefanikiwa kupata ushindi mara moja katika mechi saba. Makocha wan chi nyingine waliotimuliwa baada ya timu zao kufanya vibaya katika mechi zao ufunguzi za makundi zilizofanyika Octoba ni pamoja na kocha wa Algeria, Gabon na Libya. Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Ephraim Mashaba yeye amesimamishwa pamoja na ushindi wa timu yake dhidi ya Senegal kwa tuhumiwa kuwatukana maofisa wa shirikisho la soka la nchi hiyo.
SOUTHGATE ADAI YUKO TAYARI KUINOA UINGEREZA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema ameonyesha anaweza kuhimili vishindo vya kuiongoza timu hiyo katika mechi mechi kubwa zenye shinikizo. Southgate mwenye umri wa miaka 46 anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Sam Allardyce baada ya kumaliza mkataba wake wa kuisimamia nchi hiyo katika mechi nne bila kufungwa baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hispania. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Southagate amesema anadhani katika mechi nne alizosimamia ameonyesha kuwa anaweza mikikimikiki ya kukiongoza kikosi cha nchi hiyo. Southagate alipewa mikoba ya muda akitokea katika kikosi cha nchi hiyo cha vijana chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuondoka Allardyce aliyedumu kwa siku 67 pekee. Katika mechi zake alizosimamia kocha huyo alishinda mchezo wake wa kwanza ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malta kabla ya kuja kupata sare ya bila kufungana na Slovenia na baadae kuwaadabisha mahasimu wao wa siku nyingi Scotland kw mabao 3-0 wiki iliyopita.
Subscribe to:
Posts (Atom)