Wednesday, November 30, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: ZANZIBAR HEROES KUTUPA KARATA YAO YA MWISHO.
TIMU ya taifa ya Zanzibar-Zanzibar Heroes leo inatarajia kutupa karata yake ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji itavaana na Somalia katika mchezo wa kundi B utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Zanzibar ambayo katika mchezo wao wa kwanza ilikubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Uganda na kutoa sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa pili dhidi Burundi itakuwa ikiomba Uganda waifunge Burundi ili waweze kupata nafasi ya kusonga mbele. Timu hiyo ambayo mbali na kuomba ushindi kwa timu ya Uganda lakini pia wao itabidi wawafunge Somalia mabao yasiyopungua manne. Matokeo yakiwa hivyo Zanzibar itakuwa imefungana pointi na Burundi wote wakiwa na alama nne hivyo Zanzibar kusonga mbele kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga na kuiacha Burundi ikirejea nyumbani.
Monday, November 28, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: KILI STARS KUTUPA KARATA NYINGINE LEO.
TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjro Stars leo inatarajiwa kutupa karata yake nyingine pale itakapojitupa uwanjani kupambana na timu ya Djibouti katika mchezo wa Kombe la Challenge utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kilimanjaro ambao katika mchezo wao wa awali ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rwanda- Amavubi inabidi kushinda`mchezo wao wa leo ili kurudisha imani kwa mashabiki na kuweka matumaini hai ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Mabingwa hao mara tatu wa michuano hiyo leo huenda wakamkosa mshambuliaji wao hatari Mbwana Samata anaesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu baada ya kuumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda. Katika mchezo mwingine utakaochezwa mapema mchana huu timu ya Rwanda itapambana na Zimbabwe huku timu zote zikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda michezo yao ya kwanza.
PODOLSKI APATA AJALI.
MCHEZAJI wa kimataifa wa Ujerumani Lukas Podolski amepata ajali gari akiwa niani kuelekea mazoezini. Mchezaji huyo ambaye anakaribia kutimiza mchezo wa 100 toka aanze kuitumikia timu ya taifa aligongana na gari lingine lililokuwa na watu watatu wa familia moja. Watu wawili kati ya ya watatu waliokuwemo katika gari hilo walipelekwa hospitali kwa uchunguzi baada ya kupata majeraha madogo madogo. Podolski mwenye miaka 26 ambaye anakipiga katika klabu ya Cologne iliyopo katika ligi ya Bundesliga hakupata majeraha yoyote katika ajali hiyo ingawa chanzo cha ajali hakijajulikana mpaka sasa.
WAZIRI MKUU BULGARIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MCHEZAJI BORA.
WAZIRI Mkuu wa Bulgaria Boiko Borisov yuko mbioni kuitwa katika orodha ya mchezaji bora wa mwaka wan chi hiyo baada ya mshambuliaji wa Manchester United kuchoka kushinda tuzo hiyo mara kwa mara. Borisov akipata nafasi huwa anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya daraja la tatu ya Vitosha Bistritsa ambayo kwa jina la utani inatambulika kama Tigers na mpaka sasa anaongoza kwa kura 2000 zilizopigwa na mashabiki kumuingiza katika orodha hiyo. Akihojiwa Borisov mwenye miaka 52 amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumwambia kwamba yeye ni mchezaji mbovu na kuisifia timu yake ya Tigers kuwa ni timu bora. Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo kuruhusu mashabiki kushiriki katika mchakato huo ambapo watateua orodha ya wachezaji 20 watakaoshindanishwa wakati kura za mwisho zitapigwa na waandishi wa habari. Waziri Mkuu huyo mbali ya kuwa mshambuliaji hodari pia ana mkanda mweusi katika sanaa ya mapigano ya karate na mchezaji mzuri wa mchezo wa tenisi.
"BARCELONA BADO INA NAFASI YA KUNYAKUWA LA LIGI." CRUYFF.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Barcelona Johan Cruyff amewashangaa watu wanaodai kuwa timu hiyo haiwezi kutetea ubingwa wake wa La Liga msimu huu. Wakati akihojiwa na waandishi kabla ya mchezo kati ya timu ya hiyo na Esperance ya Tunisia Cruyff amesema kuna mataji manne msimu huu na Barcelona hawajalipoteza lolote mpaka sasa hivyo haoni sababu ya watu kuibeza timu hiyo kwasasa. Barcelona imepotza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa Getafe baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 Jumamosi iliyopita hivyo kuwa nyuma katika nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya alama sita nyuma ya vinara wanaoongoza ligi hiyo Real Madrid. Mchezaji huyo wa zamani ambaye kwasasa ana umri wa miaka 64 amesema kuwa watu wengi inaonekana hawajui ubora wa timu ya Barcelona na sio kwamba mambo yanakwenda vibaya kwasababu wamefungwa huo mchezo mmoja.
RAMBIRAMBI AZIDI KUMIMINIKA KUFUATIA KIFO CHA SPEED.
SALAMU za rambirambi zimeendelea kuminika kufuatia kifo cha aliyekuwa meneja wa timu ya Taifa ya Wales ambaye alikutwa amekufa akiwa nyumbani kwake. Kiungo huyo wa zamani mwenye miaka 42 ameichezea Wales michezo 85 na amekuwa akikinoa kikosi cha nchi hiyo katika michezo 10. Mojawapo ya watu walioguswa na kifo cha Speed ni pamoja na aliyekuwa meneja wa timu hiyo Mark Hughes, nahodha wa kikosi hicho Bobby Gould, Michael Owen, Waziri wa Michezo wan chi hiyo pamoja na rafiki wa karibu wa meneja huyo Graig Bellamy. Polisi walithibitisha kuwa mwili uligundulika nyumbani kwake katika mji wa Huntington ambapo alikutwa amejinyonga huku poilisi wakisema hakuna mtu yoyote anayehisiwa kufanya tukio hilo. Chama cha Soka cha nchi hiyo kimeelezea kusikitishwa na kifo cha mchezaji huyo ambapo katika taarifa yake kimesema huenda mchezaji mashuhuri wa zamani alijiua mwenyewe.
Sunday, November 27, 2011
MANCINI AWACHARUKIA WACHEZAJI WA LIVERPOOL.
MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amedai kuwa wachezaji wa Liverpool wanapaswa walaumiwe kufuatia kutolewa kwa mshambuliaji wake Mario Balotelli wakati timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Anfield. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Italia alitolewa nje baada ya kupata kadi mbili za njano ikiwa ni dakika 18 tu toka aingie akitokea benchi. Mancini amesema hakubaliani na kadi ya pili aliyopewa mchezaji huyo kwani mwamuzi hakutaka kumpa kadi hiyo hadi pale wachezaji wa Liverpool walivyomzonga mwamuzi huyo kumlalamikia. Balotelli alipewa kadi ya kwanza ya njano kwa kosa la kumvuta mchezaji wa Liverpool Glen Johnson wakati kadi ya pili ya njano alipewa kufuatiwa kumshika Martin Skrtel kwa mikono.
CECAFA CHALLENGE CUP: HARAMBEE STARS KUIKWAA MALAWI.
KOCHA wa timu ya taifa ya Kenya-Harambee stars Francis Kamanzi amesema kikosi kitakuwa kikishambulia zaidi wakati kitakapocheza na Malawi katika michuano ya Kombe la Challenge utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo mchana. Kikosi hicho kiliwasili jana mchana tayari kwa mashindano hayo huku kikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 7-0 katika mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kocha huyo amesema Malawi ni timu nzuri hivyo hawawezi kuwadharau lakini akatamba kuwa kikosi chake imara huku akisifu washambuliaji wake wenye kasi kuwa watasaidia kuibuka na ushindi katika mchezo huo. Harambee Stars imepangwa katika kundi C wakiwa na timu za Sudan, Malawi na Ethiopia katika michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA.
Thursday, November 24, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: ZANZIBAR KUANZA NA UGANDA LEO.
MICHUANO ya kombe la Challenge inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika michezo ya leo ya kundi B Zanzibar itakuwa kibaruani kupambana na Uganda mchezo ambao utachezwa jioni wakati katika mchezo wa kwanza Burundi itapepetana na Somalia.
Mara ya mwisho Uganda na Zanzibar zilikutana katika robo fainali ya michuano hiyo mwaka jana na Uganda ilifanikiwa kuitoa Zanzibar kwa penalti 5-3, baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida. Akihojiwa kocha wa Zanzibar Hemed Morocco amesema mchezo huo utakuwa ni mgumu kwakuwa Uganda ni timu nzuri lakini akaahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi katika mchezo huo.
Mara ya mwisho Uganda na Zanzibar zilikutana katika robo fainali ya michuano hiyo mwaka jana na Uganda ilifanikiwa kuitoa Zanzibar kwa penalti 5-3, baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida. Akihojiwa kocha wa Zanzibar Hemed Morocco amesema mchezo huo utakuwa ni mgumu kwakuwa Uganda ni timu nzuri lakini akaahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi katika mchezo huo.
BESIKTAS YAFUNGIWA MECHI MOJA.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki-PFDK limeifungia klabu ya Besiktas kucheza mchezo wao mmoja wa nyumbani bila mashabiki kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wao na Galatasaray. Klabu hiyo pia imepigwa faini ya euro 94,000 kwa ajili la tukio hilo lililotokea wiki iliyopita katika uwanja wake uitwao Inonu. Mchezaji wa Galatasayar Emmanuel Eboue ndiye alikuwa mhanga katika tukio hilo ambapo mashabiki hao wenye hasira walimpiga na vitu mbalimbali ikiwemo chupa za maji na viberiti vya gesi wakati wa mchezo huo. Wakati huohuo mchezaji wa kimataifa wa Brazil Felipe Melo amefungiwa kucheza mchezo mmoja kwa kosa la kugombana na mashabiki hao, Besiktas inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu nchini humo wakati Galatasayar wao wanashika nafasi ya tatu.
BRAZIL YAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UBAGUZI.
Waandaaji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil wamezindua kampeni ya kupinga suala la ubaguzi wa rangi michezoni Alhamisi hii. Shirikisho la Soka la Brazil-CBF wametaja mzunguko wa mechi za ligi kuu ya nchi hiyo zinazochezwa wiki hii kuwa ni mzunguko wa kupinga ubaguzi. Katika taarifa yake CBF wamesema suala la ubaguzi haliwezi kutatuliwa kwa kushikana mikono wakipinga na kauli ya kushtusha aliyoitoa Rais wa FIFA Sepp Blatter aliyesema masuala ya ubaguzi michezoni yanaweza kumalizwa na wachezaji wenyewe kwa kushikana mikono baada ya mchezo. Kauli ilileta utata na kukemewa na wadau wengi wa mchezo huo mpaka ikamlazimu Blatter kuomba radhi kwa kauli yake hiyo.
MARADONA ASHUKURU WALIOMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE.
Mchezaji nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona ametoa shukrani kwa wote waliomtumia ujumbe mfupi wa kumpa pole kufuatia kifo cha mama yake Dalma Franco. Mchezaji huyo ambaye alikiongoza kikosi Argentina kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1986 amesema kuwa anawashukuru wote pamoja na wale waliokaa kimya dakika moja kutoa heshima zao kwa mama huyo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Argentina. Maradona ambaye ana miaka 51 amesema pia ameguswa na ujumbe aliotumiwa na Rais wan chi hiyo Cristina Kirchner pamoja na majirani wa mji Villa Fiorito ambao ndio nyumbani kwa mchezaji huyo. Mchezaji huyo ambaye anaifundisha klabu ya Al-Wasl ya Falme za Kiarabu aliondoka huko Jumapili iliyopita kuja kumuuguza mama yake lakini akiwa njiani alijulishwa kuwa mama yake huyo alikuwa amefariki dunia. Mojawapo ya watu wengine maarufu waliotuma slamu zao rambirambi kwa mchezaji huyo ni pamoja na muigizaji Ricardo Darin, bingwa wa zamani wa michuano ya tenisi ya wazi ya Marekani mwaka 2009 Juan Martin Del Porto, mcheza soka Martin Palermo pamoja na nyota wa Barcelona Lionel Messi.
MILAN YAANZA MAZUNGUMZO NA TEVEZ.
KLABU ya AC Milan imeanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili. Tevez amekuwa katika misukosuko na City toka mwanzoni mwa msimu ambapo alitaka kuondoka na wiki chache zilizopita alipigwa faini na klabu hiyo kwa kukataa kupasha misuli moto wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwezi uliopita. Mchezaji huyo ameichezea klabu hiyo mara chache msimu huu akiwa na Edin Dzeko, Mario Balotelli, Sergio Aguero na David Silva wakiunda safu ya ushambuliaji. Milan wako sokoni wakitafuta mshambuliaji mbadala baada ya Antonio Cassano kufanyiwa upasuaji wa moyo baada ya kuugua ghafla wakati wa mchezo dhidi Roma ambao walishinda mabao 3-2, mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja msimu wote huu.
TENGA ATETEA KITI CHAKE CECAFA.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Tenga amechaguliwa leo (Novemba 24 mwaka huu) bila kupingwa baada ya mpinzani wake Fadoul Hussein wa Djibouti kutotokea kwenye uchaguzi. Kutokana na hali hiyo, mjumbe kutoka Uganda alitoa hoja ya Tenga kupitishwa bila kupingwa, hoja ambayo iliungwa mkono na Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan, Zanzibar, Ethiopia, Burundi na Eritrea. Jumla ya nchi wanachama zilizopiga kura katika uchaguzi uliofanyika hoteli ya New Africa ni kumi na moja, na kila moja ilikuwa na kura moja tu. Kwa upande wa nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji kulikuwa na wagombea wanane. Waliopita katika raundi ya kwanza na kura zao kwenye mabano ni Abdiqani Saeed Arab wa Somalia (8),Tariq Atta Salih wa Sudan (8) na Raoul Gisanura wa Rwanda (8). Wengine katika raundi ya kwanza na kura walizopata kwenye mabano ni Sahilu Wolde wa Ethiopia (4), Justus Mugisha wa Uganda (4), Tesfaye Gebreyesus wa Eritrea (4), Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar (2) na
Abubakar Nkejimana wa Burundi (3). Mjumbe aliyefanikiwa kushinda katika raundi ya pili na kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ni Wolde wa Ethiopia aliyepata kura tano dhidi ya nne za Mugisha na mbili za Gebreyesus. Mwenyekiti anakaa madarakani kwa miaka minne wakati wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanachaguliwa kila baada ya miaka miwili.
Abubakar Nkejimana wa Burundi (3). Mjumbe aliyefanikiwa kushinda katika raundi ya pili na kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ni Wolde wa Ethiopia aliyepata kura tano dhidi ya nne za Mugisha na mbili za Gebreyesus. Mwenyekiti anakaa madarakani kwa miaka minne wakati wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanachaguliwa kila baada ya miaka miwili.
MKWASA ATAJA KIKOSI CHA MWISHO CHA KILIMANJARO STARS.
Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza kesho. Wachezaji waliobaki kati ya 28 waliokuwa wameitwa awali ni Juma Kaseja (Simba), Shabani Kado (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam) na Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Nurdin Bakari (Yanga), Haruna Moshi (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Wengine ni Said Maulid (Angola), Musa Mgosi (DC Motema Pembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC), Mrisho Ngassa (Azam), Ramadhan Chombo (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Rashid Yusuf (Coastal Union). Kilimanjaro Stars itacheza mechi yake ya kwanza Novembe 26 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
KENYA KUANDAA CHALLENGE 2012.
Kenya inatarajiwa kuandaa michuano ya Kombe la Challenge ya Baraza la Vyama vya Michezo la nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA itakayofanyika mwaka 2012. Hatua ya kuiteua Kenya kuandaa michuano hiyo mwakani ilifikiwa Alhamisi hii katika mkutano wa uchaguzi wa baraza hilo uliofanyika Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Sam Nyamweya alielezea kuteuliwa huko kuandaa michuano hiyo kama habari njema na kulishukuru baraza hilo kwa kuwaamini kuwa wenyeji. Nyamweya amesema kazi kubwa inabidi ianze sasa kwakuwa wanataka mji wa Kisumu uwe mmoja wapo utakaokuwa wenyeji wa michuano hiyo na mapema watakaporudi wataitaarifu manispaa ya mji huo kuanza maandalizi.
CECAFA CHALLENGE CUP: ZIMBABWE YACHUKUA NAFASI YA NAMIBIA.
Nicholaus Musonye, Katibu Mkuu CECAFA |
Wednesday, November 23, 2011
TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA.
TANZANIA imeendelea kuporomoka katika viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kushuka nafasi tatu. Awali Tanzania iliporomoka hadi nafasi ya 131 lakini bado imeonekana kushuka zaidi katika viwango hivyo hadi nafasi ya 136 katika viwango vilivyotolewa leo. Kwa upande wan chi zingine za Afrika kuna mabadiliko katika timu zinazoshika nafasi tano za juu kwa ubora Afrika ambapo Ghana na Algeria zimepanda nafasi mbili 29 na 31 huku Misri wakiporomoka hadi nafasi ya 31. Hispania bado inaongoza katika orodha hiyo pamoja na kupoteza mchezo wao na Uingereza wakifuatiwa na Uholanzi, Ujerumani, Uruguay, Uingereza, Brazil, Ureno, Croatia, Italia na Argentina kukamilisha orodha ya timu 10 bora katika viwango hivyo.
Tuesday, November 22, 2011
BALLACK KUTIMIZA MECHI WA 100 KATIKA MICHUANO YA ULAYA.
NAHODHA wa Bayer Leverkusen Michael Ballack anatarajia kutimiza mechi yake ya 100 katika mashindano ya vilabu Ulaya wakati timu ya hiyo itapopambana na klabu yake ya zamani ya Chelsea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano hii. Chelsea inaongoza kwa alama 2 zaidi ya Leverrkusen katika kundi E na Ballack anategemea mchezo mgumu watakapokutana haswa baada ya timu hiyo kufungwa na Liverpool katika mchezo wa ligi. Kiungo huyo amesema Chelsea wanajua umuhimu wa mchezo leo hivyo kufanya timu hiyo kuwa hatari siku ya leo lakini wanaweza kuwafunga kwakuwa wanacheza wakiwa nyumbani na kila mtu anusubiria mchezo huo. Ballack alijiunga na Leverkusen mwaka 2010 kwa mara ya pili baada ya kuitumikia Chelsea kwa miaka minne na hivi sasa amerudi katika kiwango chake.
BIN HAMMAM AKATA RUFANI CAS.
MOHAMED bin Hammam amekata rufani katika Mahakama ya Juu ya Kimichezo-CAS kubadilishiwa adhabu aliyopewa ya kufungiwa maisha na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia tuhuma za kununua wajumbe wa kumpigia kura wakati wa uchaguzi. Ripoti kutoka mahakama hiyo imesema katika taarifa kuwa imepokea rufani ya bin Hammam lakini bado haijapangiwa tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo. Bin Hammam atahitaji hukumu hiyo ifikapo mwezi Mei mwakani wakati Shirikisho la Soka barani Asia litakuwa bado limefungwa kisheria kuiziba nafasi yake kwa kuteua kiongozi mpya wa shirikisho hilo. FIFA ilimfungia bin Hammam mwezi Julai mwaka huu baada ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo kumkuta na hatia ya kuwanunua viongozi wa vyama vya soka vya Caribbean kumpigia kura wakati wa uchaguzi ambao alikuwa akipambana na Rais wa FIFA Sepp Blatter.
MWAMUZI ALIYETAKA KUJIUA APATA NAFUU.
MWAMUZI ambaye alitaka kujiua masaa machache kabla ya kwenda kuchezesha mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani-Bundesliga mwishoni mwa wiki iliyopita ameruhusiwa kutoka hospitali. Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema katika tarifa yake Jumatatu kuwa mwamuzi huyo anayeitwa Babak Rafati ambaye ana umri wa miaka 41 hali yake inaendelea vizuri na anaendelea na matibabu. Rafati alikutwa alikutwa akitokwa na damu katika chumba cha hoteli alichofikia kabla ya mchezo wa Bundesliga kati ya Cologne na Mainz ambao alitakiwa kuuchezesha na sasa mchezo huo umeahirishwa mpaka Desemba 13 mwaka huu. Shirikisho hilo limesema kwasasa Rafati anahitaji amani na utulivu ambapo atahitaji muda na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu alichopitia.
ETO'O, ENOH WAITWA KAMATI YA NIDHAMU.
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Cameroon-Fecafoot imewaita wachezaji Samuel Eto’o na Eyong Enoh kwasababu ya kuchochea mgomo wiki iliyopita. Sakati limeibika baada ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon kugoma kwenda Algeria kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu hiyo kutokana na kutolipwa marupurupu yao katika michezo miwili iliyopita waliyocheza na Morocco pamoja na Sudan. Wachezaji hao walitarajiwa kufikishwa mbele ya kamati hiyo jana, lakini waliomba shauri hilo liahirishwe mpaka hapo maafisa wa Fecafoot nao watakapoitwa na kamati hiyo. Mbali na kina Eto’o pia Benoit Assou-Ekotto ambaye ni beki wa Tottenham Hotspurs nae ameitwa na kamati hiyo kwa kosa la kutojiunga na kikosi hicho katika mchezo dhidi ya Morocco pamoja na mechi waliyosusia ya Algeria.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN, UNITED, INTER KIBARUANI LEO.
MABINGWA wa zamani wa Ulaya timu za Bayern Munich, Manchester United na Inter Milan zitajitupa uwanjani kutafuta nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika michezo yao itakayochezwa Jumanne hii. Bayern wenyewe watahitaji suluhu dhidi ya timu ya Villarreal watakayocheza nayo ambayo imepoteza michezo yake yote katika kundi A na kuingia hatua hiyo ya mtoano wakati United itahitaji ushindi dhidi ya Benfica ili kujihakikishia nafasi hiyo. Inter nao watahitaji suluhu katika mchezo wao wa leo dhidi ya Trabzonspor ili kujihakikishia nafasi ya kujiunga na majirani zao AC Milan ambao tayari imeshasonga mbele katika hatua ya makundi wakati mabingwa mara tisa wa michuano hiyo Real Madrid itabidi ishinde mchezo wao wa kundi D dhidi ya Dinamo Zagreb ili kuhakikisha wanamaliza wakiwa wanaongoza kundi hilo. Michezo mingine itayochezwa leo ni pamoja na Manchester City ambao itahitaji ushindi dhidi ya Napoli ili kusonga mbele, SCKA Moscow wataikaribisha Lille wakati Otelul Galati itacheza na Basle.
Monday, November 21, 2011
BECKHAM AISAIDIA GALAXY KUNYAKUWA KOMBE LA MLS.
TIMU ya Los Angeles Galaxy imefanikiwa kunyakuwa kombe la Ligi ya soka ya Marekani-MLS kwa kuifunga Houston Dynamo kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Jumapili usiku. Alikuwa ni nahodha wa Galax Landon Donovan ambaye alishinda bao hilo pekee dakika ya 72 akimalizia pasi murua ya Robbie Keane na kuihakikishia timu hiyo ubingwa wake wa kwanza toka waliposhinda mwaka 2005. Galaxy walionyesha dalili za ushindi tokea mwanzoni mwa mchezo baada kuonyesha kandanda safi karibu kipindi chote mchezo huo. Wakiwa na David Beckham ambaye alitua katika klabu hiyo mwaka 2007, Robbie Keane kutoka Ireland na Donovan katika kikosi hicho walikisaidia vyema kikosi hicho kuhakikisha kinashinda mchezo huo.
REDKNAPP FITI KUIVAA VILLA.
MENEJA wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema anatarajia kuwa katika benchi la ufundi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Aston Villa utakaochezwa leo katika Uwanja wa White Hart. Redknapp mwenye miaka 64 ambaye anatajwa Uingereza alikuwa nje katika baadhi ya mechi za ligi za ligi hiyo pamoja na ule wa ligi ya Ulaya dhidi ya Rubin Kazan baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa moyo. Meneja huyo amesema kwasasa anajisikia vyema hivyo anaweza kuwemo katika benchi la ufundi la timu hiyo ambalo alimwachia msaidizi wake Joe Jordan na Kelvin Bond wamsaidie wakati yeye akijiuguza. Akihojiwa meneja huyo amesema alipata wakati mgumu kukitizama kikosi chake ambacho kiliifunga Fulham mabao 3-1 ni afadhali angekuwepo uwanjani.
VILLAS-BOAS ADAI ANA UHAKIKA NA KIBARUA CHAKE.
MENEJA wa Chelsea Andre Villas-Boas amesisitiza kuwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich bado ana imani nae katika mipango ya muda mrefu pamoja na kupoteza michezo mitatu ya ligi kati ya minne waliyocheza. Mapema Jumapili uongozi wa Chelsea ulilaani vikali baadhi magazeti kuandika kuwa kuna nyufa zimejitokeza baina ya kocha huyo na uongozi wa klabu hiyo. Ambapo baada ya kipigo walichokipata kutoka kwa Liverpool cha mabao 2-1 kocha huyo amesema ana uhakika wa kibarua chake kwakuwa Abromovich hakulipa kiasi cha paundi milioni 13 kumuondoa katika klabu yake ya zamani ya Porto halafu alipe tena mihela hiyo kumuondoa katika klabu hiyo. Aliendelea kusema kuwa hilo sio suala la mmiliki huyo kuwa na subira kwakuwa walishazungumza kuwa wanatengeza kitu kipya katika klabu hii kwa ajili ya baadae. Baada ya kupoteza mchezo huo sasa Chelsea wako nyuma kwa alama 12 kwa vinara wa ligi hiyo Manchester City na Villas-Boas amekiri kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweka matumaini hai ya kunyakuwa kombe hilo.
Sunday, November 20, 2011
Saturday, November 19, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: UGANDA YATAJA KIKOSI CHAKE.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Uganda Bobby Williamson ameteua majina ya wachezaji 21 kwa ajili ya kuunda kikosi cha nchi hiyo kitakachopambana katika michuano Kombe la Challenge itakayoanza baadae mwaka huu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi Jumatatu Novemba 21 katika Uwanja wa Namboole jijini Kampala kabla ya kusafiri kuelekea Dar es Salaam baadae wiki ijayo. Akizungumzia suala hilo Ofisa Habari wa kikosi hicho alithibitisha uteuzi wa kikosi hicho ambacho amesema ni kikosi imara ambacho kitarejea na kombe hilo nyumbani. Kikosi hicho kinaundwa na makipa Adel Dhaira, Robert Odongkara na Ali Kimera, mabeki ni Simon Massa, Godfrey Walusimbi, Habibu Kavuma, Isaac Issinde, Andy Mwesigwa, Henry Kalungi. Wakati viungo watakuwa ni Mike Mutyaba, Sula Matovu, Moses Oloya, Vincent Kayizzi, Daniel Wagaluka, Tonny Mawejje, Mussa Mudde na Patrick Ochan huku washambuliaji wakiwa Brian Omony, Emmanuel Okwi, Mike Sserumaga na Robert Ssentongo.
ETO'O, AYEW, GERVINHO, KEITA, YAYA KUGOMBEA TUZO ZA BBC.
SHIRIKA la Utangazaji nchini Uingereza-BBC limeteua majina ya wachezaji watano wa Afrika watakaogombania tuzo ya mwanasoka bora kutoka Afrika wa shirika hilo mwaka huu. Mwaka jana Asamoah Gyan ndio alishinda tuzo hiyo ambapo mwaka huu katika mchuano huo wapo Andre Ayew anayekipiga katika klabu ya Marseille, Samuel Eto’o anayekipiga klabu ya Anzhi ya Urusi, Seydou Keita anayechezea klabu ya Barcelona, na Gervinho anayecheza Arsenal pamoja na Yaya Toure anayecheza Manchester City. Mshindi wa tuzo hiyo atachaguliwa kwa njia ya kupigiwa kura na mashabiki kwa njia ya ujumbe mfupi na mtandao ambapo mwisho wa kuchagua itakuwa ni Desemba 9 na mshindi atatangazwa wiki moja baadae. Kwa miaka ya karibuni Ayew amekuwa mchezaji tegemeo kwa klabu yake pamoja na nchi ameweza kuisaidia nchi yake kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku akiiongoza klabu yake ya Marseille kombe la Ligi Kuu ya Ufaransa pamoja na Kombe la Chama cha Soka cha nchi hiyo.
CONFEDERETION CUP: AFRICAIN NA MAS KUPEPETANA LEO KATIKA FAINALI YA KWANZA.
KLABU Africain ya nchini Tunisia itaikaribisha timu ya MAS ya Morocco leo Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho mchezo ambao hautahudhuriwa na mashabiki uwanjani. Wanasiasa nchini Morocco wamelalamika jinsi baadhi ya mashabiki wa timu ya Wydad Casablanca walivyonyanyaswa jijini Tunis wakati wa mchezo wa fainali ya pili ya Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika dhidi ya Esperance. Pia kulikuwa matatizo kwa mashabiki hao ambao walikuja kuishangilia timu yao katika Uwanja wa Ndege wa Tunis wakati wakiwa wanarudi nyumbani. Hatahivyo suala la kucheza bila mashabiki katika mchezo wa leo haihusiani na suala hilo kwasababu timu ya Africain tayari walipewa adhabu kufungiwa kwa mashabiki wake kwa mechi mbili kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wa makundi dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast. Klabu kongwe nchini Tunisia ambayo ina zaidi ya miaka 91 pia ilitozwa faini ya dola 100,000 na kuonywa kuwa endapo mashabiki wake wakirudia tabia za vurugu basi wataondolewa kabisa katika michuano hiyo na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.
BULGARIA WATOZWA FAINI KWA UBAGUZI.
SHIRIKISHO la Soka la Bulgaria-BFU limetozwa faini ya Euro 40,000 na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa ushangiliaji wa kibaguzi waliofanya mashabiki wa nchi hiyo katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya dhidi ya England uliofanyika mwezi Septemba. Katika taarifa yake waliyoituma kwa njia ya mtandao UEFA imesema mashabiki hao waliokuwa nyumbani walikuwa wakishangilia huku moja kwa moja wakiwatupia maneno ya kibaguzi wachezaji wa Uingereza katika mchezo wao huo uliofanyika jijini Sofia Septemba 2. Pamoja na juhudi za BFU kupinga masuala kibaguzi kumekuwa na matukio machache katika nchi ya Balkan katika miaka ya karibuni. Mashabiki wa klabu ya CSKA Sofia walikuwa wakipiga kelele za nyani kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Djibril Cisse wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2005. UEFA imewapa BFU siku tatu za kukata rufani kupinga adhabu hiyo.
MARADONA NAE AMSHUKIA BLATTER.
MCHEZAJI nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona amedai hatua zichukuliwe dhidi ya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu suala la ubaguzi kwenye mchezo mapema wiki hii. Blatter alitoa kauli iliyoleta utata miongozi mwa wadau wengi wa mchezo huo akidai suala la ubaguzi baina ya wachezaji halipo na kama likitokea basi linaweza kumalizwa na wachezaji wenyewe kwa kushikana mikono baada ya mchezo.
Maradona akihojiwa juu ya suala hilo wakati na mkutano na waandishi wa habari huko Falme za Kiarabu-UAE amesema bosi huyo wa FIFA ameshafanya makosa mengi kabla mengine yakitokana na maamuzi yake na mengine kauli zake hivyo hiyo sio mara yake ya kwanza. Maradona aliongeza kusema kuwa ubaguzi haukubaliki na Blatter na FIFA huwa wanachukua hatua haraka kwasababu matokeo yake huwa sio mazuri kwa mchezo hivyo vitendo vinatakiwa kupingwa vikali lakini akahoji kwanini hatua hazichuliwi dhidi ya bosi huyo. Kwasasa Maradona ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Argentika katika fainali za Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 anakinoa kikosi cha timu ya Al Wasl ya huko Uarabuni.
Maradona akihojiwa juu ya suala hilo wakati na mkutano na waandishi wa habari huko Falme za Kiarabu-UAE amesema bosi huyo wa FIFA ameshafanya makosa mengi kabla mengine yakitokana na maamuzi yake na mengine kauli zake hivyo hiyo sio mara yake ya kwanza. Maradona aliongeza kusema kuwa ubaguzi haukubaliki na Blatter na FIFA huwa wanachukua hatua haraka kwasababu matokeo yake huwa sio mazuri kwa mchezo hivyo vitendo vinatakiwa kupingwa vikali lakini akahoji kwanini hatua hazichuliwi dhidi ya bosi huyo. Kwasasa Maradona ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Argentika katika fainali za Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 anakinoa kikosi cha timu ya Al Wasl ya huko Uarabuni.
Friday, November 18, 2011
BLATTER AOMBA RADHI.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ameomba msamaha kufuatia kauli yake iliyoleta mtafaruku kuhusiana na suala la ubaguzi. Bosi huyo wa FIFA Jumatano wiki hii alitoa kauli inayosema kuwa suala ubaguzi viwanjani linatakiwa kumalizwa kwa wachezaji kushikana mikono baada ya mchezo. Blatter amesema ameumizwa na bado anaumia kufuatia kauli yake hiyo iliyoleta mtafaruku na kukiri kuwa haikuwa kauli nzuri na anajutia kufanya hivyo.
Aliendelea kusema kuwa unapofanya kitu ambacho sio sahihi unachoweza kufanya ni kuomba msamaha na aliwaomba msamaha wote walioathirika kutokana na kauli kauli yake hiyo. Lakini alipoulizwa kuhusu suala la baadhi ya wadau waliomtaka ajiuzulu kutokana na kauli yake hiyo alisema haoni sababu ya kufanya hivyo.
Aliendelea kusema kuwa unapofanya kitu ambacho sio sahihi unachoweza kufanya ni kuomba msamaha na aliwaomba msamaha wote walioathirika kutokana na kauli kauli yake hiyo. Lakini alipoulizwa kuhusu suala la baadhi ya wadau waliomtaka ajiuzulu kutokana na kauli yake hiyo alisema haoni sababu ya kufanya hivyo.
"TEVEZ HANA NAFASI KATIKA KIKOSI CHANGU." MANCINI.
MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amemfungia milango mshambuliaji wake Carlos Tevez ambaye yuko kwao Argentina bila ruhusa ya klabu hiyo. Mancini alimtaka mchezaji huyo kumuomba msamaha mapema mwezi huu baada ya mchezaji huyo kukaa kupasha misuli moto katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya dhidi ya Bayern Munich uliochezwa mwezi Septemba mwaka huu. Meneja huyo aliondoa nafasi hiyo leo wakati akihojiwa katika mkutano na waandishi wa habari waliomuuliza kama kuna uwezekano wa mchezaji huyo kumjumuisha katika kikosi chake. Meneja huyo alijibu kuwa hakuna nafasi hiyo kwa mchezaji huyo tena.
WENGER AFURAHIA HENRY KUFANYA MAZOEZI NA VIJANA WAKE.
MENEJA wa timu Arsenal Arsene Wenger ana matumaini kuwa kuwepo kwa mshambuliaji wa timu hiyo wa zamani Thierry Henry katika mazoezi kutaongeza chachu ya ushindi katika kikosi chake ambacho kitapambana na Norwich kesho katika mchezo wa ligi. Henry mwenye umri wa miaka 34 ambaye pia aliwahi kuwa kuwa nahodha wa kikosi hicho amejiunga na klabu hiyo kwa ajili ya mazoezi ya kujiweka fiti wakati huu ambao timu yake ya New York Red Bulls imetolewa katika hatua ya mtoano wa ligi ya Marekani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa aliondoka Arsenal na kuhamia Barcelona mwaka 2007 na Wenger alifurahi kumuona mchezaji huyo tena akiwa mazoezini na vijana wake kwa ajili ya kujiweka fiti.
20 WAITWA NGORONGORO HEROES.
Kocha Mkuu wa timu za Taifa za vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kitakachoshiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA). Michuano hiyo itafanyika Gaborone, Botswana kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama wa COSAFA na Tanzania inayoshiriki kama mwalikwa. Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga). Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars). Ngorongoro Heroes ambayo iko kundi D pamoja na Zambia, Afrika Kusini na Mauritius inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 30 mwaka huu kwenda Gaborone.
TENGA KUFUNGA KOZI YA CAF.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga kesho atafunga kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyofanyika kuanzia Novemba 7 mwaka huu. Ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 30 utafanyika kuanzia saa 4.30 asubuhi katika ofisi za TFF. Kozi hiyo iliendeshwa na wakufunzi wanne, mmoja wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wawili wa CAF na mmoja wa Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU). Mkufunzi wa FIFA alikuwa Jan Poulsen, kutoka CAF ni Sunday Kayuni (Tanzania), Kasimawo Laloko (Nigeria) wakati kutoka Denmark ni Kim Poulsen. Makocha walioshiriki ni Christopher Eliakim, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Mussa Furutuni, Mecky Maxime, Gideon Kolongo, Maka Mwalwisi, Haji Amir, Tiba Mlesa, Stephen Matata, Wane Mkisi, Leonard Jima na Ahmed Mumba. Wengine ni Peter Mhina, Absolom Mwakyonde, Maarufu Yassin, Mussa Kamtande, Wilfred Kidau, Eliasa Thabit, Dismas Haonga, Fulgence Novatus, Juma Mgunda, Hassan Banyai, Mohamed Tajdin, Sebastian Nkoma, Emmanuel Massawe, Gabriel Gunda, Abdul Nyumba na Richard Kabudi.
CLUB WORLD CUP: BARCA KUKUTANA NA MABINGWA WA AFRIKA.
MABINGWA wa soka barani Ulaya klabu ya Barcelona inatarajia kupambana na mshindi kati timu ya Esperance au Al-Sadd katika nusu fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia. Ratiba hiyo ilipangwa Alhamisi ambapo kikosi cha Barcelona kinachoongozwa na kocha Pep Guardiola kitapambana na aidha Esperance kutoka Tunisia ambao ni mabingwa wa Afrika au Al- Sadd ya Qatar ambao ni mabingwa wa bara la Asia. Rais wa Esperance Riadh Bennour amesema ratiba hiyo ni nzuri pamoja na kwamba watu wengi wanategemea kuona mchezo wa fainali ya michuano hiyo zicheze timu za Barcelona na Santos ya Brazil. Aliongeza pamoja na watu kutegemea hivyo wao watajaribu kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanaingia fainali na kucheza na timu mojawapo kati ya hizo. Michuano hiyo ambayo hukusanya viabu bingwa kutoka katika kila bara duniani inatarajiwa kufanyika Japan katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.
Thursday, November 17, 2011
28 WAITWA KILIMANJARO STARS.
KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars Jamhuri Kihwelu ametaja majina ya wachezaji 28 watakaounda kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Challenge yanayotarajiwa kuanza Novemba 25 mpaka Desemba 10 mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam, kocha huyo amesema kikosi hicho kinatarajiwa kuweka kambi Ijumaa Novemba 18 katika Hoteli ya Rainbow ambapo watakaa hapo kwa muda wa wiki moja kabla kufanya mchujo na kubakiwa na wachezaji 20 wataounda kikosi hicho. Amesema katika kikosi hicho kutakuwa na makipa Juma Kaseja ambaye atakuwa nahodha wa kikosi hicho, Deo Mushin na Shaban Kado mabeki ni Shomari Kapombe, Godfrey Taita, Juma Jabu, Paulo Ngelema, Erasto Nyoni, Salum Telela na Juma Nyoso. Viungo watakuwa ni Shaaban Nditi, Ibrahim Mwaipopo, Nurdin Bakari, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Ramadhani Chombo, Jimmy Chogy, Mohamed Sudi, Nizar Khalfan, Rashid Yusuph na Said Morad wakati washambuliaji watakuwa ni Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, John Bocco na Gaudence Mwaikimba, Hussein Javu na Daniel Ruben.
RIO ASHANGAZWA NA KAULI YA BLATTER KUHUSU UBAGUZI.
BEKI wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema amshangazwa na madai ya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter akidai kuwa hakuna ubaguzi katika mchezo wa mpira uwanjani. Blatter alijichanganya katika kauli yake akzungumzia suala la ubaguzi uwanjani kuwa linaweza kutatuliwa kwa wachezaji kupeana mikono baada ya mchezo ingawa baadae alidai kuwa ameeleweka vibaya. Katika mtandao wa kijamii wa Twitter Ferdinand aliandika ujumbe wa kuonyesha kushangazwa na kauli hiyo kwa kusema kuwa anaweza kuwa amekosea kusoma matamshi ya Blatter aliyotoa na kama hajakosea kosea kusoma basi ameshangazwa na kauli ya kiongozi huyo. Ferdinand baadae alimtumia ujumbe kwa Blatter. Katika ujumbe huo aliosema kuwa matamshi yake kuhusiana na ubaguzi yanashangaza na kwa kweli yanachekesha na iwapo mashabiki watapaza sauti zao kwa maneno ya kibaguzi jee kushikana mikono hapo ni sawa? Matamshi ya Blatter yamekuja wakati nahodha wa Chelsea John Terry akichunguzwa na polisi pamoja na Chama cha Soka cha Uingereza-FA juu ya tuhuma za kumtamkia maneno ya kibaguzi mlinzi wa QPR Anton Ferdinand, ambaye ni mdogo wake Rio.
Wednesday, November 16, 2011
HIDDINK KIBARUA CHAOTA NYASI UTURUKI.
Guus Hiddink amekatishiwa mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Uturuki baada ya nchi hiyo kushindwa kufuzu kwa fainali za Kombe la Euro mwaka 2012. Uturuki ilipoteza kwa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Croatia baada ya kwenda sare ya kutofungana mechi ya pili siku ya Jumanne.Shirikisho la Kandanda la Uturuki - TFF - limesema wamefikia makubaliano kumaliza mkataba wa mwalimu huyo wa zamani wa Chelsea, ambao ulikuwa umalizike mwakani. Hiddink, mwenye umri wa miaka 65, alichukua kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Uturuki mwezi wa Agosti mwaka 2010 na nchi hiyo ilishika nafasi ya pili katika kundi A. Hiddink alishawahi kuwa mwalimu wa timu za taifa za Uholanzi, Korea Kusini, Australia na Urusi, pamoja na vilabu vya PSV Eindhoven, Real Madrid na Chelsea. Taarifa rasmi iliyotolewa na TFF katika mtandao imesema: "Tungependa kumshukuru Bw Guus Hiddink kwa kazi yake wakati akiifundisha timu yetu ya taifa, na tunamtakia kila la kheri katika kazi yake siku za usoni."Katika mahojiano kabla ya mechi siku ya Jumanne alisema alitazamia kumaliza kufanya kazi na Uturuki na akaongeza: "Nilifanya kazi kwa ajili ya kuijenga timu kwa siku za mbele lakini nadhani hii itakuwa mechi yangu ya mwisho na timu hii - ukweli ndio huo."Hiddink, anayeaminika ni mmoja wa mameneja hodari wa kandanda, inasemekana bado anahitajika sana na vilabu kama Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Anzhi Makhachkala zimeonesha tamaa ya kutaka kumchukua.
CECAFA CHALLENGE CUP: KILIMANJARO STARS KUANZA KAMPENI YAKE DHIDI YA RWANDA.
Mabingwa watetezi wa michuano ya Afrika Mashariki na kati timu ya Tanzania Bara Kilimajaro Stars itaanza kampeni ya kutetea Ubingwa wake dhidi ya Rwanda katika michuano ya mwaka huu. Michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la vyama vya michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Cecafa inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 25 hadi Decemba 10 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa hii leo siku ya ufanguzi kutakuwa na michezo miwili ambapo timu ya Burundi itacheza dhidi yaSomalia wakati Zanzibar Heroes wakicheza dhidi ya Uganda. Kwa upande wake Rais wa Cecafa LEODGER TENGA amesema timu ya Eritrea imejitoa katika michuano hiyo hivyo nafasi kuchukuliwa na timu kutoka Namibia. Kuingia kwa Namibia kumefanya michuano ya mwaka huu kuwa na timu mbili ikiungana na Malawi ambayo ilishatangwazwa huko nyuma. Mashindano hayo yatafanyika katika kituo kimoja cha Dar es salaam kutokana na Mkoa wa Mwanza kushindwa kupata wadhamini wakuendesha mashindano Mkoani humo. Katika hatua nyingine TENGA ameipongeza timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2014.
UEFA 2012: HISPANIA, UHOLANZI KUONGOZA DRAW YA UEFA.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA wamethibitisha nchi za Hispania na Uholanzi ndio zitakuwa timu za juu pamoja na wenyeji Poland na Ukraine katika mchakato wa kupanga ratiba ya michuano ya Kombe la Ulaya 2012. Nchi za Ujerumani, Uingereza, Urusi na Italia zitakuwa zinafuatia katika mchakato huo unaotarajiwa kufanyika Desemba 2 mwaka huu jijini Kiev ambapo timu 16 zitagawanywa katika makundi. Nafasi za tatu zitakuwepo nchi za Croatia, Ugiriki, Ureno na Sweden wakati nafasi za nne zitakuwa nchi za Denmark, Ufaransa, Jamhuri ya Czech na Ireland. Katika taarifa yake UEFA imesema timu hizo zimepangwa kutokana na nafasi zao katika orodha ya timu bora duniani.
AC MILAN YAMNYATIA DROGBA DIRISHA DOGO.
MAKAMU wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani amesema angependa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwakani. Timu hiyo vigogo nchini Italia hivi inakabiliwa na upungufu upande wa ushambuliaji baada ya mshambuliaji wake Antonio Cassano kuwa nje kwa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Galliani angependa pia kumsajili Nocolas Anelka au Mario Balotelli lakini akakiri kuwa Drogba ndiye chaguo lake la kwanza. Galliani amesema akiliambia gazeti moja nchini humo kuwa muda mrefu amekuwa akimpenda mshambualiaji huyo toka alipokuwa akicheza katika klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa.
EURO 2012: URENO, CZECH REPUBLIC NA CROATIA ZAFUZU.
TIMU za taifa za Ureno, Czech Republic na Croatia zimefuzu kucheza michuano ya Ulaya inayotarajiwa kufanyika mwakani. Ureno walifuzu kucheza michuano hiyo kwa kuifunga Bosnia mabao 6-2 katika michezo miwili waliyocheza wakati Jamhuri ya Czech wao walifuzu baada ya kuifunga Montenegro mabao 3-0 katika michezo miwili waliyocheza. Pamoja na Suluhu ya bila ya kufungana waliyopata Croatia dhidi ya Uturuki nchi hiyo ilisonga mbele baada ya kupata ushindi mnono 3-0 katika mchezo wa kwanza jijini Istanbul wakati Jamhuri ya Ireland nao waliingia katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Estonia na kutimiza idadi ya mabao 5-1 katika michezo miwili waliyokutana. Mbali ya hizo nchi nyingine ambazo zimeshafuzu kucheza michuano hiyo ni pamoja na Poland na Ukraine ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo nyingine ni Ujerumani, Urusi, Italy, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Denmark, Hispania na Sweden.
ROAD TO BRAZIL: TANZANIA, KENYA, UGANDA ZAFUZU HATUA YA MAKUNDI.
Golikipa wa timu ya Chad akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na mshambualiaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu katika baina ya timu hizo ulichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. |
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo wa Taifa Stars na Chad. |
Michezo mingine iliyochezwa jana ni Rwanda iliibamiza Eritrea kwa mabao 3-1 na kusonga mbele kwa idadi ya mabao 4-1 katika michezo miwili waliyocheza, Equatorial Guinea nayo ilisonga mbele licha kipigo cha mabao 2-1 walichokipata jijini Antananarivo. wakati Jamhuri ya Didemokrasia ya Kongo-DRC wao waliendeleza ubabe kwa timu ya Swaziland kwa kuichapa mabao 5-1 jijini Kinshasha na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 8-1.
Tuesday, November 15, 2011
REAL-BARCA CLASICO DATE ANNOUNCED.
MCHEZO wa mahasimu wa soka nchini Hispania kati ya Real Madrid na Barcelona unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Desemba 10 mwaka huu tarehe ambayo ilitangazwa jana. Madrid walikuwa wanataka mchezo huo uchezwe Jumapili mchana Desemba 11 ili wadau wao katika bara la Asia wapate kushuhudia mchezo huo. Hatahivyo Barcelona walipinga suala hilo na kusisitza mchezo huo uchezwe Jumamosi ili kutoa nafasi ya timu hiyo kuondoka mapema kwenda kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika Japan ambapo timu inatarajiwa kusafikiri asubuhi ya Jumapili mara baada ya mchezo huo wa jumamosi. Barcelona haijawahi kupoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu ya Hispania-La Liga toka kocha wake Pep Guadiola alipochukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwaka 2008 ingawa Madrid walifanikiwa kuifunga Barcelona katika mchezo mmoja wa Kombe la Mfalme. Madrid ndio wanaoongoza ligi kwasasa wakiwa na tofauti ya pointi 3 mbele ya mahasimu wao hao huku wakiwa wamebakisha michezo mitatu kabla hajakutana.
Monday, November 14, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: WAAMUZI 19 WAINGIA KATIKA USAILI.
BARAZA la Soka kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati-CECAFA limeteua waamuzi 19 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Challenge inayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 mwaka huu. Kenya ndio imetoa waamuzi wengi zaidi ktika uteuzi huo ambao ni Davies sagero, Brasan Mamati na Davies Omweno wengine ni Denis Batte (Uganda), Bamlak Tessema(Ethiopia), Wish Yabarow (Somalia) na Eric Gasinzigwa (Burundi). Waamuzi wasaidizi watakuwa ni pamoja na Hassan Yacin Egueh (Djibouti), Idam Mohamed Hamid (Sudan), Yohanes Girmai (Eritrea) na Mark Sonko (Uganda). Waamuzi hao wanatarajiwa kupewa semina na majaribio kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya michuano hiyo itayochezwa katika miji miwili Dar es Salaam na Mwanza ambapo mwishoni mwa semina hiyo waamuzi wote watafanyiwa vipimo vya afya na watakaofaulu ndio watakaoteuliwa kuwa waamuzi wa michuano hiyo. Wenyeji Kilimanjaro Stars ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo walishinda mwaka jana baada ya kuifunga Ivory Coast kwa 1-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
MISRI YAKUBALI KIPIGO CHA MABAO 2-0 DHIDI YA BRAZIL, HASSAN AWEKA REKODI.
KIUNGO mkongwe wa timu ya Taifa ya Misri Ahmed Hassan ameweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kimataifa baada ya kucheza mchezo wake wa 178 wakati timu yake ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Brazil katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika Doha, Qatar. Hassan ambaye ana umri wa miaka 36 alianza kukichezea kikosi hicho mapema mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 20 ambapo sasa amelingana na golikipa wa Saudi Arabia Mohamed Al Deayea ambaye alistaafu kucheza soka la kimataifa mwaka 2006. Kiungo huyo aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Hosni Abd Rabou na mara moja alikabidhiwa kitambaa cha unahodha alichokuwa amevaa Wael Gomaa.
Katika mchezo mshambuliaji anayechezea klabu ya Valencia ya Hispania Jonas ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Brazil bao la kwanza akiwa amefunga dakika ya 39 kabla kumalizia linguine dakika ya 59.
Katika mchezo mshambuliaji anayechezea klabu ya Valencia ya Hispania Jonas ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Brazil bao la kwanza akiwa amefunga dakika ya 39 kabla kumalizia linguine dakika ya 59.
UEFA KUWAJADILI MASHABIKI WAKOROFI WA CELTIC.
KAMATI Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA linatarajiwa kusikiliza kesi ya ushangiliaji mbaya uliokuwa ukifanywa na mashabiki wa klabu ya Celtic wakati wa mchezo Ligi ya Ulaya baina ya timu hiyo na Rennes. Kamati hiyo ya UEFA inatarajia kusikiliza kesi hiyo Desemba 8 mwaka huu ambapo katika mchezo baina ya timu hizo mashabiki w Celtic walisikika wakiimba nyimbo za kuchukiza katika mchezo huo ulifanyika Novemba 3 katika Uwanja wa Celtic Park. Uefa imesema katika shauri hilo hakutakuwa na umuhimu wa kuwepo kwa mwakilishi kutoka Celtic. Msemaji wa UEFA amesema kama ni kweli tuhuma hizo ni za kweli dhidi ya mashabiki hatua kali zitachukuliwa kwakuwa mambo hayo hayakubaliki mchezoni na inaweza kuvuruga amani.
Subscribe to:
Posts (Atom)