CHIPUKIZI wa Manchester United, Marcus Rashford ameitwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Uingereza ambao watakwenda kushiriki michuano ya Euro 2016 huko Ufaransa. Rashford mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa wakati Uingereza waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Australia katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Ijumaa iliyopita. Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge naye pia amejumuishwa lakini Andros Townsend wa Newcastle United na Danny Drinkwater wa Leicester City wote wameachwa katika kikosi hicho. Uingereza inatarajiwa kuchuana na Ureno katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambapo wanatarajiw akupambana na Urusi Juni 11 mwaka huu.
Kikosi kamili ni
Kipa: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).
Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).
Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal).
Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).